Kutoa sehemu ya kukaa ya nyota 5

Jaribu vidokezi hivi ili urekebishe utaratibu wako wa kukaribisha wageni.
Na Airbnb tarehe 17 Feb 2023
Inachukua dakika 2 kusoma
Imesasishwa tarehe 17 Feb 2023
Wageni wana uwezekano mkubwa wa kuweka nafasi kwenye maeneo ambayo yana tathmini nzuri. Ikiwa unapata ukadiriaji wa chini, kuna mambo kadhaa unayoweza kufanya ili uboreshe uzoefu wa wageni wako na kufikia tathmini hizo za nyota tano.

Kuweka matarajio

Hakikisha maelezo ya tangazo lako yanatoa taswira kamili na sahihi ya eneo lako.

  • Usisifu mno tangazo lako. Shiriki vidokezi na madokezo, kuanzia beseni la maji moto au meko hadi kwenye mbao za sakafu zinazotoa sauti ya mkwaruzo au kelele kutoka barabarani.

  • Pakia picha za ubora wa juu na utaje matatizo yoyote yanayoweza kutokea kwenye maelezo ya tangazo lako katika maelezo mafupi ya picha. Lenga kuweka picha mbili hadi tatu kwa kila chumba au eneo, ikiwemo vistawishi bora vyovyote.

  • Usitumie pembe zenye upana mkubwa mno wala usihariri picha zako kupita kiasi, hatua ambayo inaweza kufanya vyumba vionekane vikubwa au vyenye mwanga kuliko hali yake halisi.

Kuwasiliana kikamilifu

Kumbuka kwamba wewe ndiye mtu wa pekee wa kuwasiliana na wageni wanaokaa kwenye eneo lako.

  • Kuwa makini na uthibitishe kwamba wageni wana kila kitu wanachohitaji kabla ya kuingia, kama vile maelekezo na maagizo ya kuingia ndani.

  • Jibu haraka iwezekanavyo ujumbe wa wageni.

  • Tumia lugha jumuishi katika ujumbe wako, ambayo ni muhimu katika kuwakaribisha wageni wote.

  • Tumia programu ya Airbnb na nyenzo kama vile majibu ya haraka na ujumbe ulioratibiwa ili kurahisisha mawasiliano.

  • Tuma maelekezo ya kuingia angalau saa 24 kabla, ili wageni wawe na muda wa kuyasoma na kuuliza maswali. Hii ni muhimu hasa kwa wageni walio na mahitaji ya ufikiaji.

Kukaribisha wageni

Wakati mwingine tofauti kati ya tathmini ya nyota nne na tano ni ndogo tu kama vile kuwa mwangalifu kuhusu maelezo.

  • Usafi ni muhimu. Hakikisha sehemu zote, sakafu, na vitambaa ni safi na kutolewa vumbi. Tafuta nywele baada ya kusafisha au ishara yoyote ya uchafu au vumbi. Hata kama eneo lako linavutia sana, ni lazima liwe safi kabisa ili lipate tathmini za nyota tano.

  • Ongeza mguso wa kibinafsi kwa kuacha ujumbe wa ukaribisho au kutuma ujumbe wa ukaribisho kwenye programu.

  • Fanya sehemu yako ionekane kama nyumbani. Kwa mfano, ikiwa ina jiko, fikiria kuweka sufuria na vikaango, vijiko vya chakula na vitu muhimu vya mapishi.

  • Ishara ndogo hutimiza mambo makubwa, kama vile kuweka blanketi kwenye kochi au kutoa kahawa au chai.

Kujizatiti kuweka nafasi

Kama sehemu ya sheria za msingi kwa ajili ya Wenyeji, hupaswi kughairi nafasi zilizowekwa ambazo zimethibitishwa. Ikiwa kughairi hakuepukiki, unapaswa kufanya uwezavyo ili kughairi kukiwa na muda mwingi iwezekanavyo uliobaki. Wasiliana na Airbnb ikiwa unahitaji usaidizi.

Airbnb
17 Feb 2023
Ilikuwa na manufaa?