Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

Mwongozo wa kupiga picha za vipengele vya ufikiaji

Picha bora za tangazo husaidia kuweka matarajio kwa wageni wenye mahitaji ya ufikiaji.
Na Airbnb tarehe 22 Sep 2020
video ya dakika 5
Imesasishwa tarehe 8 Mac 2024

Vidokezi

 • Wasafiri hutafuta mara kwa mara vipengele vya ufikiaji kama vile milango isiyo na ngazi

 • Picha za ubora wa juu za vipengele hivi zinaweza kuwasaidia wageni kuamua ikiwa eneo lako linafaa

  • Pata maelezo zaidi katika mwongozo wetu wa Kituo cha Msaada kuhusu kuweka vipengele vya ufikiaji kwenye matangazo

  Wageni walio na mahitaji ya ufikiaji wangependa kujua nini cha kutarajia wanapowasili kwenye sehemu yako. Kupakia picha bora, kuanzia picha za njia yako ya kuingilia hadi picha za sehemu za ndani, hadi sehemu ya Ufikiaji ya tangazo lako kunaweza kuwasaidia wageni kubaini ikiwa wanaweza kutembea kwenye nyumba yako kwa usalama na kwa starehe.

  Kama Mwenyeji, ni jukumu lako kuhakikisha maelezo na picha za tangazo lako ni ya kisasa na sahihi. Na ingawa si jukumu lako kuelewa mahitaji ya kila mtu, kupiga picha dhahiri za sehemu yako huwaruhusu wageni watarajiwa kuamua ikiwa tangazo lako linawafaa.

  Airbnb hutathmini vipengele vyote vya ufikiaji kabla ya kuwekwa kwenye tangazo lako. Ikiwa picha haionyeshi wazi kipengele kama inavyotakiwa na miongozo yetu, tunaweza kukuomba upakie kipengele kipya au uondoe kipengele hicho kwenye tangazo lako.

  Unapofikiria kufanya mabadiliko kwenye tangazo lako, haya ni baadhi ya mambo ya kuzingatia:

  • Unaweza kubainisha kwamba ni vyumba kadhaa tu ndivyo vina vipengele vya ufikiaji. Kwa mfano, unaweza kuonyesha kwamba ni bafu moja tu ndilo lina mlango usio na ngazi.
  • Huhitaji kutoa picha za kitaalamu, unaweza tu kupiga picha ukitumia simu. Picha hizi huonekana kwenye sehemu ya Ufikiaji ya ukurasa wa tangazo lako, ambayo ni tofauti na matunzio ya picha ya tangazo lako. Ni lazima ujumuishe angalau picha moja ya kila kipengele cha ufikiaji unachochagua.
  • Tumia utepe wa kupimia ili kuwaonyesha wageni kwamba una milango mipana (hii ni sehemu ya vigezo vyetu vya picha) ambayo itatoshea viti vya magurudumu au vifaa vingine vya kutumia kutembea.
  • Kupakia picha kadhaa za kila kipengele zilizopigwa kutoka pembe na maeneo anuwai, huwasaidia wageni kuielewa vizuri sehemu yako. Kwa mfano, ikiwa unaonyesha mlango usio na ngazi, piga picha kutoka pande zote mbili za kizingiti ili mgeni aweze kuona kijia kizima cha kuingia kwenye sehemu hiyo.

  Jinsi ya kuonyesha kwamba njia ya kwenda kwenye mlango wako haina ngazi

  Je, wageni wanaweza kufika kwenye mlango wako wa mbele kutoka kwenye kijia cha miguu au maegesho ya karibu bila kukumbana na ngazi au vizingiti? Je, wanahitaji kupitia kwenye sehemu za aina gani ili kutembea kufika hapo? Hakikisha kuwa umepiga picha dhahiri za kijia kinachoelekeza kutoka nje hadi kwenye mlango wa tangazo lako.

