Ni rahisi kutangaza nyumba yako kwenye Airbnb

Unda tangazo la sehemu yako kwa hatua chache tu
Nenda kwa kasi yako mwenyewe na ufanye mabadiliko wakati wowote
Pata usaidizi wa ana kwa ana kutoka kwa wenyeji wazoefu wakati wowote
Mwenyeji mwenza anaweza kukaribisha wageni kwa niaba yako
Sasa unaweza kuajiri mwenyeji mwenza mkazi mwenye ubora wa juu ili atunze nyumba yako na wageni.
Wenyeji wenza wanaweza kufanya yote

Weka tangazo lako
Piga picha, weka bei na unda mwongozo wa kuwasili

Andaa nyumba yako
Andaa, fanya usafi na utunze nyumba yako

Simamia nafasi ulizowekewa
Fahamu shughuli zote za nafasi ulizowekewa na ujumbe wa wageni

Wasaidie wageni wako
Shughulikia maombi ya kuingia, kutoka na kwenye eneo

Haijalishi unakaribisha wageni vipi, unalindwa
Ulinzi kamili, unajumuishwa kila unapokaribisha wageni kwenye nyumba yako kwenye Airbnb.
Hadi USD milioni 3 za ulinzi wa uharibifu | |
---|---|
Hadi USD milioni 1 ya bima ya dhima | |
Mawasiliano ya usalama saa 24 |
Ulinzi Dhidi ya Uharibifu kwa Mwenyeji hufidia uharibifu fulani wa mgeni wakati wa ukaaji wa Airbnb. Si bima na inaweza kutumika ikiwa wageni hawatalipa. Bima ya dhima hutolewa na wahusika wengine. Angalia maelezo na vighairi.
Nyenzo zote unazohitaji ili kukaribisha wageni, zote katika programu moja

