AirCover kwa ajili ya Wenyeji

Ulinzi kamili.
Unajumuishwa kila wakati, bila malipo.
Kwenye Airbnb pekee.

Uthibitishaji wa utambulisho wa mgeni

Mfumo wetu kamili wa uthibitishaji hukagua maelezo kama vile jina, anwani, kitambulisho cha serikali na kadhalika ili kuthibitisha utambulisho wa wageni wanaoweka nafasi kwenye Airbnb.

Ukaguzi wa nafasi iliyowekwa

Teknolojia tunayomiliki inachambua mamia ya mambo katika kila nafasi iliyowekwa na inazuia baadhi ya nafasi zilizowekwa ambazo zinaonyesha hatari kubwa ya sherehe zenye kuvuruga na uharibifu wa mali.

Ulinzi dhidi ya uharibifu wa USD milioni 3

Ikiwa wageni hawalipii uharibifu uliofanywa kwenye nyumba na mali yako, ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji umewekwa ili kusaidia kulipia gharama za hadi USD Milioni 3, ikiwemo ulinzi huu maalumu:

Sanaa na vitu vya thamani

Rudishiwa pesa kwa ajili ya sanaa au vitu vya thamani vilivyoharibiwa.

Magari na boti

Rudishiwa pesa kwa uharibifu wa magari, maboti na vyombo vingine vya kwenye maji ambavyo unaegesha au kuhifadhi nyumbani kwako.

Uharibifu unaosababishwa na mnyama kipenzi

Rudishiwa pesa kwa ajili ya uharibifu uliosababishwa na mnyama kipenzi wa mgeni.

Kupotea kwa mapato

Ikiwa itabidi ughairi nafasi zilizowekwa za Airbnb kwa sababu ya uharibifu wa mgeni, utalipwa fidia kwa mapato yaliyopotea.

Usafi wa kina

Rudishiwa pesa kwa ajili ya huduma za kufanya usafi wa ziada zinazohitajika baada ya ukaaji wa mgeni, kwa mfano, kusafisha zulia kitaalamu.

Bima ya dhima ya USD Milioni 1

Ulinzi katika tukio nadra ambapo mgeni atajeruhiwa au mali yake kuharibiwa au kuibwa.

Mawasiliano ya usalama saa 24

Endapo utajihisi kwamba hauko salama, programu yetu itakupa ufikiaji wa kubofya mara moja kwa maafisa wa usalama waliopata mafunzo mahususi, mchana au usiku.

Pata maelezo kamili kuhusu jinsi AirCover kwa ajili ya Wenyeji inavyokulinda na vighairi vyovyote vinavyotumika.

Ni Airbnb pekee inayokupa AirCover

Airbnb
Washindani
Uthibitishaji wa utambulisho wa mgeni
Ukaguzi wa nafasi iliyowekwa
Ulinzi dhidi ya uharibifu wa USD milioni 3
Sanaa na vitu vya thamani
Magari na boti
Uharibifu unaosababishwa na mnyama kipenzi
Kupotea kwa mapato
Usafi wa kina
Bima ya dhima ya USD Milioni 1
Mawasiliano ya usalama saa 24
Ulinganisho unategemea taarifa ya umma na matoleo ya bila malipo ya washindani wakuu kufikia mwezi Oktoba mwaka 2022.

Majibu kwa maswali yako

Huwezi kupata kile unachotafuta? Tembelea Kituo chetu cha Msaada.

Njia rahisi sana ya kuweka eneo lako kwenye Airbnb

Kipengele cha Anza Kutumia Airbnb hufanya iwe rahisi kuweka eneo lako kwenye Airbnb, kikiwa na msaada wa moja kwa moja kutoka kwa Mwenyeji Bingwa kuanzia swali lako la kwanza hadi unapopata mgeni wako wa kwanza.