  Jinsi ya kupiga picha ya sehemu yako ya kuingilia:
  1. Simama angalau futi 20 (mita 6) nje ya lango la jengo kwenye kijia cha miguu au maegesho yaliyo karibu ili kuonyesha sehemu kubwa kadiri iwezekanavyo ya kijia hicho na uinamishe kamera kidogo kuelekea ardhini ili kuonyesha uso wa njia hiyo. Ikiwa tangazo lako liko katika jengo la fleti au hoteli, hakikisha umejumuisha kijia kutoka kwenye lango la jengo hadi kwenye baraza la kuelekea kwenye mlango wa nyumba yako. Ikiwa inatumika, ni muhimu pia kutoa picha za lifti au njia zozote za mwinuko.

    2. Hakikisha unaonyesha mlango wa jengo mwishoni mwa kijia.

    Jinsi ya kuonyesha njia za kuingilia zisizo na ngazi katika sehemu yako

    Waonyeshe wageni wako kwamba wanaweza kuingia kwenye mlango wa mbele, pamoja na chumba cha kulala, choo, bafu na sehemu za pamoja bila kupanda ngazi zozote au vizingiti virefu (urefu wa zaidi ya inchi 2 au sentimita 5).

    Jinsi ya kupiga picha za sehemu za kuingilia:
    1. Fungua mlango unaoelekea kwenye sehemu ya kuingilia ambao ungependa kuangazia na uinamishe kamera kidogo kuelekea sakafu ili kupiga picha dhahiri njia tambarare kwenye kila upande wa kizingiti.

      2. Rudi nyuma angalau futi 5 (mita 1.5) kutoka kwenye mlango ili kuonyesha pande zote mbili za mlango na ikiwa sehemu hiyo ina sehemu kadhaa za kuingia, hakikisha unapiga picha kila moja.

      3. Ikiwa unaonyesha chumba fulani (chumba cha kulala, bafu, sebule, n.k.) kina ufikiaji usio na ngazi, unathibitisha kuwa chumba hicho kiko kwenye ghorofa ya chini au kinafikika kupitia lifti au njia ya mwinuko. Jumuisha picha nyingi zinazoonyesha njia kuanzia kwenye mlango wa mbele hadi ndani ya chumba hicho.

       4. Ikiwa una bafu lisilo na vizingiti, fungua pazia la bafu au milango na uinamishe kamera kidogo kuelekea kwenye sakafu ya njia ya kuingilia ili kuonyesha hakuna vizingiti vinavyozidi takribani inchi 1 (sentimita 2.5).

       Kidokezi: Ili kupata njia zaidi za kupiga picha nzuri kwenye simu mahiri yako, tazama mafunzo yetu ya picha.

       Jinsi ya kupiga picha milango mipana

       Kwa wageni walio na vifaa vya kutembelea kama vile viti vya magurudumu, kujua upana wa milango yako kunaweza kuwasaidia kuamua ikiwa wataweza kutembea kwenye sehemu yako. Kwenye Airbnb, tunazingatia "mlango mpana" kuwa mlango wenye upana wa angalau inchi 32 (sentimita 81).

       Fungua mlango na utumie utepe wa kupimia ili kuonyesha upana wa fremu ya mlango. Unaweza kupiga picha mbili: moja inayoonyesha utepe mzima wa kupimia na ya pili ambayo imekuzwa zaidi ili mgeni aweze kusoma kipimo.

        Jinsi ya kuonyesha vipengele vingine vya ufikiaji

        Kuna vipengele vingine vingi ambavyo vinaweza kuwasaidia wageni kuingia na kutembea kwenye nyumba yako kwa urahisi. Ikiwa una mojawapo ya vitu hivyo, hakikisha unavipiga picha na kuviweka kwenye tangazo lako ili wageni wako wajue nini cha kutarajia.

        1. Onyesha mambo mengi kadiri iwezekanavyo kuhusu kila kipengele katika picha zako.

        2. Jaribu pia kujumuisha sehemu kubwa kadiri iwezekanavyo ya eneo la karibu, ili mgeni aone mahali ambapo kipengele hicho kipo au ukubwa wake. Kwa mfano, ikiwa unaonyesha kiti cha kuogea, hakikisha unakionyesha kikiwa ndani ya bafu.

