Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Jinsi ya kufanya
Mgeni

Tafuta Matukio yenye vipengele vya ufikiaji

Tunaamini kuwa mtu yeyote anaweza kujisikia nyumbani mahali popote—na tungependa kufanya iwe rahisi kwa watu wenye ulemavu na mahitaji mengine ya ufikiaji waweze kusafiri.

Sasa unaweza kutafuta Tukio ambalo linatoa vipengele vya ufikiaji kama vile bafu linaloweza kufikika au Tukio linalofanywa kwa lugha ya ishara.

Vipengele vya ufikiaji

Hivi ndivyo vipengele unavyoweza kutumia kuchuja Matukio:

Uwezo wa kutembea

 • Hakuna ngazi
 • Bafu linaloweza kufikika
 • Sehemu ya maegesho inayoweza kufikika
 • Ardhi imesawazishwa au ni tambarare

Mawasiliano

 • Taarifa za sauti au maneno
 • Lugha ya ishara
 • Mbinu za kuwasiliana na kiziwi
 • Mwongozaji mteule wa kipofu

Hisia

 • Hakuna kichocheo cha hisia kali
 • Sehemu tulivu ya mapumziko

Watoa huduma za ufikiaji

 • Kiingilio bila malipo kwa watu wanaowasaidia wageni wenye ulemavu

Pata maelezo zaidi kuhusu watoa huduma za ufikiaji.

Ili kuchuja kulingana na vipengele vya ufikiaji:

 1. Weka mahali uendako na tarehe unayotaka (unazotaka)
 2. Mara baada ya matokeo yako ya utafutaji kuonekana, bofya Vichujio
 3. Bofya Chagua vipengele vya ufikiaji
 4. Chagua vipengele vyovyote utakavyohitaji ili kufurahia Tukio na ubofye Hifadhi

Mahali pa kupata taarifa ya ufikiaji kwenye tangazo la Tukio

Sasa kwa kuwa umepata Tukio linalotoa vipengele vya ufikiaji, hapa ndipo unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu vipengele vya ufikiaji vya Tukio hilo na uamue ikiwa vinakidhi mahitaji yako.

 • Maelezo ya Tukio: Wenyeji wanaweza kuweka taarifa za vipengele vya ufikiaji katika maelezo ya Tukio
 • Sehemu ya ufikiaji: Wenyeji watakuwa wameweka maelezo ya kina kwa ajili ya kipengele chochote cha ufikiaji walichochagua
 • Kitufe cha kuwasiliana na Mwenyeji: Ikiwa ungependa taarifa zaidi kuhusu vipengele vya ufikiaji vya Tukio au ikiwa unahitaji mtoa huduma wa ufikiaji ashiriki katika Tukio pamoja na wewe, unaweza kumtumia Mwenyeji ujumbe moja kwa moja

Sera ya Kutobagua

Kama sehemu ya ahadi yetu ya ujumuishaji na heshima kwa kila mtu katika jumuiya yetu, Sera yetu ya Kutobagua haiwaruhusu Wenyeji kumkataa mgeni kwa sababu tu ana ulemavu. Tunatia juhudi ili kuifanya jumuiya ya Airbnb kuwa ya kufaa zaidi kwa walemavu kwa kuwapa Wenyeji na wageni fursa za kushiriki taarifa ya ufikiaji.

Je, makala hii ilikusaidia?

Makala yanayohusiana

Pata msaada kuhusu nafasi ulizoweka, akaunti na kadhalika.
Ingia au ujisajili