Kuwa mwenyeji wa tukio kwenye Airbnb
Pata mapato kwa kuwaongoza watu kwa shughuli unazozipenda.
Tukio ni nini?
Ni shughuli ambayo inazidi ziara au darasa la kawaida, iliyoandaliwa na kuongozwa na wenyeji kote ulimwenguni. Onyesha jiji lako, ufundi wako, itikadi yako, au utamaduni wako kwa kuwa mwenyeji wa tukio.
Unda shughuli, kwa namna yako
Ziara ya chakula kwa kutumia baiskeli, upigaji picha nyakati za usiku, vyakula vya tapas kwenye mashua, au yoga (pamoja na mbuzi). Unda na ubadilishe shughuli ya kipekee ambayo watu wanataka kujaribu.
Fanya ukipendacho (na ulipwe)
Chunguza sanaa ya mtaa ama urambazaji nyakati za jioni, geuza ukipendacho kuwa faida kuu. Pata mapato ya pesa bila kuihisi kuwa kama kazi.
Pata sauti kwa shughuli yako
Ongoza matembezi pamoja na mbwa wa uokoaji, au fundisha mitindo ya maadili. Ongeza uelewa wa kusudio lako kwa njia mpya kabisa.

Onyesha unachokijua

Matukio ya kila aina, kama kupika, ufundi, kuendesha mitumbwi na zaidi. Hakuna kikomo kwa yale uwezayo kufanya. Chunguza kategoria hizi zilizoonyeshwa.

Tamaduni na Historia
Elezea hadithi kuhusu alama maarufu za kijiografia katika jiji lako.
Vyakula na Vinywaji
Wakaribishe wageni katika ziara ya chakula, darasa la kupikia, tukio la eneo la kulia chakula, na mengine mengi.
Asili na nje ya nyumba
Ongoza matembezi ya nyanjani, michezo ya majini, shughuli za milimani, na mengine mengi.

Jiunge na jumuiya inayokua ya watu wadadisi

Wenyeji ni wapishi bingwa, wasanii, maDJ, na wataalamu wengine kwenye nyanja zao. Wanawafanya watu ulimwenguni kote wajisikie wameunganishwa, na kuwawezesha kuyafikia maeneo ya kipekee na shughuli ambazo haziwezi kupatikana mahali pengine popote.

DJ Jigüe
DJ Jigüe amejitolea kushiriki shauku yake kwa muziki wa Afro-Kuba. Baadhi ya wageni aliowafunulia kwenye historia ya muziki maarufu wa Kuba hata walienda kumuona akicheza kwenye tamasha huko Austin, Texas.
Cici
Mkaaji wa Shanghai na mwenyeji wa upishi Cici anaamini kupika kunaweza kuleta furaha. Huwakaribisha wageni jikoni mwake ili waweze kujifunza jinsi ya kuunda sambusa maarufu za Kichina kwa njia ya kufurahisha.

Tuko na wewe, katika hatua zote

Rasilimali kama makala pamoja na maarifa yaliyotengewa mahitaji ya uwekaji nafasi, usaidizi wako na wateja wako wa saa 24 kwa wateja, uelewa wa tukio lako, na mengine mengi.

Kazi
Kuratibu
Malipo
Utambuzi
Viafaa vilivyoundwa kwa ajili yako
Dashibodi kukupa ufahamu, maoni kuhusu jinsi ya kuboresha, uonekanaji kwa wageni ulimwenguni kote kupitia utafutaji na vichujio, malipo rahisi, na mengi zaidi.
Hadi kufikia bima ya $ milioni 1 kwa shughuli nyingi
Dumu kuwa na utulivu wa akili
Kwa matukio mengi, utawekewa bima ya hadi Dola milioni 1. Zaidi ya hayo, utapata usaidizi wa wateja wa saa 24 ili upate muda wa kushughulikia unachokipenda. Pata maelezo zaidi
Habari
Nyongeza
Matukio
Mwongozo wa kukufanya ukue
Vijarida vya kila wiki, makala, na rasilimali zimetolewa ili kukusaidia kufanikiwa katika kila hatua ya safari yako ya uwekaji nafasi.

Jinsi ya kuanza

Huu hapa ni muhtasari wa mchakato, kuanzia mwanzo hadi mwisho.

1
Jifunze viwango vyetu vya ubora
Hakikisha tukio lako linakidhi viwango vyetu vya utaalam, ufikiaji wa ndani, na muunganisho.
2
Unda ukurasa wa tukio
Ukurasa wako ndiyo njia ya watu kukupata. Tengeneza taswira ya kwanza nzuri kwa kuangazia utaalamu wako na kuweka picha za ubora wa juu.
3
Anza kukaribisha wageni kwa tukio lako
Ili mradi tukio lako linakidhi viwango, unaweza kuweka tarehe na kuanza kukaribisha wageni.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Je, ninahitaji kuwa na nyumba ili kuwa mwenyeji wa tukio?
La. Huhitaji kuwakaribisha wageni usiku mmoja katika nyumba au sehemu yako ili uwe mwenyeji wa tukio.
Je, muda wa kujitolea ni upi?
Unaweza kukaribisha wageni mara nyingi upendavyo—jisikie huru kubadilisha tarehe na nyakati zako mpaka utakapopata kinachokufaa zaidi.
Je, ninahitaji leseni ya biashara?
Kulingana na shughuli zinazohusika, matukio mengine yanaweza kuhitaji leseni ya biashara. Hakikisha umeangalia sheria za mitaa katika eneo lako ili uamue ni leseni gani zinahitajika kwa tukio lako, hasa ikiwa kuna chakula, pombe, au usafiri unaohusika. Jifunze zaidi