Kila nafasi iliyowekwa kwenye nyumba inakuwa na AirCover kwa ajili ya wageni. Ikiwa kuna tatizo kubwa kwenye nyumba yako ya Airbnb ambalo mwenyeji wako hawezi kulitatua, tuko hapa ili kukusaidia.
Hapa ndipo tunaweza kusaidia:
Timu yetu inaweza kukusaidia kupata eneo kama hilo, kwa kuzingatia eneo na vistawishi, kulingana na upatikanaji kwa bei sawa. Ikiwa nyumba kama hiyo haipatikani au ungependa kutoweka nafasi tena, tutakurejeshea fedha zote au sehemu ya fedha, ikiwemo ada za huduma.
AirCover kwa ajili ya wageni hutoa usaidizi kwa matatizo makubwa kwenye uwekaji nafasi wako wa nyumba, kwa mfano:
AirCover kwa ajili ya wageni haijumuishi usumbufu mdogo zaidi, kama vile kiyoyozi kilichovunjika.
Mwenyeji wako ndiye mtu wako bora zaidi wa kuwasiliana naye ikiwa kuna jambo lolote litakalotokea. Unaweza kumtumia mwenyeji wako ujumbe moja kwa moja ili kumjulisha kinachoendelea. Tatizo likitokea wakati wa ukaaji wako:
Je, unahitaji kuwasiliana nasi? Wasiliana nasi kwa simu, barua pepe au gumzo.
Ikiwa utahisi hauko salama, tuko hapa kukusaidia kupata kipaumbele kwa wahudumu wa usalama waliopewa mafunzo maalumu ambao watakusaidia kutatua matatizo yako ya usalama au kukuunganisha moja kwa moja na mamlaka za dharura za eneo husika, mchana au usiku.
AirCover kwa ajili ya wageni si bima. Haishughulikii matatizo yanayohusiana na usafiri (kwa mfano: Safari yako imechelewa kwa sababu ya dhoruba au mizigo yako imeharibiwa na mtoa huduma wako). Pata maelezo zaidi kuhusu AirCover kwa ajili ya bima ya wageni na safari, uwekaji nafasi au ulinzi wa sehemu ya kukaa.
Ikiwa wewe ni mwenyeji, pata maelezo zaidi kuhusu AirCover kwa ajili ya Wenyeji na maboresho ambayo tumefanya.