Airbnb 2023 Toleo la Kiangazi kwa ajili ya Wenyeji
Toleo la Kiangazi

Tunakuletea maboresho 25 kwa ajili ya Wenyeji, kuanzia kalenda hadi kutoka

Maoni yako yalihamasisha kila aina ya vipengele vipya katika uzoefu wa huduma ya kukaribisha wageni. Ukiwa na ufikiaji wa mapema, unaweza kuanza kuvitumia leo.

Nyenzo za kupanga bei zilizobuniwa upya

Sasa nyenzo zote za kupanga bei ziko kwenye kalenda, kwa hivyo unaweza kuweka na kurekebisha bei zako kwa urahisi kutoka sehemu moja. Kupitia mchanganuo wetu wa bei uliosasishwa, utaona pia jumla ya bei ya wageni na kile unachopata.

Linganisha matangazo sawia

Kwa mara ya kwanza kabisa, unaweza kulinganisha bei yako na bei ya wastani ya matangazo sawia yaliyowekewa nafasi karibu nawe ili kukusaidia uendelee kuwa na ushindani zaidi.

Telezesha ili uchague na mwonekano wa kila mwaka

Sasa katika kalenda, unaweza kutelezesha ili kuchagua tarehe kwenye simu, hakuna tena kugusa kila siku kivyake. Na hivi karibuni, utapata muhtasari wa miezi 12 kwa ufupi mwonekano mpya wa kila mwaka.

Maelekezo ya kutoka yaliyo ndani ya programu

Weka haraka maelekezo ya kutoka ya kawaida kwenye tangazo lako na ujumuishe kwa urahisi maombi mahususi. Wageni watakumbushwa kuhusu majukumu ya kufanya kabla ya kuondoka na wanaweza kugusa ili kukujulisha wanapokuwa wameondoka.

Arifa za ujumbe kusomwa

Wewe na wageni wako nyote mtapata arifa ya kuonyesha kuwa ujumbe umesomwa kwa hivyo unajua ikiwa ujumbe umesomwa. Isitoshe, sasa unaweza kushiriki maelekezo ya kutoka kwa haraka ukitumia majibu mapya ya haraka.

Ruhusa na malipo ya Mwenyeji Mwenza

Ni rahisi kuwaalika Wenyeji Wenza wapya na unaweza kuweka ruhusa za Mwenyeji Mwenza kwa mbofyo, chagua ruhusa kamili, kalenda na kikasha au kalenda tu. Pia inawezekana kuweka na kushiriki malipo na Mwenyeji Mwenza wako.

