Nembo ya Airbnb 2023 Toleo la Kiangazi
Toleo la Kiangazi

Tunakuletea Airbnb Vyumba na vipengele vipya 50 na zaidi

Airbnb Vyumba: Kukiwa na safu mpya ya Mjue Mwenyeji

Mtazamo wetu mpya kuhusu Airbnb ya awali unakuwezesha kupata uzoefu wa jiji kama mwenyeji kwa kukaa na mwenyeji mkazi, na sasa unaweza kumjua Mwenyeji wako kabla ya kuweka nafasi.

Mwelewe zaidi Mwenyeji wako

Safu za Mjue Mwenyeji zinajumuisha maelezo kuhusu yule utakayekaa naye, kama vile kazi yake, lugha anazozungumza na ukweli wa kufurahisha.

Soma tathmini na zaidi

Wanapenda kukaa na nini? Je, wageni wengine wanasema nini kuwahusu? Soma safu nzima ili uelewe.

Pata chumba sahihi chenye vipengele vipya muhimu

Aina mpya, mahususi

Sasa kuna aina iliyopangwa yenye zaidi ya vyumba vya kujitegemea milioni moja, kukiwa na ufikiaji wa sehemu za pamoja katika nyumba.

Vichujio vilivyobuniwa upya

Tumeboresha jinsi unavyobadilisha kati ya aina za maeneo na tunaonyesha bei ya wastani ya kila moja kwa ulinganisho rahisi.

Vipengele vipya vya faragha

Elewa iwapo ni mabafu ya pamoja, yaliyoambatishwa au ya kujitegemea, nani mwingine anayeweza kuwa hapo na iwapo kuna kufuli kwenye chumba.

Zaidi ya vipengele 50 vipya kulingana na maoni yako

Tumefanya maboresho katika hali zote za utumiaji wa Airbnb, kuanzia kujisajili hadi kutoka.

Onyesho la jumla ya bei

Angalia jumla ya bei, ikiwemo ada zote kabla ya kodi kwenye programu, ikiwemo matokeo ya utafutaji, kichujio cha bei, ramani na kurasa za tangazo.

Pini mpya ndogo kwenye ramani

Tumeongeza pini ndogo kwenye ramani zetu ili iwe rahisi kuona nyumba za Airbnb zinazopatikana zaidi katika maeneo unayotafuta.

Matamanio yaliyobuniwa upya

Pata mtazamo bora wa matamanio yako, kukiwa na kiolesura kilichobuniwa upya kinachotumia picha kubwa za nyumba ulizohifadhi.

Utafutaji kwa mwezi ulioboreshwa

Kupata sehemu za kukaa za muda mrefu ni rahisi na rahisi zaidi kwa kutumia kiolesura kipya cha saa ambacho kinakuwezesha kutafuta sehemu ya kukaa ya mwezi 1 hadi 12.

Maelekezo ya kutoka ya uwazi

Wenyeji wanaweza kushiriki maelekezo kuhusu jinsi ya kutoka kwenye nyumba yao katika ukurasa wao wa tangazo, kwa hivyo unajua nini cha kutarajia kabla ya kuweka nafasi.

Lipa kwa awamu

Tulishirikiana na Klarna ili uweze kulipa malipo 4 yasiyo na riba (Marekani na Kanada), au kila mwezi kwa ajili ya sehemu za kukaa zenye zaidi ya USD 500 (Marekani pekee).

Ramani za haraka

Kasi ya kuonyesha upya haraka hukuruhusu kuona matangazo mapya haraka unaposogeza ramani.

Pini thabiti kwenye ramani

Tumeboresha pini za ramani ili zikae zilipo unapokuza na kuzungusha ramani.

Utafutaji mahiri wa kujikamilisha kiotomatiki

Pata mapendekezo bora, majina sahihi zaidi ya mahali, na marudio machache wakati wa kutafuta.

Hifadhi matamanio kwa mguso mmoja

Hifadhi matangazo moja kwa moja kwenye matamanio yako ya sasa kutoka kwenye matokeo ya utafutaji kwa mbofyo mmoja tu.

Kalenda ya Matamanio

Kalenda iliyosasishwa hufanya iwe rahisi kuona upatikanaji wa nyumba zilizoorodheshwa.

