Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Jinsi ya kufanya
Mwenyeji

Kuweka vipengele vya ufkiaji kwenye matangazo

Inafurahisha unapoweza kukaribisha watu zaidi kwenye eneo lako kwa kuweka vipengele vya ufikiaji, wageni wengi hutafuta nyumba kulingana na mahitaji mahususi.

Jinsi inavyofanya kazi

Kwanza, hakikisha tangazo lako limechapishwa. Kisha unaweza kuhariri tangazo kulingana na chumba na uonyeshe kila kipengele cha ufikiaji kwa kuweka angalau picha moja iliyo dhahiri.

Hariri tangazo lako ili kujumuisha vipengele vya ufikiaji

  1. Nenda kwenye Menyu, chagua Matangazo kisha ubofye tangazo unalotaka kuhariri (Tafadhali kumbuka: tangazo lako linahitaji kuwa tayari limechapishwa ili kuweka vipengele hivi).
  2. Nenda kwenye Vipengele vya ufikiaji
  3. Kwa kila kipengele ulichonacho, gusa Nina kipengele hiki. Pia utakumbushwa kuweka picha.
  4. Mara baada ya kuweka picha, bofya Hifadhi.

Utahitajika kuweka angalau picha moja kwa kila kipengele. Vipengele na picha zote lazima zikidhi miongozo yetu hapa chini. Mara baada ya vipengele vyako kuthibitishwa kulingana na miongozo yetu ya picha, vitaonyeshwa kwenye sehemu ya vipengele vya Ufikiaji ya tangazo lako.

Hariri chumba chako ili kujumuisha vipengele vya ufikiaji

  1. Nenda kwenye Menyu, chagua Matangazo, kisha ubofye kadi ya tangazo unalotaka kuhariri
  2. Chini ya Sehemu yako ya kihariri tangazo, nenda kwenye Ziara ya Picha
  3. Chagua chumba, bofya Vipengele vya ufikiaji, kisha uweke vipengele vyako vya ufikiaji.

Utahitajika kuweka angalau picha moja kwa kila kipengele. Vipengele na picha zote lazima zikidhi miongozo yetu hapa chini. Mara baada ya vipengele vyako kuthibitishwa kulingana na miongozo yetu ya picha, vitaonyeshwa kwenye sehemu ya vipengele vya Ufikiaji ya tangazo lako.

Ikiwa umeunganishwa kwenye Airbnb kupitia meneja wa chaneli au programu ya usimamizi wa nyumba kwenye uoanishaji kamili, utahitaji kusasisha vistawishi vyako vya ufikiaji kupitia programu yako ya API. Wasiliana na mtoa huduma wako wa programu ya API ili kumuuliza kuhusu ratiba yake ya kutoa kipengele cha API ya Ufikiaji ili uweze kuweka vistawishi vyako.

Pata maelezo zaidi kuhusu kujisikia nyumbani na ujumuishaji katika Airbnb kwenye sera yetu ya ufikiaji.

Ufafanuzi wa vipengele vya ufikiaji na miongozo ya picha

Ili kubainisha vipengele vya ufikiaji ulivyonavyo, rejelea maelezo yaliyo hapa chini na uhakikishe kuwa chumba chako au sehemu yako inakidhi matakwa haya kabla ya kuchagua kipengele hicho. Hakikisha unaangalia mwongozo wa Airbnb wa kupiga picha vipengele vya ufikiaji.

Kwa ajili ya tangazo lako

Maegesho yanayofikika

Ufafanuzi wa kipengele:

Kuna eneo la maegesho binafsi lenye upana wa angalau futi 11 (mita 3.35). Au, kuna maegesho ya umma yaliyotengwa kwa ajili ya mtu mwenye ulemavu ambayo yana alama au ishara dhahiri.


Vigezo vya picha:

  • Kwa maeneo ya maegesho ya umma, onyesha ishara au alama ili kuashiria kwamba yametengwa kwa ajili ya watu wenye ulemavu
  • Kwa maeneo binafsi ya maegesho au barabara binafsi zinazoelekea kwenye nyumba, piga picha ukiwa mbali ili kuonyesha kwamba sehemu hiyo ina upana wa futi 11 (mita 3.35) au zaidi

Kijia chenye mwangaza kinachoelekeza kwenye mlango wa wageni

Ufafanuzi wa kipengele:

Njia au kijia kinachoelekea kwenye mlango wa mgeni kina mwanga wa kutosha usiku.


