Kuweka matarajio dhahiri kwa kila mgeni

Usahihi ni kila kitu linapokuja suala la kukaribisha wageni.
Na Airbnb tarehe 17 Feb 2023
Inachukua dakika 2 kusoma
Imesasishwa tarehe 17 Feb 2023

Kama sehemu ya sheria za msingi kwa ajili ya Wenyeji, ukurasa wa tangazo lako unapaswa kuelezea eneo lako kwa usahihi, ukionyesha vipengele na vistawishi vinavyopatikana kuanzia wakati wa kuingia hadi kutoka. Wageni watavunjika moyo ikiwa kile wanachopata hakilingani na jinsi ulivyoelezea sehemu yako.

Kuweka matarajio halisi

Usisifu kupita kiasi eneo lako wala usiache nje kitu chochote muhimu. Ni bora kusema ukweli kuhusu mapungufu yanayoweza kuwa katika sehemu yako na kitongoji chako, kama vile iwapo mapazia yako yanaingiza mwanga mwingi wa asubuhi au iwapo eneo lako liko karibu na eneo la ujenzi.

Hakikisha unaweka matarajio vizuri kwa vidokezi hivi:

  • Waambie wageni kile wanachoweza kutarajia hasa katika maelezo ya tangazo lako na uweke picha zilizo na maelezo mafupi. Ikiwa kuna mbwa kwenye sehemu hiyo au ngazi zinatoa sauti ya mkwaruzo, wajulishe wageni.
  • Weka idadi sahihi ya vyumba na mabafu. Aina ya tangazo lako inapaswa pia kuonyesha eneo lako halisi, ikiwa liko katika fleti, usieleze kwamba ni nyumba ya mashambani.
  • Usitilie chumvi vistawishi vyako. Kama uko umbali wa saa moja kutoka kwenye kivutio maarufu, usiseme kwamba uko karibu, bainisha umbali wako. Ikiwa bwawa lako au beseni la maji moto lina saa za msimu au nyakati za kufunga, zijumuishe kwenye tangazo lako.

Kuwafurahisha wageni wako

Wenyeji wenye mafanikio wanaahidi mambo machache lakini wanatimiza mengi. Hii inamaanisha wanaepuka kutilia chumvi mno maelezo ya tangazo lao nao hufanya mengi zaidi ili kutoa ukarimu mzuri.

Jaribu mapendekezo haya ili kuwafurahisha wageni wako wakati wa kuingia:

  • Toa picha halisi. Epuka pembe zenye upana mkubwa mno na uepuke kuhariri kupita kiasi, hatua ambayo hufanya sehemu hiyo ionekane kubwa au angavu zaidi kuliko ilivyo. Unaweza kuajiri mpiga picha mtaalamu kutoka Airbnb katika baadhi ya maeneo.
  • Kubali matengenezo ya kawaida. Angalia sehemu yako mara kwa mara ili kuthibitisha kuwa kila kitu kilichotangazwa kinapatikana na kinafanya kazi. Ikiwa una beseni la maji moto, bwawa la kuogelea, mashine ya kuosha vyombo na kadhalika, hakikisha kwamba vinafanya kazi vizuri kabla ya wageni kuwasili.
  • Toa kitu cha ziada kama ishara ya shukrani kwa wageni wako. Hiki kinaweza kuwa rahisi kama vile ujumbe wa ukaribisho ulioandikwa kwa mkono au pakiti ya biskuti.
Airbnb
17 Feb 2023
Ilikuwa na manufaa?