Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

Jinsi ya kufanya sehemu yako iwe yenye starehe kwa watu wanaofanya kazi wakiwa mbali

Vistawishi kama vile Wi-Fi ya kasi na sehemu mahususi ya kufanyia kazi vinaweza kuwavutia wageni.
Na Airbnb tarehe 11 Mei 2022
Inachukua dakika 4 kusoma
Imesasishwa tarehe 11 Mei 2022

Vidokezi

  • Sehemu mahususi ya kufanyia kazi inaweza kuwa rahisi kama meza iliyo karibu na soketi na kiti chenye kustarehesha

  • Toa Wi-Fi ya kasi na vistawishi vingine maarufu

Kufanya kazi ukiwa mbali kunavyoendelea kuwa jambo la kawaida katika maeneo mengi, tumeona mabadiliko makubwa katika jinsi na sababu za watu kusafiri. Hii inaweza kusababisha wageni wengi zaidi kuvutiwa na sehemu ambazo huwasaidia kufanya kazi zao mahali popote.

Hivi ndivyo unavyoweza kutoa vistawishi sahihi, kuweka sehemu mahususi ya kufanyia kazi na kutangaza sehemu yako.

Toa Wi-Fi ya kasi na ya kuaminika

Muunganisho wa intaneti ni wa lazima kwa watu wanaofanya kazi wakiwa mbali wanaotafuta Wi-Fi ya kasi na ya kuaminika ili kuwezesha simu za video na kazi nyingine.

Unaweza kuthibitisha kasi ya Wi-Fi ya tangazo lako bila kuondoka kwenye programu ya Airbnb kwa kutumia jaribio la kasi ya Wi-Fi. Nyenzo hii hukuruhusu kufanya majaribio ya kasi ya Wi-Fi ya nyumba yako, kisha kuionyesha moja kwa moja kwenye ukurasa wa tangazo lako—ili kukusaidia kuwavutia wageni wengi zaidi wanaohitaji muunganisho wa kasi.

Ikiwa maeneo fulani ya sehemu yako yana mawimbi dhaifu, nyongeza na viendelezi vya Wi-Fi vinaweza kuboresha utendaji wao. Inaweza pia kuwa muhimu kujifunza jinsi ya kuangalia ruta yako ukiwa mbali ili kufuatilia Wi-Fi yako.

Fanya jaribio la kasi ya Wi-Fi

Weka sehemu mahususi ya kufanyia kazi

Wageni wanatafuta sehemu mahususi za kufanyia kazi kama kistawishi muhimu—na kuunda moja ni rahisi kuliko unavyofikiria. Ili kuweka kistawishi hiki kwenye tangazo lako, utahitaji kutoa meza au dawati ambalo linatumika tu kwa ajili ya kufanya kazi, ufikiaji wa soketi na kiti chenye kustarehesha.

Kwa sababu wenzi wanaofanya kazi wakiwa mbali wanaweza kuhitaji sehemu tofauti, fikiria kuweka maeneo mawili ya kufanyia kazi. Unaweza kuwajulisha wageni kuhusu vipengele hivi kwa kuchagua Sehemu mahususi ya kufanyia kazi katika sehemu ya Vistawishi kwenye tangazo lako na kwa kuangazia sehemu zozote za kufanyia kazi katika maelezo ya tangazo lako, picha na maelezo mafupi.

Wenyeji ambao hawana nafasi ya kuweka sehemu mahususi ya kufanyia kazi bado wanaweza kuwakubali watu wanaofanya kazi wakiwa mbali. Wakati mgeni anahitaji kufanya kazi akiwa mbali, "Ninabadilisha mojawapo ya viti vya meza ya jikoni na kiti chenye magurudumu cha ofisini kilicho na takia," anasema Emilia, Mwenyeji Bingwa huko Orono, Maine. "Ninadhani kwamba kiti hicho peke yake huleta mabadiliko makubwa."

Fikiria vistawishi vingine muhimu

Zaidi ya sehemu mahususi ya kufanyia kazi, wageni pia wanathamini vitu vya ziada ambavyo vinaweza kufanya kazi ya mbali ipendeze na iwe yenye tija.