Vigezo vya picha:

  • Onyesha kwa udhahiri vyanzo vyote vya nuru vinavyoangazia kijia kinachoelekea kwenye mlango wa wageni
  • Usijumuishe vyanzo vya mwanga kutoka ndani ya nyumba
  • Hakikisha picha inaonyesha mahali taa zilipo kuhusiana na kijia

Njia isiyo na ngazi inayoelekea kwenye mlango wa mgeni

Ufafanuzi wa kipengele:

Njia za nje na za ndani kuelekea kwenye mlango wa wageni, kama vile njia za miguu, ushoroba au lifti, hazina ngazi, vizingiti au vizuio


Vigezo vya picha:

  • Piga picha nyingi kadiri inavyohitajika ili upige picha kijia chote kuanzia kwenye sehemu ya maegesho ya wageni hadi kwenye mlango wa wageni
  • Kwa fleti na hoteli, piga picha za kijia chote ikiwemo picha za mlango wa hoteli, ukumbi, ushoroba na lifti, ikiwa inafaa
  • Milango lazima iwe wazi ili kuonyesha kwamba njia haina ngazi na vizuizi

Mlango wa mgeni usio na ngazi

Ufafanuzi wa kipengele:

Mlango wa kuingia wa mgeni hauna ngazi na vizuizi na kizingiti cha mlango kina urefu wa chini ya inchi 2 (sentimita 5).

Katika hoteli au jengo la fleti, mlango wa mgeni ni mahali ambapo wageni wanaingia kwenye chumba chao. Kwa aina nyingine zote za nyumba, mlango wa mgeni ni mlango wa kuingia kwenye nyumba.


Vigezo vya picha:

  • Fungua mlango wa kuingia wa mgeni
  • Weka kamera nje ya mlango ukiangalia kwenye nyumba
  • Inamisha kamera chini ili upige picha kizingiti chote cha mlango

Kifaa cha kumwinua mtu kinachoning'inia darini au kinachosogezwa


Ufafanuzi wa kipengele:

Kuna kifaa kilichobuniwa mahususi ili kumwinua mtu na kumweka na kumtoa kwenye kiti cha magurudumu. Kimeangikwa kwenye dari au kuachwa huru.


Vigezo vya picha:

  • Kifaa cha kumwinua mtu lazima kiwe kimeundwa mahususi ili kumweka mtu na kumtoa nje ya kiti cha magurudumu

  • Onyesha kwa udhahiri kifaa cha kumwinua mtu na mahali kilipo kwenye chumba cha kulala au bafu kwenye picha yako

Kifaa cha kumwinua mtu kwenye bwawa la kuogelea au beseni la maji moto

Ufafanuzi wa kipengele:


Kuna kifaa kilichobuniwa mahususi ambacho kinaweza kumwinua mtu na kumweka au kumtoa kwenye bwawa la kuogelea au beseni la maji moto.


Vigezo vya picha:

  • Kifaa cha kumwinua mtu lazima kiwe kimeundwa mahususi ili kumweka mtu ndani na kumtoa nje ya bwawa la kuogelea au beseni la maji moto

  • Onyesha kwa udhahiri kifaa cha kumwinua mtu na mahali kilipo karibu na bwawa la kuogelea au beseni la maji moto

Kwa vyumba vilivyo katika nyumba yako

Mlango wa mgeni una upana wa angalau inchi 32 (sentimita 81)

Ufafanuzi wa kipengele:

Njia ya kuingia ya mgeni ina angalau upana wa inchi 32 (sentimita 81).


Vigezo vya picha:

  • Weka utepe wa kupimia kwenye mlango ulio wazi kati ya sehemu mbili nyembamba zaidi za kiunzi

  • Piga picha moja inayoonyesha utepe mzima wa kupimia ndani ya fremu ya mlango

  • Piga picha ya pili ya utepe wa kupimia huku vizio vya vipimo vikionekana dhahiri

Ufikiaji wa vyumba usio na ngazi


(kipengele kinapatikana kwenye vyumba vya aina zote)

Ufafanuzi wa kipengele:

Chumba hicho kiko kwenye ghorofa ya chini au kinaweza kufikiwa kwa lifti au kijia chenye mteremko na hakuna ngazi au vizingiti vinavyozidi inchi 2 (sentimita 5) kati ya mlango wa mgeni na chumba.




