Weka upya tangazo lako

Sasisha picha zako na maelezo ili kusaidia kuweka matarajio yaliyo dhahiri zaidi.
Na Airbnb tarehe 26 Feb 2024
Inachukua dakika 3 kusoma
Imesasishwa tarehe 26 Feb 2024

Ukaribishaji wageni wenye ukadiriaji wa nyota tano huanza kwa kuweka matarajio yaliyo dhahiri kwenye ukurasa wako wa tangazo. Wageni wanataka sehemu yako iwe katika hali nzuri na iwe kama ilivyoonyeshwa kwenye picha zako. Pia wanataka vistawishi vyote ulivyoorodhesha viwe rahisi kupata na kutumia.

Kuna uwezekano mdogo wa wageni kujiuliza kuhusu au kuhukumu vibaya eneo lako unapotoa maelezo zaidi. Utapata nyenzo unazohitaji ili kuonyesha upya maelezo ya tangazo lako katika Kichupo cha Matangazo.

Unda ziara ya picha

Wasaidie wageni waelewe mpangilio wa nyumba yako kwa kutumia ziara ya picha ili kupanga picha za nyumba yako kiotomatiki kulingana na chumba.

Anza kwa kujumuisha picha za sasa za kila chumba na sehemu ya pamoja.

  • Tumia picha zenye ubora wa juu. Piga picha katika hali ya mlalo ikiwa na mwangaza wa kutosha. Pakia ukubwa mkubwa zaidi wa faili, angalau 1024 kwa pikseli 683. Zingatia kuajiri mpiga picha mtaalamu.
  • Pakia picha kadhaa kwa kila chumba. Toa mchanganyiko wa picha zilizopigwa kwa mbali, ubali wa kati na karibu zaidi. Kuza mwonekano wa maelezo muhimu, kama vile chaja ya simu ya kawaida kwenye meza ya kitandani au mpangilio wa kahawa na chai jikoni.
  • Angazia vipengele na vistawishi. Toa picha za mipangilio ya kulala, maeneo ya nje, na vipengele vyovyote maalumu kwa ajili ya wanyama vipenzi, familia zilizo na watoto, au watu wanaofanya kazi mbali na ofisi.
  • Jumuisha vipengele vya ufikiaji. Onyesha jinsi eneo lako linavyoweza kuwakaribisha watu wenye matatizo ya kutembea. Hakikisha unasoma mwongozo wa Airbnb wa kupiga picha vipengele vya ufikiaji.

Kisha, fuata hatua hizi ili uweke ziara yako.

  1. Chagua Tengeneza ziara yako ya picha. Injini mahususi ya AI ya Airbnb inapanga picha za tangazo lako papo hapo katika aina 19 za vyumba na sehemu. Picha ambazo haizitambui zinakwenda chini ya Picha za ziada.

  2. Tathmini ziara yako ya picha. Hakikisha umejumuisha angalau picha moja ya kila chumba katika nyumba yako. Unaweza kusogeza, kuongeza, au kufuta picha.

  3. Weka maelezo dhahiri ya kila picha yanayoelezea kile kinachotolewa na kila chumba au sehemu. 

  4. Ili kuhakiki jinsi picha zako zinavyoonekana kwenye tangazo lako, nenda kwenye Sehemu yako kisha uguse kitufe cha Angalia.

"Watu wengi wanapenda vitu vya kuona na wanaweza kutumia muda mwingi kwenye picha zako kuliko maelezo ya tangazo lako," anasema Sadie, Mwenyeji Bingwa huko Santa Fe, New Mexico.

Rekebisha maelezo ya tangazo lako

Wageni wanataka nyumba za kwenye Airbnb zilingane na maelezo ya tangazo. Kurasa za tangazo zenye ubora wa juu zinaelezea kwa usahihi kile ambacho wageni wanaweza kutarajia kuona, kusikia na kupata kwenye eneo lako wakati wa ukaaji wao.

  1. Hakikisha kwamba Kichwa cha tangazo lako kinaongeza maelezo ya kipekee kuhusu nyumba yako na mazingira yake. Kwa mfano, "Studio tulivu karibu na Uffizi" kinaonyesha kwa maneno machache kwamba eneo hilo ni fleti iliyoko katikati huko Florence, Italia.

  2. Chini ya Maelezo ya tangazo, wajulishe wageni jinsi ilivyo kukaa kwenye sehemu yako. Toa taarifa muhimu kuhusu mahali nyumba yako ilipo, mapambo, au ukarimu. Kwa mfano, unaweza kuelezea kwamba sitaha inatazama korongo wakati jua linapotua au kwamba nyumba yako iko juu ya mkahawa ambao una shughuli nyingi kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 4:00 usiku.

  3. Chini ya Nyumba yako, toa maelezo ya jumla ya vyumba na sehemu zako za wazi. Tumia sehemu hii kusisitiza maelezo yanayotekelezeka yanayojibu maswali ya wageni. Kwa mfano, unaweza kueleza kwamba ua wa nyuma umejengewa uzio, na kuna nafasi ya kutosha ya watoto na wanyama vipenzi kucheza. 

  4. Chini ya Kushiriki mahali, unaweza pia kuweka mahali mahususi kwa ajili ya nyumba yako ili kuwasaidia wageni waelewe eneo hilo. Vinginevyo, wataona tu eneo la jumla hadi watakapoweka nafasi.

Maelezo dhahiri na thabiti huwa yanafanya kazi vizuri zaidi. Kusifia au kutia chumvi kile unachotoa kunaweza kusababisha maudhi na tathmini mbaya.

Weka vistawishi

Kihariri cha Tangazo kinafanya kuweka vistawishi kuwe rahisi zaidi kuliko hapo awali.

  1. Chini ya Vistawishi, gusa alama ya kujumlisha (+). Unaweza kuangalia vistawishi karibu 150 kulingana na aina au kulingana na herufi au utafute kulingana na jina.

  2. Chagua ishara ya kujumlisha mbele ya kipengele chochote ambacho nyumba yako inacho.

  3. Gusa kitufe cha Angalia ili kuona jinsi mabadiliko kwenye ukurasa wako wa tangazo yatakavyoonekana kwa wageni.

Ni muhimu kuweka vistawishi vyako vyote na kuweka kila kitu kikiwa sawa. Wageni wanaweza kuchuja utafutaji wao wa vipengele maarufu na vistawishi kama vile kiyoyozi, maegesho bila malipo na mashine ya kufulia au kukausha.

Sasisha tangazo lako

Unda ziara ya picha, boresha maelezo ya tangazo lako, au uweke vistawishi.
Nenda kwenye kichupo cha Matangazo

Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Airbnb
26 Feb 2024
Ilikuwa na manufaa?