         Mifano ya kila kipengele cha ufikiaji

         Vyuma vya kujishikilia kwenye bafu au choo: Hivi ni vyuma ambavyo vimefungwa kwa makomeo ukutani vinavyoweza kubeba uzito na vimekusudiwa kuwasaidia watu kujisawazisha. Havipaswi kuwa chanja za kuweka taulo, vipasha joto vya taulo au sehemu ya mlango wa bafu.

         Kiti cha kuogea: Kwa kawaida, hii ni benchi au kiti huru kilichoundwa ili kuwasaidia watu wenye matatizo ya kutembea kuweza kuoga. Hiki pia kinaweza kuwa kiti kilichojengwa ukutani, lakini hakipaswi kuwa fanicha ambayo haijakusudiwa kutumika kwa kuoga (kama vile fanicha ya barazani au viti vya plastiki vya kukunjwa ambavyo vinaweza kumfanya mtu ateleze kwenye sakafu yenye majimaji).

         Kifaa cha kumwinua mtu kinachoning'inia kwenye dari au kinachosogezwa: Hii ni lifti iliyowekwa kwenye dari au kifaa huru kinachosaidia kuwaweka au kuwatoa watu kwenye kiti cha magurudumu.

         Sehemu ya kuegeshainayoweza kufikika : Hii ni sehemu ya maegesho ya umma ambayo imetengwa kwa ajili ya watu wenye ulemavu au eneo binafsi la maegesho kwenye nyumba yako ambalo lina nafasi ya angalau futi 11 (mita 3.5) inayotoshea gari moja. Kwenye picha, onyesha sehemu ya maegesho ya umma iliyo na ishara zilizobainishwa za maegesho au eneo binafsi la kuegesha lenye gari lililoegeshwa karibu na sehemu ya maegesho ya wageni kwa ajili ya marejeleo. Unaweza pia kutumia utepe wa kupimia kwenye picha ili kuonyesha upana.

         Kifaa cha kumwinua mtu bwawani: Hiki ni kifaa kinachomwinua mtu na kumweka ndani au kumtoa nje ya bwawa au jakuzi.

         Kijia kilicho na mwangaza wa kutosha kinachoelekea mlangoni: Hii ndiyo njia ya nje kutoka kwenye barabara binafsi inayoelekea kwenye nyumba au kijia cha nje kinachoelekea kwenye mlango wa nyumba yako kinachopata mwangaza kutoka kwenye taa za barabarani, taa za mandhari au vyanzo vingine vya taa. Jaribu kupiga picha ya kijia hicho wakati wa usiku au alfajiri ili wageni waweze kuona eneo la taa na ukubwa wa mwangaza wake.

         Unaweza pia kuzingatia njia nyingine za kuwasaidia wageni wenye mahitaji ya ufikiaji. Kukiwa na mawasiliano yaliyo wazi na mabadiliko kadhaa kwenye sehemu na tangazo lako, unaweza kuleta tofauti kubwa sana kwa wageni wengi.

         Jake, mgeni mwenye matatizo ya kutembea, anasema hivi kwa ufupi: "Kuwa na taarifa sahihi mapema humruhusu mtu mwenye ulemavu kuwa mtalii."

         *Kulingana na takwimu za Airbnb zilizokusanywa kuanzia mwezi Januari hadi Mei mwaka 2019

         Vidokezi

         • Wasafiri hutafuta mara kwa mara vipengele vya ufikiaji kama vile milango isiyo na ngazi

         • Picha za ubora wa juu za vipengele hivi zinaweza kuwasaidia wageni kuamua ikiwa eneo lako linafaa

          • Pata maelezo zaidi katika mwongozo wetu wa Kituo cha Msaada kuhusu kuweka vipengele vya ufikiaji kwenye matangazo

          Airbnb
          22 Sep 2020
          Ilikuwa na manufaa?