Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.

Kuhakikisha eneo lako ni safi sana

Ikiwa sehemu yako si safi, wageni wanaweza kutoa tathmini mbaya.
Na Airbnb tarehe 17 Feb 2023
Imesasishwa tarehe 17 Feb 2023

Kutoa huduma kwenye sehemu safi ndiyo sehemu muhimu zaidi ya ukarimu wa nyota tano. Kama sehemu ya sheria za msingi kwa ajili ya Wenyeji, sehemu zote zilizotangazwa kwenye Airbnb zinapaswa kuwa safi bila hatari za afya wageni wanapoingia. Wenyeji ambao wana mkakati thabiti wa kufanya usafi watapata mafanikio zaidi.

Unda mkakati wa kusafisha

Iwe unafanya kazi hiyo mwenyewe au unaajiri msafishaji, ni muhimu kwamba sehemu yako isafishwe vizuri baada ya mgeni kuondoka na kabla ya mwingine kuingia, wakati wote.

Ikiwa wageni watapata nywele bafuni au vyombo vichafu ndani ya sinki, ukaaji wao utavurugika. Hii inaweza kuwafanya waandike tathmini mbaya au hata kupunguza muda wa ukaaji wao.

Ikiwa unaajiri msafishaji, pitia mchakato wa kufanya usafi mara moja wewe mwenyewe ili ujue hasa kile kinachohitajika kufanywa. Hakikisha unapanga muda wa kutosha kati ya wageni ili usafi ufanywe kwa kina. Pata msafishaji wa pili au mpango mbadala ikiwa msafishaji wako hawezi kuukamilisha kwa siku moja.

Unapotengeneza mpango wako, jaribu vidokezi hivi kutoka kwa Wenyeji wengine:

  • Tandua vitanda na uanze kufua kwanza ili uwe na muda wa kutosha kufua mashuka mengi ikihitajika..
  • Safisha na upanguse sehemu zote, ukizingatia sana sehemu zinazoguswa mara nyingi kama vile rimoti na vitasa vya milango.
  • Tandika vitanda, badilisha taulo, weka upya mablanketi na mito ya mapambo, na utumie rola ya mashuka kwenye kitu chochote kinachoihitaji.
  • Fungua madirisha unaposafisha ili hewa safi iingie ikiwa hali ya hewa inafaa.
  • Fagia na upige deki sakafu mwisho ili kukusanya vumbi au uchafu wowote.

Fuata orodha kaguzi hii ya kusafisha

  • Sehemu zote zinapanguswa na kusafishwa.
  • Sakafu zote hufutwa vumbi au kufagiwa na kupigwa deki
  • Maeneo yote hayana vijidudu, wadudu, utando wa buibui, kuvu na madoa.
  • Mashuka na taulo ni safi bila madoa.
  • Vitanda vyote vimefanywa upya, ni vyororo na kuvingirishwa.
  • Vyoo vyote, sinki, mabafu ya manyunyu na mabeseni yanasafishwa na kutakaswa.
  • Shampuu, sabuni ya maji ya kuogea, sabuni ya mkono au sabuni ya sahani zimejazwa upya.
  • Vifaa vyote vya usafi wa mwili vimehifadhiwa mahali pasipoonekana kwa macho.
  • Vyombo vyote na vifaa vya kupikia ni safi na vimewekwa mbali.
  • Vifaa vyote vya jikoni, ikiwemo friji, jiko na oveni, ni safi na tayari kutumiwa. Hakuna mabaki ya chakula kwenye friji.
  • Takataka zote zinaondolewa.
  • Sehemu hiyo inanukia vizuri na safi.
Airbnb
17 Feb 2023
Ilikuwa na manufaa?