Haya ni baadhi ya machaguo ya kuzingatia kwa ajili ya sehemu yako:

  • Sehemu mbadala za kufanyia kazi. Sebule, chumba cha kulia au baraza zinaweza kutoa mazingira mapya ya kuburudisha na kuruhusu watu wengi kufanya kazi kwa wakati mmoja.
  • Usaidizi wa mkao. Kinara cha kompyuta mpakato, kiti cha ofisi kinachoboresha mkao na kikanyagio kinachoweza kurekebishwa vinaweza kusaidia kustarehesha siku za kazi zenye shughuli nyingi.
  • Mwangaza mzuri. Ingawa madirisha au milango ya kioo ambayo hutoa mwangaza wa asili ni bora, taa ya dawati inaweza kusaidia kuangaza sehemu ya kufanyia kazi.
  • Mashine ya kutengenezea kahawa na birika la chai. Wageni wengi hufurahia kutengeneza kahawa ili kuwasaidia wanapofanya kazi. Unaweza hata kutoa chai na kahawa—na ufanye zaidi ya ilivyotarajiwa, mwanablogu wa mtindo wa maisha Elsie, Mwenyeji Bingwa huko Nashville, Tennessee, anapendekeza kutoa machaguo kadhaa ya kutengeneza kahawa, kama vile aina ya "French press" na mashine ya kutengeneza kahawa kiotomatiki.
  • Vifaa vya ofisi. Vitu rahisi kama vile kalamu mpya na madaftari madogo mara nyingi huwa na manufaa, huku ufikiaji wa printa ukiweza kusaidia kutofautisha tangazo lako.
  • Usaidizi wa kiteknolojia. Skrini ya kompyuta, vipaza sauti mahiri na chaja za ziada za simu zinaweza kuboresha sehemu yako ya kufanyia kazi.
  • Mandharinyuma ya mkutano wa video. Karatasi ya ukutani inayovutia, mimea au michoro iliyoko kwenye mandharinyuma ya sehemu ya kufanyia kazi inaweza kuwavutia wageni ambao mara nyingi hupiga simu za video.
  • Kupunguza kelele. Nguo kama mapazia, mazulia, mablanketi na mito zinaweza kusaidia kupunguza mikengeusho yenye kelele.

Tangaza sehemu yako inayofaa kwa kazi

Mara baada ya kufanya sehemu yako iwe yenye starehe kwa watu wanaofanya kazi wakiwa mbali, ni muhimu kusasisha maelezo ya tangazo lako, vistawishi na picha ili kuwajulisha wageni kwamba una eneo linalofaa kwa kazi.

  • Tumia vizuri vichujio vya utafutaji. Wanapovinjari matangazo, wageni wengi hutumia vichujio kupata sehemu zilizo na vistawishi wanavyotaka, kwa hivyo hakikisha kwamba unaweka alama kwenye Sehemu mahususi ya kufanyia kazi na kitu kingine chochote unachotoa.
  • Sasisha picha zako na maelezo mafupi. Kwa sababu wageni wanaweza kuangalia picha za tangazo lako kabla ya kusoma maelezo, hakikisha kwamba picha zako zinajumuisha sehemu zozote za kazi unazotoa. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kupiga picha nzuri
  • Waruhusu wageni wajione wakiwa kwenye sehemu yako. Hakikisha kwamba maelezo ya tangazo lako yanaonyesha jinsi sehemu yako inavyopokea wageni wanaofanya kazi wakiwa mbali. Ikiwa kweli unataka kuonekana, unaweza kujumuisha taarifa hiyo katika kichwa cha tangazo lako.

Inaweza pia kuwa muhimu kutuma ujumbe kwa wageni kabla hawajawasili. Kwa kuwakumbusha iwapo unatoa vitu kama vile kahawa au monita ya kompyuta, unaweza kuwasaidia kupanga ipasavyo.

Tunatumaini kwamba vidokezi hivi vitakusaidia kuunda sehemu yenye makaribisho. Kwa kuzingatia mahitaji ya wageni wako, utaweza kutoa ukaaji unaostarehesha na wenye tija kwa watu wanaofanya kazi wakiwa mbali.

Vidokezi

  • Sehemu mahususi ya kufanyia kazi inaweza kuwa rahisi kama meza iliyo karibu na soketi na kiti chenye kustarehesha

  • Toa Wi-Fi ya kasi na vistawishi vingine maarufu
Airbnb
11 Mei 2022
Ilikuwa na manufaa?