Kuangalia kwa haraka vipengele vyote vipya vya Mwenyeji

Angalia jumla ya bei
Unaweza kuona jumla ya bei yako ya kila usiku kwenye programu ili kujua kila wakati kile ambacho wageni watalipa.
Telezesha ili uchague tarehe
Telezesha kidole ili uchague au kuhariri tarehe kwa haraka kwenye kalenda, hakuna haja ya kugusa siku mojamoja.
Maelekezo ya kutoka ya programu
Andaa maelekezo ya kutoka haraka zaidi kwa kuchagua kutoka kwenye orodha iliyowekwa tayari ya majukumu ya kawaida.
Arifa za ujumbe kusomwa
Wewe na wageni wako wote mnapata arifa kuonyesha kuwa ujumbe umesomwa, hivyo unajua ikiwa ujumbe umesomwa.
Kichupo cha Mwenyeji Mwenza
Kichupo kipya kinakuwezesha kutazama Wenyeji Wenza wote na kusimamia ruhusa na malipo yao.
Ufikiaji wa Mapema
Sasa unaweza kujaribu vipengele vipya, kisha utusaidie kuvirekebisha kwa kushiriki maoni yako.
Mchanganuo wa bei
Mchanganuo wa bei uliosasishwa unaonyesha kile ambacho wageni wanalipa na kile unachopata.
Linganisha matangazo sawia
Linganisha bei yako na bei ya wastani ya matangazo sawia yaliyo karibu ili uendelee kuwa na ushindani.
Mipangilio ya bei na upatikanaji
Nyenzo za kalenda zilizoboreshwa zimesasishwa ili kuwa na hali thabiti ya utumiaji katika vifaa vyote.
Mapunguzo ya kila wiki na kila mwezi
Tumia kitelezeshi kipya ili kuweka au kurekebisha mapunguzo, huku pia ukiona bei ambayo wageni watalipa.
Kalenda ya mwaka kwenye simu
Hivi karibuni, unaweza kuona upatikanaji wako kwa mwaka na bei ya kila mwezi, kwenye skrini moja.
Maelezo mahususi ya kutoka
Weka maombi maalumu kwenye maelekezo yako ya kutoka ambayo ni ya kipekee kwa nyumba yako.
Taarifa ya kutoka ya kiotomatiki
Wageni watatumiwa maelezo yako ya kutoka kiotomatiki siku moja kabla ya kuondoka.
Arifa za kutoka za mbofyo mmoja
Kwa kugusa tu, wageni sasa wanaweza kukujulisha wakati waliotoka kwenye sehemu yako.
Majibu ya haraka ya kutoka
Tumia majibu ya haraka na ujumbe ulioratibiwa ili kushiriki kwa urahisi maelekezo yako ya kutoka.
Soma vidokezi vya Wenyeji wa Vyumba
Wasifu wa Mwenyeji wa Vyumba vya Airbnb sasa unaonyesha nukuu maarufu kuhusu Mwenyeji.
Ukweli wa kufurahisha kwenye wasifu
Pangilia wasifu wako kwa namna ya kufurahisha, maelezo mapya kama vile wimbo wako ulioupenda ukiwa shule ya sekondari ya juu.
Historia ya safari ya mwenyeji
Shiriki safari ulizofanya kwenye Airbnb ili kuwapa wageni hisia nzuri ya namna safari yako ilivyokuwa.
Mapendeleo ya mwenyeji
Sasa unaweza kuchagua mambo unayopenda kutoka kwenye orodha iliyowekwa mapema ili kusaidia kupata mambo ambayo wewe na mgeni mnayapenda kwa pamoja.
Wasifu wa mgeni wa kina zaidi
Wageni wanaweza kuongeza maelezo mapya kwenye wasifu wao, kwa hivyo unajua zaidi kuhusu anayeweka nafasi.
Mialiko Rahisi ya Mwenyeji Mwenza
Sasa ni rahisi zaidi kukaribisha Wenyeji Wenza ili kusaidia kusimamia matangazo yako.
Ruhusa mpya za Mwenyeji Mwenza
Weka ruhusa mpya, ukichagua: ufikiaji kamili, kalenda na kikasha pokezi, au kalenda tu.
Malipo mapya ya Mwenyeji Mwenza
Sasa unaweza kushiriki malipo na Mwenyeji Mwenza kama asilimia au kiasi kisichobadilika.
Kuthibitisha utambulisho wa wageni
Wageni wote wanaoweka nafasi duniani kote watapitia mchakato wa kuthibitisha utambulisho wao.
Ukaguzi wa uwekaji nafasi duniani
Teknolojia ambayo husaidia kupunguza hatari ya sherehe na uharibifu sasa inapatikana ulimwenguni kote.

Airbnb Vyumba: Kukiwa na safu mpya ya Mjue Mwenyeji

Kipengele kipya cha vyumba vya kujitegemea, kukiwa na safu ya Mjue Mwenyeji ili kuwasidia wageni wakujue kabla hawajaweka nafasi na nyenzo za utafutaji zinazofanya tangazo lako lionekane.

Mjue Mwenyeji

Shiriki na wageni maelezo kukuhusu, kama vile mambo unayopenda, jina la mnyama kipenzi, mambo ya kufurahisha na kinachofanya kukaa kwako kuwe maalumu.

Vichujio vilivyobuniwa upya

Vichujio vilivyosasishwa hufanya iwe rahisi kwa wageni kubadili baina ya aina za sehemu za kukaa na kuangalia kwa urahisi bei za wastani za vyumba na nyumba.

Aina ya Airbnb Vyumba

Ni rahisi kuliko hapo awali kwa wageni kugundua matangazo ya Airbnb Vyumba yaliyo na aina mpya iliyoonyeshwa juu ya ukurasa wetu wa kwanza.