AirCover kwa ajili ya Wenyeji
Uthibitishaji wa utambulisho wa mgeni
Mfumo wetu kamili wa uthibitishaji hukagua maelezo kama vile jina, anwani, kitambulisho cha serikali na kadhalika ili kuthibitisha utambulisho wa wageni wanaoweka nafasi kwenye Airbnb.
Ukaguzi wa nafasi iliyowekwa
Teknolojia tunayomiliki inachambua mamia ya mambo katika kila nafasi iliyowekwa na inazuia baadhi ya nafasi zilizowekwa ambazo zinaonyesha hatari kubwa ya sherehe zenye kuvuruga na uharibifu wa mali.
Ulinzi dhidi ya uharibifu wa USD milioni 3
Ikiwa wageni hawalipii uharibifu uliofanywa kwenye nyumba na mali yako, ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji umewekwa ili kusaidia kulipia gharama za hadi USD Milioni 3, ikiwemo ulinzi huu maalumu:
Sanaa na vitu vya thamani
Rudishiwa pesa kwa ajili ya sanaa au vitu vya thamani vilivyoharibiwa.
Magari na boti
Rudishiwa pesa kwa uharibifu wa magari, maboti na vyombo vingine vya kwenye maji ambavyo unaegesha au kuhifadhi nyumbani kwako.
Uharibifu unaosababishwa na mnyama kipenzi
Rudishiwa pesa kwa ajili ya uharibifu uliosababishwa na mnyama kipenzi wa mgeni.
Kupotea kwa mapato
Ikiwa itabidi ughairi nafasi zilizowekwa za Airbnb kwa sababu ya uharibifu wa mgeni, utalipwa fidia kwa mapato yaliyopotea.
Usafi wa kina
Fidiwa kwa ajili ya huduma za kufanya usafi wa ziada zinazohitajika ili kuondoa madoa na harufu ya moshi.
Bima ya dhima ya USD Milioni 1
Ulinzi katika tukio nadra ambapo mgeni atajeruhiwa au mali yake kuharibiwa au kuibwa.
Mawasiliano ya usalama saa 24
Endapo utajihisi kwamba hauko salama, programu yetu itakupa ufikiaji wa kubofya mara moja kwa maafisa wa usalama waliopata mafunzo mahususi, mchana au usiku.
Ni Airbnb pekee inayokupa AirCover
Airbnb | Washindani | |
---|---|---|
Uthibitishaji wa utambulisho wa mgeni | ||
Ukaguzi wa nafasi iliyowekwa | ||
Ulinzi dhidi ya uharibifu wa USD milioni 3 | ||
Sanaa na vitu vya thamani | ||
Magari na boti | ||
Uharibifu unaosababishwa na mnyama kipenzi | ||
Kupotea kwa mapato | ||
Usafi wa kina | ||
Bima ya dhima ya USD Milioni 1 | ||
Mawasiliano ya usalama saa 24 |