Ujumbe wa matamanio

Sasa unaweza kuweka ujumbe binafsi kwenye nyumba kwenye matamanio yako.

Ada ya chini kwa ajili ya sehemu za kukaa kuanzia mwezi mmoja

Tumepunguza sana ada yetu ya huduma kwa wageni kuanzia mwezi wa nne wa sehemu ya kukaa.

Lipa kwa benki

Lipa kwa kutumia akaunti ya benki iliyounganishwa ili uokoe pesa kwenye sehemu za kukaa za siku 28 au zaidi (Marekani pekee).

Onyesho la malipo ya kila mwezi

Kwa sehemu za kukaa kuanzia mwezi mmoja, angalia kinachostahili kwa miezi ya sasa na ya baadaye wakati wa kutoka.

Vikumbusho vya kutoka

Pata kumbusho kuhusu kile unachohitaji kufanya ili kutoka, siku moja kabla ya kuondoka.

Maoni ya kutoka katika tathmini

Sasa unaweza kutoa maoni kuhusu kutoka kwako wakati wa kutathmini ukaaji.

Salio la kuweka nafasi tena papo hapo

Ikiwa Mwenyeji ataghairi katika dakika za mwisho, wageni wengi watapata salio la kuweka nafasi tena papo hapo.

Usaidizi wenye kipaumbele kwa wateja katika safari

Lengo la timu yetu maalumu ya usaidizi wa saa 24 ni kujibu asilimia 90 za simu kwa Kiingereza ndani ya dakika 2.

Umbali kutoka kwenye vivutio

Unatafuta alama maarufu kwenye Airbnb? Matokeo yataonyesha umbali kutoka katika kila nyumba.

Kuonyesha nyumba zinazofaa kwa watoto wachanga

Ikiwa unasafiri na mtoto, matokeo ya utafutaji yataangazia vistawishi kama vile vitanda vya watoto.

Kuonyesha nyumba zinazofaa kwa watoto

Ikiwa unasafiri na watoto, matokeo ya utafutaji yataonyesha vistawishi kama vile vyumba vya michezo.

Kuonyesha nyumba kwa ajili ya sehemu za kukaa kuanzia mwezi mmoja

Unapanga ukaaji wa muda mrefu? Matokeo ya utafutaji yataonyesha vistawishi kama vile sehemu mahususi za kufanyia kazi.

Kuthibitisha Utambulisho wa Wenyeji

Wenyeji wote wanaowekewa nafasi kwenye Airbnb watapitia mchakato wa kuthibitisha utambulisho wao ifikapo mwisho wa mwezi Juni.

Mchakato ulioboreshwa wa uthibitishaji wa utambulisho

Ilipohitajika, tulifanya iwe rahisi kuongeza taarifa zaidi ili kuthibitisha utambulisho wako.

Rufaa kwa uwekaji nafasi uliozuiwa

Sasa unaweza kukata rufaa dhidi ya nafasi iliyowekwa ambayo imezuiwa ikiwa imetambuliwa kimakosa kuwa ina hatari ya kufanya sherehe.

Kichujio cha bei ambacho ni thabiti

Bei hujirekebisha kiotomatiki unapotumia kichujio cha aina ya sehemu ya kukaa.

Kichujio cha mabafu ya Airbnb Vyumba

Unapoweka nafasi kwenye Airbnb Vyumba, sasa unaweza kutafuta mabafu ya kujitegemea yaliyoambatishwa.

Tumeweka pia vipengele vipya ili kufanya huduma ya kukaribisha wageni iwe rahisi

Wenyeji wanaona jumla ya bei

Wageni wanaweza kuona jumla ya bei yao ya kila usiku kwenye programu ili kujua kila wakati kile ambacho wageni watalipa.

Telezesha ili uchague tarehe

Wenyeji wanaweza kutelezesha kidole ili kuchagua tarehe kwenye kalenda, hakuna haja ya kugusa siku mojamoja.

Maelekezo ya kutoka ya programu

Wenyeji wanaweza kuunda maelekezo ya kutoka haraka zaidi kwa kuchagua kwenye orodha iliyowekwa tayari.

Arifa za ujumbe kusomwa

Wageni na Wenyeji wote wanapata arifa ya kuonyesha kuwa ujumbe umesomwa mara unapokuwa umefunguliwa.

