Ruhusa mpya za Mwenyeji Mwenza na malipo rahisi

Dhibiti kile ambacho Wenyeji Wenza wanaweza kufikia na ushiriki malipo kwenye Airbnb.
Na Airbnb tarehe 11 Jun 2024
Imesasishwa tarehe 11 Jun 2024

Maelezo ya mhariri: Makala haya yalichapishwa kama sehemu ya Airbnb 2023 Toleo la Mei. Taarifa zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa. Pata maelezo kuhusu toleo letu la hivi karibuni.

Kuwa na Mwenyeji Mwenza kunaweza kufanya kukaribisha wageni kuwa rahisi zaidi na kuwa na faida kubwa. Anaweza kuwa jirani, mwanafamilia, rafiki, au mtu uliyemwajiri. Wenyeji Wenza wanaweza kukusaidia kusimamia kalenda yako, kusasisha tangazo lako na kuwajibu wageni.

Ulituambia kwamba unataka kuwa na uwezo wa kuamua kile Wenyeji Wenza wanaweza kufikia kwenye tangazo lako na kutoa malipo kwenye nafasi ulizoweka, moja kwa moja kwenye Airbnb. Tumesasisha nyenzo zetu za kukaribisha wageni pamoja ili kufanya iwe rahisi kukaribisha wageni.

Kupata nyenzo zako za mwenyeji mwenza

Nenda kwenye kichupo cha Matangazo kisha uchague tangazo. Sogeza hadi kwenye sehemu ya Wenyeji Wenza ili ufikie taarifa kuhusu Wenyeji Wenza wako, uweke ruhusa zao na upange malipo yao.

Unaweza pia kuwaalika Wenyeji Wenza wapya. Ili kukubali mwaliko wako, watahitaji kuwa na akaunti ya Airbnb.

Mwalike Mwenyeji mwenza, weka ruhusa zake na ufanye mwaliko wako uwe mahususi katika sehemu mpya ya Wenyeji Wenza.

Kuweka ruhusa kwa ajili ya Wenyeji wenza

Unapomwalika Mwenyeji Mwenza, utaombwa uchague anachoweza kufikia ili kusaidia kusimamia tangazo lako. Machaguo hujumuisha:

  • Ufukiaji kamili, kudhibiti kalenda na tangazo, kuondoa na kuweka ruhusa za Wenyeji Wenza wengine, utume ujumbe kwa wageni, utazame malipo na historia ya muamala na kuwasilisha na kudhibiti maombi ya fidia kwa niaba yako katika Kituo cha Usuluhishi na chini ya Ulinzi dhidi ya uharibifu wa Mwenyeji*

  • Kufikia kalenda na ujumbe, kutazama kalenda na kutuma ujumbe kwa wageni 

  • Ufikiaji wa kalenda, kutazama kalenda na maelezo ya kuingia na kutoka 

Wenyeji Wenza wote wataonekana kama Wenyeji Wenza kwenye tangazo lako, isipokuwa wale walio na ufikiaji wa kalenda pekee. Wenyeji Wenza wenye ufikiaji kamili wanaweza kujiweka kuwa Mwenyeji mkuu kwenye tangazo au unaweza kuchagua kufanya hivyo. Unaweza kubadilisha ruhusa za Wenyeji Wenza wakati wowote.

Kushiriki malipo na Wenyeji Wenza kwenye Airbnb

Unaweza kuchagua kugawana sehemu ya mapato yako na Mwenyeji Mwenza mmoja au zaidi. Mara tu utakapoweka malipo ya pamoja na Mwenyeji Mwenza wako akathibitisha, atapokea malipo kwa ajili ya nafasi zilizowekwa baada ya wageni kuingia. Vizuizi vya kugawana malipo vinatumika katika baadhi ya maeneo. Pata maelezo zaidi

Nyenzo hizi za wenyeji wenza ni sehemu ya Airbnb 2023 Toleo la Mei, kukiwa na maboresho 25 kwa ajili ya Wenyeji.

Dhibiti ruhusa na malipo ya Mwenyeji Mwenza

Sasisha sasa

Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

*Wenyeji Wenza wa matangazo yaliyo nchini Japani hawawezi kuanzisha, kusimamia au kutatua maombi ya vitu vilivyoharibika au kupotea katika Kituo cha Usuluhishi au maombi ya kufidiwa chini ya Ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji kwa niaba ya Wenyeji.

Ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji si sera ya bima. Haiwalindi Wenyeji wanaotoa sehemu za kukaa nchini Japani, ambapo Bima ya Mwenyeji wa Japani inatumika. Kwa Wenyeji wanaotoa sehemu za kukaa nchini China Bara, Mpango wa Ulinzi wa Mwenyeji wa China unatumika. Vikomo vyote vya malipo vinaonyeshwa katika USD.

Kwa matangazo yaliyo katika jimbo la Washington, majukumu ya mikataba ya Airbnb chini ya ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji yanalindwa na sera ya bima iliyonunuliwa na Airbnb. 

Ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji unadhibitiwa na sheria, masharti na vizuizi isipokuwa kwa Wenyeji ambao nchi yao ya makazi au biashara ni nchini Australia. Kwa Wenyeji kama hao, ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji unadhibitiwa na sheria, masharti na vizuizi hivi.

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Airbnb
11 Jun 2024
Ilikuwa na manufaa?