Ufikiaji kwenye Airbnb
Hivi ndivyo tunavyofanya iwe rahisi kusafiri nasi.
Aina ya Zinazofikika
Gundua nyumba za kipekee zilizo na vipengele vya ufikiaji vilivyothibitishwa ikiwemo vijia visivyo na ngazi vya kuingia kwenye nyumba, chumba cha kulala na bafu. Kila nyumba katika aina hii hufanyiwa uchanganuzi wa kina wa 3D ili kuthibitisha vipengele vyake vya ufikiaji na kuonyesha maelezo muhimu kama vile upana wa mlango.

Vichujio vya utafutaji vilivyoboreshwa
Tumerahisisha vichujio vyetu vya ufikiaji ili kutoa huduma bora zaidi ya utafutaji.

Tathmini ya ufikiaji
Huwa tunatathmini kila kipengele cha ufikiaji kinachowasilishwa na Wenyeji wa sehemu za kukaa ili kuhakikisha kipo sahihi.

Kuwasiliana moja kwa moja na Wenyeji kupitia ujumbe
Piga gumzo moja kwa moja na Wenyeji ili kupata taarifa zaidi kuhusu vipengele vya ufikiaji vya sehemu yao ya kukaa au Tukio.


Jinsi tunavyofanya Airbnb ifikike zaidi
Timu mahususi
Airbnb ina timu zinazozingatia kuunda bidhaa ambazo kila mtu anaweza kutumia. Timu hizi hufanya kazi na wahandisi, wabunifu na wengine kote katika kampuni ili kusaidia kuhakikisha kuwa bidhaa zetu zinaundwa kwa kuzingatia ufikiaji.
Utafiti na utetezi
Tunafanya utafiti na watu ambao wana mahitaji ya ufikiaji na kufanya kazi na wataalamu katika jumuiya.
Viwango vya ufikiaji vya kidijitali
Tunajitahidi kupata viwango vya ufikiaji vya kidijitali vilivyowekwa na Miongozo ya Ufikiaji wa Maudhui ya Tovuti. Tunawekeza pia kwenye nyenzo za majaribio za kiotomatiki ili kutusaidia kutambua matatizo zaidi.