Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

Vutia wageni ukitumia jaribio jipya la kasi ya Wi-Fi

Fahamu jinsi ya kuthibitisha na kuonyesha kasi ya Wi-Fi yako—kistawishi muhimu cha Airbnb.
Na Airbnb tarehe 11 Ago 2021
Inachukua dakika 3 kusoma
Imesasishwa tarehe 3 Nov 2021

Vidokezi

  • Wi-Fi ni mojawapo ya vistawishi maarufu zaidi ambavyo wageni hutafuta

  • Jaribio jipya la kasi ya Wi-Fi hukuruhusu kuthibitisha na kuonyesha kasi ya Wi-Fi yako

  • Fanya majaribio ya Wi-Fi yako—ikiwa itaonyesha kuwa Mbps 50 au zaidi, "Wi-Fi ya kasi" itaangaziwa kwenye tangazo lako

Wageni wengi hutegemea intaneti ya kasi ili kufurahia safari na ni muhimu kwa wageni wanaofanya kazi wakiwa mbali. Kwa kweli, utafiti wa Airbnb unaonyesha kwamba Wi-Fi ni mojawapo ya vistawishi ambavyo wageni hutafuta mara nyingi na kwamba kuweka meza ya kufanyia kazi kwa kompyuta mpakato kwenye vistawishi vya tangazo kunaweza kuwasaidia baadhi ya Wenyeji kuongeza mapato yao.*

Kasi ni muhimu kuhusiana na Wi-Fi, kuanzia kutazama filamu hadi kujiunga na simu ya mkutano bila tatizo lolote. Sasa Wenyeji wanaweza kuthibitisha kasi ya Wi-Fi ya tangazo lao bila kuondoka kwenye programu ya Airbnb kwa kutumia jaribio jipya la kasi ya Wi-Fi. Nyenzo hii hukuruhusu kufanya majaribio ya kasi ya Wi-Fi ya nyumba yako kwa urahisi, kisha kuionyesha moja kwa moja kwenye ukurasa wa tangazo lako—ili kukusaidia kuwavutia wageni wengi zaidi wanaotafuta sehemu za kukaa zenye muunganisho wa intaneti.

Kupima Wi-Fi yako kwa kutumia programu yako ya Airbnb

Jaribio la kasi ya Wi-Fi kwa sasa linapatikana kwenye programu ya Airbnb kwa ajili ya iOS na Android. Ili kuanza, utahitaji kuwa kwenye sehemu yako na kuunganishwa kwenye mtandao wa Wi-Fi wa nyumba yako.

Ukiisha kufika hapo, fuata hatua hizi:

  1. Bofya Wasifu kisha ubofye Badilisha kwenda kukaribisha wageni
  2. Bofya Matangazo kisha ubofye tangazo unalotaka
  3. Chini ya Kuhusu tangazo, nenda kwenye Vistawishi
  4. Sogeza hadi Wi-Fi kisha ubofye Weka maelezo
  5. Bofya Fanya majaribio ya kasi ya Wi-Fi (utahitaji kuruhusu ufikiaji wa eneo ikiwa bado haujaidhinishwa)
  6. Bofya Anza jaribio
  7. Baada ya matokeo kuonyeshwa, bofya Hifadhi ili kasi ya Wi-Fi yako iweze kuonekana kwenye ukurasa wa tangazo lako
  8. Ikiwa kasi ya Wi-Fi yako ni Mbps 50 au zaidi, tangazo lako litaangaziwa kuwa na Wi-Fi ya kasi

    Pata maelezo zaidi kuhusu kutoa Wi-Fi kwa wageni

    Kuelewa kasi ya Wi-Fi yako

    Kasi ya intaneti hupimwa kwa megabiti kwa sekunde na nambari hii inaweza kuonyesha kasi ya muunganisho wako. Hizi ni tarakimu tofauti unazoweza kuona kutokana na jaribio la kasi ya Wi-Fi na maana yake:

    • Hakuna chochote kinachoonyeshwa: Hakuna Wi-Fi inayopatikana. Huna Wi-Fi au huwezi kuunganisha. Jaribu kuwasha tena ruta yako au uhamie kwenye sehemu nyingine katika nyumba yako.
    • Mbps 1-6: Kasi ya msingi ya Wi-Fi. Wageni wanaweza kuangalia ujumbe na kuvinjari wavuti.
    • Mbps 7-24: Kasi thabiti ya Wi-Fi. Wageni wanaweza kutazama video za HD mtandaoni.
    • Mbps 25-49: Kasi ya kuridhisha ya Wi-Fi. Wageni wanaweza kutazama video zenye ubora wa juu za 4K mtandaoni na kujiunga kwenye simu za video.
    • Mbps 50 na zaidi: Safi sana! Kasi ya juu ya Wi-Fi. Wageni wanaweza kutazama video za 4K na kujiunga na simu za video kwenye vifaa vingi. Tutaangazia Wi-Fi ya kasi kwenye tangazo lako.

    Pata maelezo zaidi kuhusu kuthibitisha kasi ya intaneti yako

    Kuwajulisha wageni kuhusu kasi ya Wi-Fi yako

    Mara baada ya jaribio kukamilika na matokeo yako kuhifadhiwa, kasi ya Wi-Fi yako (katika megabiti kwa sekunde) itaonekana kwenye sehemu ya Vistawishi vyako karibu na Wi-Fi na kuruhusu wageni kuthibitisha kasi ya intaneti yako kabla ya kuweka nafasi.

    Ikiwa kasi yako ni Mbps 50 au zaidi, utafungua kistawishi kipya: "Wi-Fi ya kasi" itaonekana kwenye ukurasa wa tangazo lako.

    Kwa kuwa Wi-Fi ni kistawishi muhimu sana, tunafurahi kukupa nyenzo inayoweza kukusaidia kuonyesha kasi ya Wi-Fi yako kwa wageni—na kusaidia kuongeza uvutio wa tangazo lako kwenye Airbnb.

    *Kulingana na data ya ndani ya Airbnb iliyopima vistawishi vilivyotafutwa mara nyingi zaidi kuanzia tarehe 1 Septemba, 2020 hadi tarehe 1 Septemba, 2021.

    Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

    Vidokezi

    • Wi-Fi ni mojawapo ya vistawishi maarufu zaidi ambavyo wageni hutafuta

    • Jaribio jipya la kasi ya Wi-Fi hukuruhusu kuthibitisha na kuonyesha kasi ya Wi-Fi yako

    • Fanya majaribio ya Wi-Fi yako—ikiwa itaonyesha kuwa Mbps 50 au zaidi, "Wi-Fi ya kasi" itaangaziwa kwenye tangazo lako

    Airbnb
    11 Ago 2021
    Ilikuwa na manufaa?