Kuangazia Mwenyeji Bingwa: kuchangamsha nyumba baada ya msiba

Mjane anasimulia jinsi kukaribisha wageni wa kimataifa kulimsaidia kupona.
Na Airbnb tarehe 8 Feb 2019
Inachukua dakika 3 kusoma
Imesasishwa tarehe 3 Apr 2025

Mwenyeji Bingwa Marianne ghafula tu akajikuta peke yake kwenye nyumba iliyosanifiwa vizuri ambayo yeye pamoja na marehemu mume wake waliirekebisha pamoja. Ili aweze kujiinua, alianzisha biashara yake, akifungua nyumba yake ya California kwa wageni kutoka duniani kote. Kwa maneno yake mwenyewe, anasema namna ambavyo kukaribisha wageni kuliyapatia maisha yake maana mpya na kile kinachomaanisha kuwa mjasiriamali mwanamke:

Kulikuwa na jambo la manufaa kuhusu kuwa na maisha, kuwa na watu wanaorudi kwenye nyumba yako.

Nilipompoteza Mike, kulikuwa na hisia kubwa saa ya kupoteza, ya utupu. Alikwenda kufanyiwa upasuaji mwezi Mei mwaka 2017 kwa kile kilichopaswa kuwa upasuaji wa kawaida, lakini changamoto zilijitokeza na hakufanikiwa kutoka akiwa hai. Siku nne kabla ya tukio hili, tulikuwa tumesherehekea miaka 26 ya kuwa pamoja.

Binti yangu alikuwa amehamia nyumbani ili aishi na mimi. Karibu mwaka mmoja baadaye, alihama na ghafla nilijikuta nikiwa peke yangu nyumbani.

Sikumbuki tukio au sababu mahususi iliyonifanya nianze kukaribisha wageni. Iliendelea kujitokeza katika ufahamu wangu. Baadaye nilisafiri mwezi Septemba mwaka 2017 kwenda kuwasalimia marafiki huko Oregon, na hapo nilikaa kwa mwenyeji wa Airbnb. Yule mwenyeji alikuwa mtu mwema, na nilimsimulia kile kilichotokea. Nilianza kuhisi kwamba kuwa mwenyeji kunaweza kuwa jambo linalowezekana kwangu.

Kwa kifo cha mume wangu, pensheni yake ilisitishwa na huo ulikuwa upotevu mkubwa wa mapato. Nimejiajiri kama mwalimu, mwandishi na mbunifu wa uso wa ardhi. Sikuwa mahali ambapo ningeweza kuweka mkazo.

Katika mawazo yangu, Airbnb kilikuwa chanzo cha kupata fedha kwa urahisi. Lakini ni kazi. Na kuwa mwanamke asiye na mume, nilikuwa na wasiwasi kuhusu usalama. Nilinunua makufuli kwa ajili ya vyumba vya wageni na chumba changu, lakini nadhani nilifunga mlango wangu mara moja tu wakati ambapo kulikuwa na mtu anaingia usiku sana. Rafiki yangu ambaye pia ni mwenyeji alinishauri niandike maelezo kuhusu nyumba yangu ili kuwavutia watu ninaowahitaji hapa, na hadi sasa ushauri huu unaonekana kuwa umefanya kazi. Labda ni ujinga, lakini nina imani fulani kwamba kwa sehemu kubwa, watu ni wema.

Kukaribisha wageni kukawa njia ya kupunguza hali ya upweke. Ikawa sababu ya kudumisha usafi wa nyumba, sababu ya kuwa na sura ya ujasiri. Unapaswa ujinyanyue kidogo. Hayo yote yalikuwa mambo mazuri.

Nakumbuka Mike akiwa na kila mtu anayeingia. Inasikitisha lakini pia inatia nguvu.

Alipenda kufanya kazi kwenye nyumba hii. Alikuwa seremala. Tuliponunua nyumba hiyo mnamo mwaka 1995, ilikuwa imeharibika na kuhitaji marekebisho naye akaifanya iwe mahali pazuri pa kuishi. Kwa njia nyingine, napata uzoefu wa hisia yake, msisimko wake wakati watu wanaingia kwenye nyumba, wanaangalia useremala na kusema, "Lo!"

Najisikia fahari sana. Ninaihisi kwa ajili yetu sote. Ni jambo zuri kiasi gani kwamba ninaweza kuishiriki hiyo.

Mwanzoni nilikuwa nawaambia wageni kwamba nimempoteza mume wangu. Kisha kidogo kidogo, halikuwa jambo ambalo nilikuwa naanza kuwaelezea.

Nimebarikiwa sana na wageni ambao wamekuwa wakija kwangu. Kwa kuwa ninaishi Santa Monica, walitaka kwenda ufukweni, kwenye gati, na Venice, kwa hivyo kwa kweli sikuwaona. Bado nilikuwa nahitaji sehemu kubwa zaidi na utulivu mwingi, kwa hivyo lilikuwa jambo zuri kabisa.

Mara kadhaa, tulikuwa tukizungumza huku tukinywa kahawa au tukiwa tumekaa kwenye bembea ya baraza tukiwa na glasi ya mvinyo huku tukipata upepo mwanana wa bahari. Baadhi ya wageni walikuwa watu wazuri kuzungumza nao. Lilikuwa ni jambo la kukumbusha kwamba maisha yanaendelea, kama yanavyosikika kiistiari

Kukaribisha wageni kukawa njia ya kupunguza hali ya upweke.
Marianne,
Santa Monica, California

Mgeni mmoja alikuwa msichana. Sikuwa nimetaja kwamba Mike alikuwa amekufa, lakini labda aliona picha zake kwenye nyumba. Aliniambia kwamba alikuwa amempoteza mpenzi wake miezi michache iliyopita katika ajali. Kwa hivyo nilijikuta katika nafasi hii nzuri ya kuweza kufungua si nyumba tu, bali sehemu ya kumwezesha kuzungumza kuhusu msiba wake na mtu anayeelewa. Na kwa upande wangu, alikuwa mtu ambaye ningeweza kuzungumza naye kuhusu Mike. Kulikuwa na msingi wa uafikiano, sadifa ya ajabu. Tumeandikiana ujumbe mfupi mara kadhaa. Anaweza kurudi au asirudi, lakini kwa muda mchache tuligusana maisha.

Kama wenyeji, tunashiriki sehemu ya kukaa, lakini wakati mwingine tunashiriki mambo mengi zaidi.

Kwa kufungua nyumba yangu, niliweza kutoa kitu fulani hata wakati ambapo nilihisi nimeishiwa kabisa.

Sasa nina biashara yangu mwenyewe. Na kuna mambo mengi ya kusemwa kuhusu kuwa mmiliki wa biashara na kuwa na udhibiti kamili kuhusu vile unavyoendesha maisha yako. Kuna maana ya kweli ya hisia ya nguvu ya mwanamke pale anapokuwa anaendesha biashara yake.

Linaweza kuonekana kwa watu kuwa ni suala la imani isiyokuwa na msingi, lakini kuna kitu kitakatifu sana kuhusu kumkaribisha mtu usiyemjua. Kama wenyeji, tunahudumu kama waongozaji wa wasafiri waliochoka. Na wakati tunapopata maumivu, kuumia na upweke, mwingiliano na uhusiano huo unatoa uponyaji kwa kiasi fulani.

Picha kwa hisani ya Marianne

Airbnb
8 Feb 2019
Ilikuwa na manufaa?