Kuelewa kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo

Kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo kinaweza kurahisisha mchakato wa kuweka nafasi na kulisaidia tangazo lako lionekane.
Na Airbnb tarehe 14 Des 2020
Inachukua dakika 2 kusoma
Imesasishwa tarehe 1 Mei 2024

Kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo huwaruhusu wageni kuweka nafasi kwenye nyumba yako mara moja kwa tarehe zinazopatikana. Huna haja ya kutathmini na kukubali kila ombi la kuweka nafasi, jambo linalookoa muda. Wageni wengi pia hupenda urahisi unaotolewa na kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo.

Jinsi kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo kinavyofanya kazi

Unaweza kuwasha au kuzima kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo wakati wowote. Sasisha mipangilio yako ya kuweka nafasi katika kichupo cha Matangazo.

Unapotumia kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo, wageni wote wanaoweka nafasi lazima wapitie mchakato wa Airbnb wa uthibitishaji wa utambulisho, wakubaliane na sheria za nyumba yako na watimize mahitaji yako ya mgeni.

Unaweza kuweka mahitaji yako ili kutoa huduma ya Kuweka Nafasi Papo Hapo kwa wageni ambao wana rekodi nzuri pekee. Hiyo inamaanisha kwamba wamekamilisha angalau ukaaji mmoja na hawajapokea tathmini zozote mbaya.

Ikiwa unahitaji kitambulisho cha serikali wakati wa kuingia ana kwa ana au ikiwa ni matakwa ambapo nyumba yako ipo, unaweza kuwaomba wageni kwa kuwatumia ujumbe kupitia kichupo chako cha Ujumbe.

Utahitaji kusasisha kalenda yako unapotumia kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo. Fikiria kuoanisha kalenda yako ya Airbnb na kalenda nyingine zozote unazotumia. Hatua hii hukusaidia kuepuka kupata uwekaji nafasi usiotarajiwa au kughairi nafasi iliyowekwa kwa sababu ya hitilafu ya uratibu, hali ambayo inaweza kusababisha kutozwa ada za kughairi na athari nyingine.

Unaweza kughairi nafasi iliyowekwa bila adhabu kwa sababu halali, kama vile mgeni kusema waziwazi kwamba huenda atavunja mojawapo ya sheria za nyumba yako. Kumbuka kwamba huwezi kamwe kughairi kwa sababu yoyote inayokiuka sera ya kutobagua ya Airbnb.

Kwa nini bado unaweza kupata maombi ya kuweka nafasi

Kuna hali chache ambapo unaweza kupata maombi ya kuweka nafasi hata unapotumia kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo:

  • Kalenda yako imepitwa na wakati.
  • Hivi karibuni umeghairi nafasi iliyowekwa.
  • Mgeni asiyetimiza mahitaji yako anaweza kutuma ombi la kuweka nafasi. 

Utahitaji kujibu kwa kukubali au kukataa nafasi iliyowekwa, au kutuma ujumbe kwa wageni wako watarajiwa ndani ya saa 24.

Chagua mpangilio wa kuweka nafasi unaokufaa

Unadhibiti wakati gani na jinsi gani wageni wanaweka nafasi kwenye eneo lako. Ingawa kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo kinatoa ufanisi na urahisi, baadhi ya Wenyeji wanaweza kuona kwamba maombi ya kuweka nafasi yanawafaa zaidi.

Chagua njia ambayo inakusaidia kuepuka kughairi wageni kwa sababu zinazoweza kuzuiwa.

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.
Airbnb
14 Des 2020
Ilikuwa na manufaa?