Kukaribisha wageni si kwa wamiliki wa nyumba pekee
Fleti zinazofaa Airbnb hufanya iwe rahisi kwako kupangisha, kukaribisha wageni na kupata mapato ya ziada unapokuwa mbali.
Maswali yako yajibiwa
Maswali yanayoulizwa sana
Je, nyumba yangu inafaa kwenye Airbnb?Pata maelezo zaidi kuhusu ada.
Wageni wa Airbnb wanapendezwa na sehemu za kila aina, vyumba vya ziada, fleti, nyumba, nyumba za likizo, hata nyumba za kwenye mti. Je, ni lazima nikaribishe wageni kila wakati? Hapana, unadhibiti kalenda yako. Unaweza kukaribisha wageni mara moja kwa mwaka, usiku chache kwa mwezi au mara nyingi zaidi. Ada za Airbnb ni zipi? Haulipishwi kuunda tangazo na Airbnb kwa kawaida hukusanya ada ya huduma ya asilimia 3 ya jumla ndogo ya nafasi iliyowekwa mara tu unapolipwa. Katika maeneo mengi, Airbnb hukusanya na kulipa kodi za mauzo na utalii kiotomatiki kwa niaba yako. Mambo ya msingi kuhusu kukaribisha wageni
Ninaanzaje?Weka tangazo lako. Ninawezaje kuandaa nyumba yangu kwa ajili ya wageni? Hakikisha kwamba nyumba yako ni safi, haina mparaganyo na kwamba kila kitu kinafanya kazi vizuri. Vitu kama vile mashuka safi na vifaa vya usafi wa mwili husaidia kuunda sehemu ya kukaa yenye starehe na ya kuvutia. Angalia mwongozo wetu wa kuandaa nyumba yako. Ninalindwa vipi ninapokaribisha wageni? AirCover kwa ajili ya Wenyeji hutoa ulinzi kamili kila wakati unapokaribisha wageni kwenye nyumba yako kwenye Airbnb. Pata maelezo zaidi kuhusu AirCover kwa ajili ya Wenyeji na kile kinachojumuishwa. Je, kuna vidokezi vyovyote kuhusu kuwa mwenyeji bora? Kuanzia kushiriki orodha ya maeneo unayopenda mahali ulipo hadi kujibu haraka ujumbe wa wageni, kuna njia nyingi za kuwa mwenyeji bora. Pata vidokezi zaidi vya kukaribisha wageni.
Unaweza kuunda tangazo katika hatua chache tu, hayo yote kwa kasi yako mwenyewe. Anza kwa kutuambia kuhusu nyumba yako, piga picha kadhaa na uweke maelezo kuhusu kinachofanya iwe ya kipekee. Bima na kanuni
Je, kuna kanuni zozote zinazotumika katika jiji langu? Pata maelezo zaidi kuhusu kukaribisha wageni kwa kuwajibika. Itakuwaje ikiwa nina maswali mengine? Wenyeji wakazi ni chanzo kizuri cha taarifa na vidokezi. Tunaweza kukuunganisha na mwenyeji mzoefu wa Airbnb katika eneo lako ambaye anaweza kujibu maswali ya ziada. Muulize mwenyeji.
Baadhi ya maeneo yana sheria na kanuni za kukaribisha wageni kwenye nyumba yako. Ni muhimu ujifahamishe sheria zozote ambazo zinaweza kuhusika katika eneo lako. Pia, kulingana na mahali unapoishi, unaweza kuhitaji kuwasiliana na HOA yako, kusoma mkataba wako wa upangishaji au kumjulisha mwenye nyumba wako au majirani kuhusu mipango yako ya kukaribisha wageni kwenye Airbnb. Wenyeji wenza
Je, wenyeji wenza wanaweza kukusaidia kufanya nini?kuajiri mwenyeji mwenza afanye jambo moja au kila kitu. Ingawa kila mwenyeji mwenza hutoa huduma tofauti, anaweza kusaidia katika mambo kama vile kuweka tangazo lako la Airbnb, kuandaa nyumba yako, kusimamia nafasi zilizowekwa na ujumbe, kufanya usafi na matengenezo na kusaidia katika maombi kwenye sehemu hiyo ambayo wageni wako wanaweza kuwa nayo. Je, ninaweza kupata mwenyeji mwenza kwenye Airbnb? Airbnb inafanya iwe rahisi kupata na kuajiri mwenyeji mwenza mkazi mwenye ubora wa juu katika programu ya Airbnb. Tathmini, tuma ujumbe na uchague mwenyeji mwenza anayefaa zaidi mahitaji yako. Pata maelezo kuhusu Mtandao wa Wenyeji Wenza. Nitamlipaje mwenyeji mwenza wangu? Wewe na mwenyeji mwenza mnapaswa kukubaliana kuhusu masharti ya malipo kabla hajaanza kukusaidia. Una chaguo la kushiriki na mwenyeji mwenza wako sehemu ya malipo ya kila nafasi iliyowekwa moja kwa moja kupitia Airbnb. Masharti fulani yanaweza kutumika, kulingana na eneo lako na pia eneo la tangazo lako na mwenyeji mwenza. Pata maelezo kuhusu jinsi malipo ya mwenyeji mwenza yanavyofanya kazi.
Unaweza Wenyeji kwenye Mtandao wa Wenyeji Wenza kwa kawaida wana ukadiriaji wa juu, viwango vya chini vya kughairi na uzoefu thabiti wa kukaribisha wageni wa Airbnb. Ukadiriaji unategemea tathmini za wageni kwa matangazo wanayokaribisha wageni au kushirikiana kukaribisha wageni na huenda usiwakilishe huduma za kipekee za mwenyeji mwenza.
Mtandao wa Wenyeji Wenza unaendeshwa na Airbnb Global Services Limited, Airbnb Living LLC na Airbnb Plataforma Digital Ltda. Unapatikana katika maeneo mahususi pekee. Pata maelezo zaidi.