Sasisho la Mwaka 2022

Kupambana na ubaguzi na kujenga ujumuishaji

Mradi wa Mnara wa Taa

Mradi wa Mnara wa Taa, uliozinduliwa mwaka 2020, husaidia kugundua na kushughulikia tofauti katika jinsi watu wasio weupe wanavyohudumiwa kwenye Airbnb. Tumeanzisha mpango huu kwa kushirikiana na Color Of Change na kwa mwongozo kutoka kwa mashirika kadhaa ya haki za raia na faragha. Pata maelezo zaidi
Kutumia takwimu halisi
Tunachunguza jinsi wageni na Wenyeji wanavyotumia tovuti yetu. Uchambuzi wa kitakwimu hutusaidia kupata fursa za kuunda huduma za usawa zaidi katika jumuiya yetu.
Kulinda faragha
Tunachambua mielekeo kwa wingi na hatuhusishi taarifa ya mbari inayodhaniwa na watu au akaunti mahususi.
Kuboresha kila wakati
Timu yetu inaendelea kutambua njia mpya za kuifanya Airbnb iwe ya haki, yenye usawa na jumuishi zaidi.

Kile ambacho tumebadilisha

Kuondoa picha za wasifu za wageni kabla ya kuweka nafasi
Mwaka 2018, tulitekeleza mabadiliko ili kuhakikisha kwamba Wenyeji wataona picha ya mgeni kwenye mchakato wa kuweka nafasi baada ya kukubali ombi la kuweka nafasi pekee. Uchambuzi umegundua kwamba mabadiliko haya yameongeza kidogo Kiwango cha Mafanikio ya Kuweka Nafasi, kiwango ambacho wageni nchini Marekani kutoka kwa makundi tofauti ya mbari hufanikiwa kuweka nafasi kwenye tangazo la Airbnb, kwa wageni ambao wanachukuliwa kuwa ni Weusi.
Tathmini zaidi kwa wageni zaidi
Wageni wenye tathmini wana Kiwango cha juu cha Mafanikio ya Kuweka Nafasi. Lakini uchambuzi wetu uligundua kwamba wageni wanaoonekana kuwa Weusi au Walatino/Wahispania wana tathmini chache kuliko wageni wanaoonekana kuwa weupe au Waasia. Tunatekeleza mabadiliko ambayo yatafanya iwe rahisi kwa wageni wote kuandikiwa tathmini wanaposafiri.
Kufanya watu zaidi wastahiki kutumia kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo
Kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo kinamruhusu mgeni aweke nafasi kwenye tangazo bila kuhitaji idhini ya Mwenyeji. Ni nyenzo bora ya kupunguza ubaguzi kwa sababu inawezesha nafasi ziwekwe bila upendeleo. Tumeanzisha mabadiliko ili kufanya iwe rahisi kwa watu milioni 5 zaidi kutumia kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo.
Kuijenga jumuiya ya usafiri ambayo ni jumuishi zaidi
Usafiri zaidi ya vituo vya kitamaduni vya watalii unaweza kuleta fursa ya kiuchumi kwa jumuiya ambazo hazijafaidika kihistoria kutokana na utalii. Katika mwaka ujao, tutaendelea kukuza na kuongeza mipango ya kimataifa kama vile Chuo cha Ujasiriamali cha Airbnb ili kuhakikisha ufikiaji mpana wa faida za kukaribisha wageni kwenye Airbnb. Jitihada zetu zinajumuisha kupanua mipango ambayo husaidia kuwaandikisha Wenyeji zaidi ambao ni watu wasio weupe.
Kupanua elimu kwa ajili ya Wenyeji
Jumuiya yetu ya Wenyeji ina jukumu muhimu katika kuunda huduma ya usawa na ya ukarimu. Mwaka huu, tulizindua Mwongozo wa Ukaribishaji Wageni Jumuishi wenye makala na video za kuelimisha ili kuwasaidia Wenyeji wawakaribishe wageni wenye uwezo, wa jinsia na kutoka jamii zote, hasa wale kutoka jumuiya zilizotengwa kihistoria. Tunatarajia kuanzisha mipango zaidi ya kielimu na vipengele vya huduma ili kujenga ujumuishaji.
Kukagua nafasi zilizowekwa zilizokataliwa ili kuondoa fursa za upendeleo
Tunajua kwamba kuna sababu halali zinazofanya nafasi iliyowekwa isifanye kazi: kalenda ya Mwenyeji inaweza kuwa imebadilika au mgeni anaweza kuwa na hitaji, kama vile kuingia mapema au kuleta wageni wa ziada, ambalo Mwenyeji hawezi kulitimiza. Tunapanua uwezo wetu wa kuchambua nafasi zilizowekwa ambazo zimekataliwa ili kusaidia kuboresha sera na huduma zetu na kupambana na ubaguzi.
Kuboresha huduma ya kuweka nafasi tena
Chini ya Sera yetu ya Kufikiwa kwa Urahisi, iliyoanzishwa mwaka 2016, wageni walio na nafasi zilizowekwa za sasa au zijazo ambao wanaripoti kubaguliwa hupata msaada wa kuweka nafasi kwenye tangazo mbadala. Hivi karibuni tulizindua Mawasiliano ya Usalama Saa 24 yaliyoundwa ili kufanya iwe rahisi kwa wageni kwenye safari kupata msaada wa haraka, ikiwemo ufikiaji wa usaidizi wa kuweka nafasi tena.
Kuendelea na ahadi yetu kwa wageni walio na matatizo ya kutembea
Vichujio vya utafutaji vya kipengele chetu cha ufikiaji hufanya iwe rahisi kwa wageni kupata na kuweka nafasi kwenye sehemu za kukaa zinazokidhi mahitaji yao. Kupitia Tathmini ya Ufikiaji, tunatathmini kila kipengele cha ufikiaji kinachowasilishwa na Wenyeji ili kuhakikisha kwamba ni sahihi. Aina yetu ya Zinazofikika, iliyozinduliwa mwezi Novemba mwaka 2022, ina mamia ya matangazo yaliyobadilishwa kwa ajili ya ufikiaji wa kiti cha magurudumu, yaliyo na vijia visivyo na ngazi vilivyothibitishwa vya kuingia kwenye nyumba, chumba cha kulala na bafu na angalau kipengele kimoja cha ufikiaji kwenye bafu. Matangazo Yanayofikika hufanyiwa uchanganuzi wa 3D ili kuthibitisha vipengele na vipimo.

Ahadi ya Jumuiya ya Airbnb

Tangu mwaka 2016, tumemwomba kila mtu anayetumia Airbnb ajizatiti kuwatendea wengine kwa heshima, bila kuhukumu au kupendelea, kwa kukubali Ahadi ya Jumuiya ya Airbnb. Mtu yeyote asiyekubali huondolewa kwenye tovuti yetu, kufikia mwaka 2022, hao ni watu milioni 2.5.

Soma ripoti kamili

Sasisho la Miaka Sita la Kazi ya Airbnb ya Kupambana na Ubaguzi na Kujenga Ujumuishaji linajumuisha matokeo muhimu ya Mradi wa Mnara wa Taa, seti yetu kamili ya takwimu na maendeleo ambayo tumefanya tangu mwaka 2016.
Tazama ripoti

Kutana na washirika wetu

Tangu mwaka 2016, tumeshauriana na kushirikiana na makundi maarufu ya haki za raia, wataalamu wa kimbari na mashirika ya faragha.