Jinsi utakavyolipwa kwa kukaribisha wageni

Pata maelezo ya misingi kuhusu lini na jinsi utakavyopokea malipo.
Na Airbnb tarehe 12 Feb 2020
Inachukua dakika 3 kusoma
Imesasishwa tarehe 15 Ago 2024

Airbnb inafanya iwe rahisi kupokea malipo, ambayo tunaita malipo yanayotumwa, kwa hatua chache tu.

Jinsi utakavyolipwa

Unachagua jinsi ambavyo ungependa kupokea pesa unayojipatia kwa kukaribisha wageni. Machaguo yako hutegemea mahali ulipo. Njia za kupokea malipo ni pamoja na:

  • Akaunti ya benki
  • Malipo ya Haraka
  • Kutuma fedha kimataifa kwa njia ya benki
  • Kadi ya Benki ya Mastercard ya Malipo ya Awali ya Payoneer
  • PayPal
  • Western Union

Ili kuweka malipo, weka njia ya kutuma malipo chini ya Malipo na kutuma malipo katika mipangilio ya akaunti yako ya kukaribisha wageni. Njia unayochagua itatumika kwenye malipo yote ya siku zijazo hadi utakapoibadilisha.

Unaweza kuhitaji kutoa taarifa zako za mlipa kodi ili tuweze kukutumia hati sahihi za kodi. Je, huna uhakika kama hii inatumika kwako? Pata maelezo zaidi kuhusu fomu za kodi

Wakati njia yako ya kupokea malipo inathibitishwa, itaonekana kama inasubiri. Mchakato wa kuthibitisha unaweza kuchukua hadi siku 10, isipokuwa uchague Malipo ya Haraka, ambayo huthibitishwa papo hapo.

Kiasi utakacholipwa

Chagua nafasi yoyote iliyowekwa kwenye kalenda yako ili uone kile mgeni alilipa na mapato yako kwa ukaaji huo. Sogeza chini, chini ya maelezo ya kuweka nafasi ili kupata orodha ya vitu vilivyobainishwa ambayo inajumuisha:

  • Bei yako ya kila usiku kwa ajili ya ukaaji wa mgeni
  • Ada zozote za hiari unazotoza kwa ajili ya kufanya usafi, wanyama vipenzi au wageni wa ziada
  • Kodi za umiliki
  • Ada za huduma za mgeni na mwenyeji
  • Malipo ya mwenyeji mwenza, ikiwa umeyaweka
  • Jumla ya malipo yako

Wenyeji wengi hulipa ada ya huduma ya Mwenyeji ya asilimia 3. Ada hii huisaidia Airbnb kulipia gharama za bidhaa na huduma zinazokusaidia kushiriki sehemu yako, kama vile usaidizi kwa wateja wa saa 24. Pata maelezo zaidi kuhusu ada za huduma

Ikiwa malipo unayopokea yapo ya chini kuliko ulivyotarajia, pengine ni kwa sababu ya mapunguzo uliyoweka au kughairi au kubadilisha nafasi iliyowekwa. Ada za muamala zinaweza pia kutumika kwa njia fulani za kupokea malipo, ingawa nyingi zinapatikana bila gharama ya ziada.

Utalipwa lini

Pesa unazopata kutokana na huduma ya kukaribisha wageni zinatolewa kwako takribani saa 24 baada ya muda ulioratibiwa wa mgeni wako kuingia. Muda halisi ambao fedha zitaingia kwenye akaunti yako hutegemea njia ya malipo ambayo umechagua.

Njia za kupokea malipo zinazopatikana na muda wake wa kawaida hadi malipo kukufikia hujumuisha:

  • Malipo ya Haraka: Dakika zisizozidi 30
  • Payoneer: Saa zisizozidi 24
  • PayPal: Siku 1 ya kazi
  • Western Union: Siku 1 ya kazi (inaweza kutofautiana kulingana na nchi/eneo)
  • Malipo kwa njia ya benki: Siku 3 hadi 5 za kazi
  • Malipo kwa njia ya benki kimataifa: Siku 3 hadi 7 za kazi

Unapokaribisha wageni kwenye ukaaji wa usiku 28 au zaidi, Airbnb hutuma mapato yako kwa awamu za kila mwezi, kuanzia saa 24 baada ya mgeni wako kuingia. Unaweza kuona hali ya malipo yako katika dashibodi yako ya mapato wakati wowote. Pata maelezo zaidi kuhusu kulipwa

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.
Airbnb
12 Feb 2020
Ilikuwa na manufaa?