Ikiwa chochote kitaenda mrama wakati wa ukaaji wako
Mtumie Mwenyeji wako ujumbe
Tatizo likitokea, jaribu kuzungumza na Mwenyeji wako kwanza. Unaweza kumtumia Mwenyeji wako ujumbe moja kwa moja kutoka kwenye kikasha chako ili kumjulisha kinachoendelea.
Ikiwa unahitaji kuomba kurejeshewa fedha zote au sehemu ya fedha kwa sababu ya tatizo hilo, kuna uwezekano mkubwa kwamba Mwenyeji wako atakubali ombi lako ikiwa mtaweza kukubaliana kuhusu kiasi kwanza.
Tuma ombi la kurejeshewa pesa
Hivi ndivyo unavyojiandaa:
- Kusanya ushahidi: Ikiwezekana, piga picha au video ili uweke kumbukumbu ya matatizo kama vile kistawishi kinachokosekana au kilichovunjika.
- Wasilisha ombi lako: Utaelezea tatizo hilo, utatoa picha au video ukiweza na kumjulisha Mwenyeji jinsi ungependa kutatua tatizo hilo.
- Subiri jibu: Ikiwa Mwenyeji wako atakataa au hatajibu, unaweza kuiomba Airbnb iingilie kati ili kukusaidia. Airbnb itarejelea Sera ya Kuweka tena Nafasi na Kurejesha Fedha ili kuamua ni msaada gani tunaweza kutoa.
Kuhusisha Airbnb
Ingawa kila wakati tunataka Wenyeji na wageni watatue masuala moja kwa moja ikiwa wanaweza, tunajua haiwezekani kila wakati. Tatizo likitokea ambalo huwezi kusuluhisha na Mwenyeji wako (au Mwenyeji wako akatae au akose kujibu ombi lako la kurejeshewa fedha), tujulishe na mwanatimu wetu ataingilia kati ili akusaidie.
Tukipata kwamba tatizo hili linalindwa na AirCover, tutakurejeshea fedha zote au sehemu ya fedha au kulingana na hali, tutakutafutia sehemu sawa na hiyo au bora ya kukaa.
Kumbuka kwamba una saa 72 za kuripoti tatizo lolote kwetu tangu wakati unapolifahamu.
Kumbuka: Katika hali ya dharura, au ikiwa usalama wako binafsi unatishiwa, wasiliana na polisi au huduma za dharura mahali uliko mara moja. Ikiwa hufahamu nambari za simu za huduma za dharura katika eneo lako, unaweza kuzipata kwenye programu ya Airbnb. Kwa matatizo mengine yoyote ya usalama, unaweza kuwasiliana nasi wakati wowote kupitia namba yetu mahususi ya Mawasiliano ya Usalama Saa 24. Soma zaidi kuhusu mbinu za kuwasiliana nasi katika Kituo chetu cha Msaada.
Makala yanayohusiana
- MgeniKile kinacholindwa na ambacho hakilindwi na AirCoverAirCover ni mpango wa ulinzi kamili unaojumuishwa bila malipo kwenye kila nafasi iliyowekwa na unakulinda dhidi ya matatizo mengi yanayoweza…
- MgeniKulindwa kupitia AirCoverAirCover ni ulinzi kamili kwa ajili ya wageni wa Airbnb.
- MgeniSera ya Kuweka Nafasi Tena na Kurejeshewa FedhaTafadhali kagua Sera yetu ya Kuweka Nafasi Tena na Kurejeshewa Fedha.