Fanya mchakato wa kuingia na kutoka uwe rahisi
Kuingia na kutoka ni nyakati muhimu ambazo zinaweza kuleta au kuvunja ukaaji wa nyota tano. Wageni wanatarajia kuingia ndani kwa urahisi, kuhisi wamekaribishwa na kuondoka bila shida.
Rahisisha mchakato wa kuingia
Wageni wanataka kujua jinsi ya kufika kwako na kufungua mlango wa mbele wanapowasili. Angalia njia za kurahisisha mchakato wa kuingia:
Boresha sehemu yako. Fikiria maboresho ya nyumba kama vile kuweka kufuli janja, mwangaza wa nje au ishara ili kuufanya mchakato wa kuingia uwe rahisi kwako na kwa wageni wako.
- Shiriki maelezo kamili. Nenda kwenye Mwongozo wa kuwasili wa tangazo lako ili kuweka au kurekebisha njia yako ya kuingia na muda, maelekezo, mwongozo wa nyumba, nenosiri la Wi-Fi na kadhalika. Wageni hupokea taarifa hii baada ya kuweka nafasi.
- Onyesha hatua za kuingia ndani. Weka picha au video ili kuwasaidia wageni kuingia. Kwa mfano, unaweza kupiga picha ya kikomeo kinachofungua lango la mbele.
- Hakiki mwongozo wako. Gusa kitufe cha Angalia ili uone taarifa yako ya kuwasili kama wageni wanavyoona. Mwombe rafiki afanyie majaribio maelekezo yako na afanye marekebisho yoyote yanayohitajika kwa ajili ya kuingia kwa urahisi.
Wageni wanaweza kukutumia ujumbe wenye maswali kuhusu kuingia. Jibu haraka kadiri iwezekanavyo, hasa ndani ya saa 24 kabla ya kuwasili kwake.
Wasaidie wageni wajisikie wamekaribishwa
Jinsi unavyowasalimu wageni na kutarajia mahitaji yao ni sifa za ukarimu mkubwa. Kuzingatia hata mambo madogo zaidi kunaweza kuwa na matokeo makubwa kwa wageni.
Ratibu ujumbe wa ukadirbisho. Siku ya kuingia, wajulishe wageni kwamba unapatikana ikiwa wanahitaji chochote.
Tekeleza ukarimu jumuishi. Kumbuka kwamba wageni huenda wasiwe na imani au desturi kama zako.
Kuwa mtu wa kujali. Onyesha kupendezwa na wageni wako na uweke kipaumbele kwa mahitaji yao huku pia ukiheshimu faragha yao.
Rie, mwanabodi wa Bodi ya Ushauri ya Wenyeji na Mwenyeji Bingwa huko Yomitan, Japani, anapenda kuandika ujumbe wa ukaribisho wenye taarifa muhimu za mahali husika. "Ikiwa ni mzazi ambaye ameniambia anakuja na familia ya mtoto mchanga, nitapendekeza duka zuri la kununua nepi," anasema. "Ikiwa wana mbwa, ninapendekeza mahali pa kununua chakula chenye ubora wa juu cha wanyama vipenzi."
Acha mvuto wa kudumu
Fikiria kutoka kama uzoefu wa mwisho wa wageni wako kwenye sehemu yako. Unataka wakumbuke uzoefu mzuri wa ukaaji waliopata.
Tumia mwongozo wa Kuwasili ili kutoa maelekezo ya kutoka yaliyo wazi na rahisi. Fikiria endapo kazi za kutoka kama vile kuondoa taka au kukusanya taulo zilizotumika ni huduma ya nyota tano kwa wageni. Kufanya kazi hizi kuwa sehemu ya utaratibu wako wa kufanya usafi kunaweza kusababisha tathmini bora.
Baada ya kila ukaaji, watumie wageni ujumbe wa shukrani. Waalike warudi, na uwajulishe kwamba unathamini maoni yao. Muulize atathamini nini wakati atakapokuja tena wakati ujao.
Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.