Vitendo jumuishi vya kumsaidia kila mgeni ahisi amekaribishwa

Pata mwongozo kutoka kwa Wenyeji wazoefu—kuanzia kusasisha tangazo lako hadi kutathmini wageni.
Na Airbnb tarehe 27 Jun 2022
Inachukua dakika 5 kusoma
Imesasishwa tarehe 15 Jul 2022

Vidokezi

Kukaribisha wageni kwenye Airbnb kunamaanisha kufungua sehemu yako kwa watu kutoka ulimwenguni kote na ujumuishaji ndio msingi wa kukaribisha wageni.

Jambo muhimu katika kuwa Mwenyeji mwenye mafanikio ni kuelewa jinsi ya kusaidia kufanya watu wa asili zote wastareheke na wajisikie nyumbani. Kama jumuiya, tumejizatiti kumkaribisha kila mgeni, wa mbari, dini, asili ya kitaifa, kabila, ulemavu, jinsia, utambulisho wa kijinsia, mwelekeo wa kingono au umri wowote, kwa heshima, bila hukumu wala upendeleo.

Ukarimu jumuishi ni sehemu muhimu ya kuwa Mwenyeji mwenye mafanikio. Hii inamaanisha:

  • Kukubali na kukaribisha wageni wote wa tamaduni tofauti

  • Kutoa huduma sawa na kuzingatia mahitaji ya wageni

  • Kujenga uhusiano kupitia tofauti na ufanano

  • Kuwa na mtazamo wa wazi na utayari wa kuuliza maswali ili kujua kile wageni wanachoweza kuhitaji kwa ajili ya ukaaji wao

Airbnb ilikusanya vidokezo kutoka kwa Wenyeji, wageni, na wataalamu ili uweze kujumuisha mazoea jumuishi katika utaratibu wako wa kukaribisha wageni na kuonyesha ukarimu kwa kila mgeni. Kuanzia kuweka tangazo lako na kuandika tathmini, vitendo hivi vilivyopendekezwa vinaweza kupunguza upendeleo usio dhahiri na kuwezesha uhusiano.

Kabla ya kuweka nafasi: Kuunda tangazo jumuishi

Kwa kuweka wazi kwamba unakaribisha watu wa asili zote, unaweza kuwasaidia wageni kutoka kwenye jumuiya zilizotengwa kihistoria wajihisi wamestareheka na kutiwa moyo kuweka nafasi kwenye sehemu yako. Tumejifunza kutokana na kuzungumza na wageni kwamba watu kutoka jumuiya hizi hasa hutafuta ishara za ujumuishaji katika matangazo kabla ya kuweka nafasi.

Haya ni baadhi ya mambo unayoweza kufanya ili kuonyesha kwamba wewe ni Mwenyeji jumuishi:

  • Fanya iwe dhahiri ndani ya sentensi chache za kwanza za maelezo ya tangazo lako kwamba unakaribisha watu wa asili zote (mifano iko hapa chini).

  • Eleza kwa usahihi vipengele vya ufikiaji vya nyumba yako na usasishe picha zako.

  • Jibainishe kwa jinsia unayotaka urejelewe kwenye wasifu wako. Ni njia ya kuonyesha vile unavyotaka urejelewe na inaashiria kwamba unajali kuhusu kumrejelea mgeni kwa jinsia anayopenda.

  • Washa kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo ili kuruhusu wageni kuweka nafasi kwenye tangazo lako bila idhini ya awali. Hii pia inaashiria kwamba uko tayari kumkaribisha mtu yeyote anayekidhi vigezo vyako vya kuweka nafasi.

  • Hutoa idhini za awali na hamasa kwa wageni ambao wanawasiliana nawe kabla ya kuweka nafasi. Tumejifunza kwamba wakati mwingine wageni huwasiliana na Wenyeji kabla ya kuweka nafasi ili kupima ikiwa watakubaliwa na kukaribishwa.

  • Kabla ya kukataa ombi la mgeni la kuweka nafasi, fikiria kwa makini kuhusu sababu yako. Je, ni sawa kwako kumweleza mgeni wako ana kwa ana?

Kidokezi: Toa maelezo zaidi kujihusu na mapendeleo yako katika wasifu wako na maelezo ya tangazo lako ili kuwapa wageni wako fursa ya kuungana.

Unaweza kujaribu kutumia kauli jumuishi ambazo Wenyeji wengine hutumia kwenye matangazo yao. Tulizungumza na wanachama wa Bodi ya Ushauri ya Wenyeji ili kupata mifano hii:

  1. Peter wa San Francisco anaandika: “Nyumba yangu ni sehemu salama kwa watu kutoka makundi yote ya walio wachache na waliotengwa. Ninawakaribisha wageni wa mbari, imani, jinsia na mielekeo yote ya kingono.”

