Kadi za zawadi za Airbnb
Unatoa. Wanaenda.
Peleka ulimwengu wa Airbnb kwa marafiki na familia. Sherehekea sikukuu, tambua nyakati muhimu na uhamasishe kusafiri. Wasaidie kwenda popote, wakati wowote, kwa kuwa muda wake wa matumizi hauishi kamwe.
Unafanya ununuzi kwa ajili ya biashara?Chagua muundo wako
Ubunifu wa kuhamasisha
Kadi za zawadi zinaweza kufanywa mahususi kwa kutumia muundo utakaochagua, ujumbe na kiwango cha zawadi
Rahisi kutuma
Inawasili ndani ya dakika chache kupitia ujumbe au barua pepe na tutathibitisha kuwa imepokelewa
Haiishi muda wake wa matumizi kamwe
Salio la zawadi linapatikana kwa ajili ya kutumiwa wakati wowote wanapokuwa tayari kusafiri
Kadi za zawadi kwa ajili ya biashara
Onyesha shukrani zako kwa wafanyakazi na wateja kupitia zawadi ambayo ni rahisi kutoa kwa tukio lolote.wasiliana na kitengo cha mauzo.
Kutoa oda ya USD 10,000 au zaidi, Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Kwa maswali zaidi tembelea Kituo cha Msaada.
Je, kadi za zawadi ni halisi au ni za kidijitali?
Kadi za zawadi zinazonunuliwa kwenye Airbnb.com nchini Marekani zinaweza kununuliwa kama kadi za zawadi za kielektroniki (eGift), ambazo zinatumwa kupitia ujumbe au barua pepe, au kadi halisi za zawadi ambazo zitatumwa kwenye anwani ya mpokeaji aishiye Marekani.
Ninaweza kununua wapi kadi halisi ya zawadi?
Unaweza kuagiza kadi halisi ya zawadi hapa au unaweza kununua kwenye vituo vinavyoshiriki vya maduka ya Target, Walmart, Best Buy, CVS, Walgreens, Kroger, Safeway na Whole Foods.
Je, kadi za zawadi zinakwisha muda wa kutumika?
Hapana, kadi zetu za zawadi haziishi muda wa matumizi.
Kadi za zawadi zinapatikana wapi?
Kadi za zawadi za Airbnb zinapatikana katika nchi nyingi duniani kote. Unaweza kupata orodha kamili ya nchi zinapopatikana na Masharti husika ya Kadi ya Zawadi hapa.
Je, ninaweza kumtumia kadi ya zawadi mtu anayeishi katika nchi tofauti?
Kadi za zawadi zinazonunuliwa nchini Marekani zinaweza kukombolewa tu na watumiaji wanaoishi nchini Marekani. Mpokeaji wa kadi ya zawadi lazima pia awe na njia halali ya malipo nchini Marekani.
Ninawezaje kuangalia salio la kadi yangu ya zawadi?
Mara baada ya kukomboa kadi yako na kuweka fedha kutoka kwenye kadi hiyo katika akaunti yako, unaweza kwenda kwenye njia za Malipo katika Akaunti yako na uangalie salio lako.
Airbnb inakubali njia zipi za malipo?
Kwa sasa tunakubali kadi maarufu za benki na Apple Pay kwa ajili ya kadi za zawadi za zilizonunuliwa kwenye Airbnb.
Kwa maswali zaidi tembelea Kituo cha Msaada.