Jinsi ya kutoa huduma ya kuingia mwenyewe kwa ajili ya kuwasili kwa urahisi

Weka kufuli janja, kicharazio au kisanduku cha funguo kwa ajili ya ufikiaji rahisi wa nyumba yako.
Na Airbnb tarehe 20 Jul 2020
Inachukua dakika 2 kusoma
Imesasishwa tarehe 13 Ago 2024

Huduma ya kuingia mwenyewe ni mojawapo ya vistawishi 10 bora kwenye Airbnb. Wageni mara nyingi huchuja matokeo yao ya utafutaji kwa sehemu zinazotoa huduma hii.* Kuweka njia ya kuingia kama vile kufuli janja kunaweza kusaidia tangazo lako lionekane zaidi.

Kuwapa wageni njia rahisi ya kujiingiza pia kunaweza kuokoa muda wako, kufanya mchakato wa kuwasili uwe shwari na kusababisha tathmini bora.

Chagua njia ya kuingia

Njia maarufu zaidi za kuingia mwenyewe ni: kufuli janja, kicharazio na kisanduku cha funguo. Njia yoyote unayochagua, ni muhimu kumpa kila mgeni aliyeweka nafasi msimbo wa kipekee wa ufikiaji. 

Baada ya kuweka kufuli janja, kicharazio au kisanduku cha funguo katika sehemu yako, kumbuka kusasisha tangazo lako. Unaweza kuweka au kuhariri njia yako ya kuingia katika mwongozo wako wa kuwasili.

Weka maelekezo ya kuingia

Shiriki vidokezi vya jinsi ya kuingia ndani. Wageni hupokea maelekezo yako kiotomatiki saa 24 hadi 48 kabla ya kuingia. 

Eleza mahali pa kupata na jinsi ya kufungua na kufunga kufuli janja, kicharazio au kisanduku chako cha funguo. Unaweza kuweka picha kwa ajili ya uwazi.

Weka majibu ya haraka

Tumia violezo hivi vya ujumbe mfupi ili uokoe muda wa kujibu maswali ya kawaida ya kuingia. Kwa mfano, unaweza kuunda moja ya kutuma wakati wowote mgeni anapoomba maelekezo ya kuendesha gari au vidokezi vya maegesho.

Unaweza kuhariri kwa urahisi na kutuma majibu yako ya haraka wakati wowote unapotuma ujumbe kwa wageni.

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

*Kulingana na data ya Airbnb inayopima vistawishi vilivyotafutwa mara nyingi zaidi ulimwenguni kote kuanzia tarehe 1 Januari hadi tarehe 30 Juni, 2024.

Airbnb
20 Jul 2020
Ilikuwa na manufaa?