  2. “Picha ya pili kwenye tangazo langu inaonyesha mnara ulioandikwa, ‘Wewe ni mmoja wetu,’” anasema Shinya wa Osaka, Japani. Shinya pia anajumuisha picha iliyoandikwa, "Ninaheshimu uanuwai na ujumuishaji," kama kauli ya nia. Unaweza pia kuandika hii katika maelezo mafupi.

Kabla ya kuwasili: Kumfanya kila mgeni ahisi kwamba amejumuishwa

Mara baada ya sehemu yako kuwekewa nafasi, tuma ujumbe wa ukarimu kwa wageni wako. Kuonyesha huruma, na si kukisia tu, kunatimiza mengi hapa.

  • Fanya ujumbe wako wa kukaribisha uwe mahususi kwa kuweka taarifa kutoka kwenye wasifu wa mgeni wako. Hii inaweza kujumuisha maswali kuhusu mambo anayoyapenda, mji alikozaliwa na burudani.

  • Tumia lugha isiyo na mwelekeo wa kijinsia unaporejelea wageni wako. Ni bora kuepuka kukisia jinsia ya mtu au hali ya uhusiano.

  • Ikiwa mgeni atauliza kuhusu mahitaji ya ufikiaji, hakikisha kwamba unajibu maswali yake na uulize ni nini kingine anachoweza kuhitaji.

Kidokezi: Jaribu kutuma ujumbe unaowauliza wageni wako, "Ninaweza kufanya nini ili kuhakikisha kwamba unapata ukaaji wenye starehe?"

Ikiwa unahitaji hamasa, chukua vidokezi kutoka kwenye ujumbe wa Wenyeji wengine wanaotuma kwa wageni. Hii hapa ni mifano miwili:

  1. Michael wa Falcarragh, Ayalandi, anasema kwamba anaweka kipaumbele kwenye kutangulia kujenga mahusiano mazuri. "Siku zote ninawashukuru wageni kwa kuomba kukaa kwenye nyumba yetu," anasema. "Kisha ninataja kwamba nitawasiliana nao wakati wao wa kuwasili unapokaribia, ninawatakia siku njema na [kuwaambia] ikiwa kuna kitu chochote wanachohitaji kwa wakati huu, wasisite kuwasiliana nami."

  2. Susan wa Denver anaandika: “Nyumba yetu ni nyumba yako. Pata kustareheka. Fanya sehemu hii iwe yako mwenyewe. Ikiwa una mawazo ya kuboresha huduma yetu kwa wageni, tafadhali tujulishe.”

Baada ya kuingia: Kuhakikisha kwamba wageni wanastareheka

Wageni, hasa wale wanaotoka katika jumuiya za waliotengwa kihistoria, wamesema kwamba mambo haya yanaweza kuwafanya wahisi kukaribishwa zaidi:

  • Ruhusu mgeni aingie mwenyewe unapoweza, lakini muulize mgeni endapo angependelea kuingia kwa kukutana na mtu ana kwa ana.
  • Usiwatembelee wageni ikiwa si lazima. Badala yake, wape faragha na uwe ueleze waziwazi kwamba unapatikana (ana kwa ana au kwa njia ya mtandao) ikiwa wanakuhitaji.

Kidokezi: Jumuisha taarifa yoyote muhimu kuhusu sehemu yako katika sheria za nyumba yako, ili wageni waweze kuifikia kidijitali.

Baada ya kutoka: Kutathmini wageni bila upendeleo

Tathmini ni msingi wa jumuiya inayoaminika ya Airbnb. Kuwaandikia wageni wako tathmini ni nafasi ya kuonyesha shukrani zako na kutoa maoni muhimu.

  • Tumia viwango sawa kumtathmini kila mgeni.

  • Wakaribishe wageni wapya kwenye Airbnb unapoweza, kisha uwatathmini baada ya ukaaji wao. Tathmini hutimiza mengi katika kuwasaidia wageni walioweka nafasi za siku zijazo.

  • Wahimize wageni waandike tathmini. Tumejifunza kwamba wasafiri kutoka kwenye jumuiya zilizotengwa kihistoria mara nyingi husoma tathmini kabla ya kuweka nafasi ili kujua iwapo wageni wengine kama wao walihisi wamekaribishwa.

Hakikisha kwamba unafuata mazoea haya jumuishi, hasa ikiwa wewe ni mpya katika huduma ya kukaribisha wageni. Kumbuka kwamba mambo muhimu zaidi kuhusiana na kukaribisha wageni wote ni kuuliza maswali kuhusu mahitaji ya wageni wako na kudumisha mawasiliano.

Unaweza kuruhusu ujumuishaji kwa kuuliza wageni wako, Je, unahitaji nini ili kuhisi umestareheka na umekaribishwa katika sehemu yangu? Na tunatumaini kwamba, kwa kufanya hivyo, utakuwa unafanya iwe rahisi kwa wageni wako kufungua mlango wako katika maisha halisi na kufurahia kukaa katika eneo lako.

Vidokezi

Airbnb
27 Jun 2022
Ilikuwa na manufaa?