Ipe biashara yako mazingira mapya

Sasa huduma yako inaweza kufikia mamilioni ya watu kwenye Airbnb.

Toa kile unachofanya vyema zaidi kupitia Huduma za Airbnb

Airbnb ni kwa ajili ya zaidi ya nyumba. Sasa ni kwa ajili ya biashara kama yako.
Kuandaa chakula
Wapishi
Mitindo ya nywele
Upodoaji
Usingaji
Huduma za kucha
Mazoezi ya viungo kwa mtu binafsi
Kupiga picha
Vyakula vilivyoandaliwa
Huduma za spa

Karibisha ulimwengu wa wateja wapya

Fikia mamilioni ya watu wanaosafiri na wanaoishi karibu nawe kwenye Airbnb.
Wageni milioni 390
waliwasili mwaka 2024
USD bilioni 81
zilitumika kwenye Airbnb mwaka 2024
Idadi ya milioni 390 inajumuisha wageni wapya na wanaorudi. Jumla ya nafasi zilizowekwa za USD bilioni 81 kwa ajili ya sehemu za kukaa na matukio.

Jitokeze kwa uzuri. Wekewa nafasi papo hapo.

Unda tangazo bora na ujaze kalenda yako kupitia kipengele cha kuweka nafasi papo hapo.

Maswali yako yamejibiwa

Maswali yanayoulizwa sana
Je, huduma yangu inafaa kuwekwa kwenye Airbnb? Huduma za Airbnb ni soko la huduma zenye ubora wa juu ambazo hufanya ukaaji wa mgeni kuwa bora zaidi. Huduma zinajumuisha kuandaa chakula, wapishi, mitindo ya nywele, upodoaji, usingaji, huduma za kucha, mazoezi ya viungo kwa mtu binafsi, upigaji picha, vyakula vilivyoandaliwa na huduma za spa. Pata maelezo zaidi kuhusu viwango vya Huduma kwenye Airbnb.Ninawezaje kutuma maombi? Ni rahisi kuanza. Kwanza, tueleze kidogo kukuhusu na huduma unayotoa. Kisha, weka picha, weka bei yako na uwasilishe tangazo lako ili litathminiwe. Tunaweza kuwasiliana nawe tukiwa na mabadiliko yaliyopendekezwa, maombi ya kupakia leseni au kuomba uthibitisho wa bima. Mara baada ya tangazo lako kuidhinishwa, unaweza kulichapisha na kuanza kutoa huduma yako kwa wateja moja kwa moja. Anza.Ada za Airbnb ni zipi? Kuunda na kuwasilisha tangazo ili litathminiwe ni bila malipo. Airbnb hukata kiotomatiki ada ya huduma ya asilimia 15 kutoka kwenye malipo ya kila huduma iliyowekewa nafasi.