Vigezo vya picha:

  • Kabla ya kupiga picha, hakikisha kwamba chumba kiko kwenye ghorofa ya chini au kinaweza kufikiwa kupitia lifti au kijia chenye mteremko

  • Inamisha kamera ili upige picha kizingiti chote cha mlango

  • Hakikisha mlango umefunguliwa na uweke kamera nje ya chumba ikiangalia ndani

Mlango wa chumba una upana wa angalau inchi 32 (sentimita 81)


(kipengele kinapatikana kwenye vyumba vya aina zote)

Ufafanuzi wa kipengele:

Njia au mlango wa kuingia kwenye chumba ina angalau upana wa inchi 32 (sentimita 81).


Vigezo vya picha:

  • Jumuisha utepe wa kupimia au rula iliyowekwa upande wa ndani wa kiunzi cha mlango huku pande zote mbili zikiwa zinaonekana na nambari zikionyeshwa wazi. Mlango unapaswa kufunguliwa wazi kadiri iwezekanavyo.

Bafu lisilo na ngazi

Ufafanuzi wa kipengele:


Hakuna ngazi au vizuizi vya kuingia kwenye bafu. Vizingiti au vilinzi vya maji vinapaswa kuwa chini ya kimo cha inchi 1.


Vigezo vya picha:

  • Onyesha bafu zima, ikiwemo mahali ambapo bomba la mvua linakutana na sakafu ya bafu.

Kiti cha kuogea

Ufafanuzi wa kipengele:


Kuna kitu cha kukalia, kama vile kiti au benchi, kwenye bafu ambacho kimefungwa kwenye ukuta au kiko huru. Kiti hicho lazima kiwe kimeundwa mahususi kwa ajili ya wageni wenye matatizo ya kutembea.


Vigezo vya picha:

  • Onyesha kiti kizima ndani ya bafu.

Chuma cha kujishikilia kilichofungwa kwa ajili ya bafu

Ufafanuzi wa kipengele:


Bafu lina angalau chuma kimoja cha kujishikilia ambacho kimetiwa makomeo au kimefungwa kwa uthabiti kwenye ukuta na kinaweza kubeba uzito. Hakipaswi kuwa uchaga wa taulo na hakipaswi kushikiliwa na vidude vya kufyonza hewa au kuwa cha muda.


Vigezo vya picha:

  • Onyesha bafu zima na utoe mwonekano dhahiri wa chuma cha kujishikilia na mahali kilipo kwenye bafu.

Vyuma vya kujishikilia kwa ajili ya choo

Ufafanuzi wa kipengele:


Eneo linalozunguka choo lina angalau chuma kimoja cha kujishikilia kilichotiwa makomeo au vinginevyo kufungwa kwa uthabiti kwenye ukuta na kinaweza kubeba uzito. Hakipaswi kuwa uchaga wa taulo na hakipaswi kushikiliwa na vidude vya kufyonza hewa au kuwa cha muda.


Vigezo vya picha:

  • Toa mwonekano dhahiri wa chuma cha kujishikilia na mahali kilipo karibu na choo.

Je, makala hii ilikusaidia?

Makala yanayohusiana

  • Mwenyeji

    Hariri kichwa cha tangazo lako

    Unaweza kubadilisha jina la tangazo lako wakati wowote ukipenda, kwa hivyo jisikie huru kulipatia jina linaloangazia kile kinachofanya eneo …
  • Mwenyeji

    Jinsi vitongoji huamuliwa

    Tangazo huwekwa moja kwa moja kwenye kitongoji kulingana na anwani yake na kitongoji hiki hakiwezi kuhaririwa.
  • Mwenyeji

    Weka vistawishi kwenye tangazo

    Wageni wanaweza kuchuja matokeo ya utafutaji wa matangazo kwa kufuatia vistawishi, kwa hivyo ni muhimu ujumuishe kila kitu unachotoa.
Pata msaada kuhusu nafasi ulizoweka, akaunti na kadhalika.
Ingia au ujisajili