Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Jinsi ya kufanya
Mwenyeji wa Tukio

Kuweka vipengele vya ufkiaji kwenye matangazo ya Tukio

Ni jambo zuri sana unapoweza kuwakaribisha watu wengi zaidi kwenye Tukio lako. Unapoweka vipengele vya ufikiaji kwenye Tangazo lako, wageni wanaweza kutumia vipengele hivi katika utafutaji wao ili kupata Matukio yanayoweza kukidhi mahitaji yao mahususi ya ufikiaji.

Jinsi inavyofanya kazi

Unaweza kuhariri Tukio lako na uonyeshe kila kipengele cha ufikiaji unachotoa kwa kuweka maelezo dhahiri kwa ajili ya wageni. Hakikisha unaangalia matakwa na miongozo ya Airbnb kwa ajili ya kutoa taarifa iliyo dhahiri, inayofaa na yenye kina cha kutosha kwa ajili ya wageni.

Hariri Tukio lako ili kujumuisha vipengele vya ufikiaji

  1. Nenda kwenye dashibodi yako ya Kukaribisha Wageni, pata Tukio unalotaka kusasisha, kisha ubofye Hariri
  2. Chini ya Mahitaji ya mgeni, pata sehemu ya "Je, tukio lako lina vipengele vyovyote vya ufikiaji?"
  3. Chagua kipengele cha vipengele vya ufikiaji ambavyo vipo kwenye Tukio lako
  4. Kisha, chagua Vipengele mahususi vya ufikiaji na uweke maelezo kwenye kila kipengele ulichochagua
  5. Bofya Hifadhi

Vipengele na maelezo yako yataonyeshwa kwenye sehemu ya Vipengele vya ufikiaji ya tangazo lako na wageni watarajiwa wanaweza kutumia vipengele hivi katika utafutaji.

Ni muhimu sana uweke maelezo ya kina kwenye kila kipengele ulichochagua. Ikiwa maelezo yako si bayana vya kutosha na si ya kina au ikiwa si sahihi, kipengele husika kinaweza kukataliwa au kuondolewa kwenye tangazo lako. Rejelea matakwa na miongozo ya Airbnb kwa ajili ya kuweka maelezo ya vipengele vya ufikiaji, vilivyotengenezwa na wataalamu.

Pata maelezo zaidi kuhusu kujisikia nyumbani na kujumuishwa kwenye Airbnb kwa kusoma sera yetu ya ufikiaji.

Je, makala hii ilikusaidia?

Makala yanayohusiana

  • Jinsi ya kufanya
    Mwenyeji

    Kukaribisha wageni wenye mahitaji ya ufikiaji

    Tathmini orodha yetu ya vipengele vya ufikiaji ambavyo unaweza kuweka kwenye tangazo lako. Fikiria kufanya mabadiliko ili kukidhi mahitaji y…
  • Sera ya jumuiya
    Mgeni

    Sera ya Ufikiaji

    Jumuiya yetu imejengwa juu ya kanuni za ujumuishaji, kujisikia nyumbani na heshima, ambayo inajumuisha kukaribisha na kusaidia watu wenye ul…
  • Jinsi ya kufanya
    Mwenyeji wa Tukio

    Kuchagua picha nzuri kwa ajili ya ukurasa wa Tukio lako

    Utahitaji angalau picha 6 nzuri, zenye ubora wa hali ya juu ambazo zinaonyesha mambo muhimu ya tukio lako. Picha hizi zinapaswa kusimulia ha…
Pata msaada kuhusu nafasi ulizoweka, akaunti na kadhalika.
Ingia au ujisajili