Kichupo cha Mwenyeji Mwenza

Kichupo kipya kinawawezesha Wenyeji kutazama Wenyeji Wenza wote na kusimamia ruhusa na malipo yao.

Ufikiaji wa Mapema

Wenyeji sasa wanaweza kujaribu vipengele vipya, kisha watusaidie kuvirekebisha kwa kushiriki maoni.

Mchanganuo wa bei

Mchanganuo wa bei uliosasishwa unaonyesha kile ambacho wageni wanalipa na kile wanachopata Wenyeji.

Linganisha matangazo sawia

Wenyeji wanaweza kuona bei ya wastani ya matangazo sawia yaliyo karibu ili kuendelea kuwa na ushindani.

Mipangilio ya bei na upatikanaji

Nyenzo za kalenda zilizoboreshwa zimesasishwa ili kuwa na hali thabiti ya utumiaji katika vifaa vyote.

Mapunguzo ya kila wiki na kila mwezi

Wenyeji wanaweza kutumia kitelezeshi ili kuweka mapunguzo, huku pia wakiona bei ambayo wageni watalipa.

Kalenda ya mwaka kwenye simu

Hivi karibuni, Wenyeji wataweza kuona upatikanaji wao kwa mwaka na bei ya kila mwezi, kwenye skrini moja.

Maelezo mahususi ya kutoka

Wenyeji sasa wanaweza kufanya mchakato wa kutoka uwe rahisi na maelekezo dhahiri yanayohusu nyumba yao.

Taarifa ya kutoka ya kiotomatiki

Wageni watatumiwa maelezo ya kutoka kiotomatiki siku moja kabla ya kuondoka.

Arifa za kutoka za mbofyo mmoja

Kwa kugusa tu, wageni sasa wanaweza kuwajulisha Wenyeji wakati muda waliotoka kwenye sehemu yao.

Majibu ya haraka ya kutoka

Wenyeji wanaweza kutumia nyenzo zilizosasishwa za kikasha ili kushiriki kwa urahisi maelekezo yao ya kutoka.

Tathmini mambo yaliyoangaziwa kuhusu Wenyeji wa Vyumba

Wasifu wa Mwenyeji wa Airbnb Vyumba sasa unaonyesha nukuu maarufu kuhusu Mwenyeji.

Ukweli wa kufurahisha kwenye wasifu wa Mwenyeji

Wenyeji wanaweza kufanya wasifu wao kuwa mahususi kwa maelezo ya kufurahisha, kama vile wimbo walioupenda wakiwa shule ya sekondari.

Historia ya safari ya mwenyeji

Wenyeji wanaweza kushiriki safari zinazofanywa kwenye Airbnb ili kuwapa wageni uelewa mzuri kuhusu namna safari yao ilivyokuwa.

Mapendeleo ya mwenyeji

Wenyeji sasa wanaweza kuchagua mambo wanayopenda kutoka kwenye orodha iliyowekwa mapema ili kusaidia kupata mambo ambayo wewe na mgeni mnayapenda kwa pamoja.

Wasifu wa mgeni wa kina zaidi

Wageni sasa wanaweza kuongeza maelezo zaidi kwenye wasifu wao, ikiwemo mapendeleo na safari zilizopita.

Mialiko Rahisi ya Mwenyeji Mwenza

Sasa ni rahisi zaidi kwa Wenyeji kuwaalika Wenyeji Wenza ili wawasaidie kusimamia matangazo yao.

Ruhusa mpya za Mwenyeji Mwenza

Wenyeji wanaweza kuweka ruhusa mpya: ufikiaji kamili, kalenda na kikasha pokezi, au kalenda tu.

Malipo mapya ya Mwenyeji Mwenza

Wenyeji wanaweza kushiriki malipo na Mwenyeji Mwenza kama asilimia au kiasi kisichobadilika.

Kuthibitisha utambulisho wa wageni

Wageni wote wanaoweka nafasi duniani kote watapitia mchakato wa kuthibitisha utambulisho wao.

Ukaguzi wa uwekaji nafasi duniani

Teknolojia ambayo husaidia kupunguza hatari ya sherehe na uharibifu sasa inapatikana ulimwenguni kote.

Kutolewa kwa kipengele na upatikanaji wa huduma unaweza kutofautiana kulingana na eneo.