Je, Airbnb huwatoza wageni kiasi gani?
Ada za huduma husaidia Airbnb kuwasaidia wenyeji na kulipia gharama za vitu kama vile uchakataji wa malipo, uuzaji na huduma kwa wateja.
Ni asilimia ya bei yako ya kila usiku pamoja na ada zozote ulizoweka, kama vile ada ya usafi. Ada za huduma zinakatwa kwenye bei yako ili kukokotoa malipo unayotumiwa. Kuna aina 2 za miundo ya ada kwenye Airbnb: ada ya kugawanya na ada moja.
Ada ya kugawanya
Wenyeji na wageni kila mmoja hulipa ada zake mwenyewe za huduma. Ada ya mwenyeji ya asilimia 3 inakatwa kwenye bei yako ili kukokotoa malipo unayotumiwa.* Aidha, wageni hulipa ada ya huduma ya asilimia 14.1 hadi 16.5 pamoja na bei yako. Hii inamaanisha unaweka bei moja lakini wageni wanaona na kulipa nyingine. Kwa mfano, ikiwa uliweka bei yako kuwa USD 100, unajipatia USD 97 na wageni wako wanalipa takribani USD 115.
Ada moja
Ada moja ya huduma inakatwa kwenye bei yako ili kukokotoa malipo unayotumiwa. Kwa kawaida ni asilimia 14 hadi 16.** Hii inamaanisha unaweka bei ambayo wageni wanaiona na kulipa. Kwa mfano, kwa ada moja ya asilimia 15.5, ikiwa uliweka bei yako kuwa USD 115, unajipatia USD 97.18 na wageni wako wanalipa USD 115.
Ada moja inahitajika kwa matangazo ya ukarimu ya kawaida, ikiwemo matangazo mengi ya hoteli na fleti zilizowekewa huduma. Wenyeji wengi ambao hutumia programu ya usimamizi wa nyumba au usimamizi wa chaneli pia wako kwenye ada moja.
Kwa nini Airbnb inatoza ada za huduma?
Ada za huduma husaidia Airbnb iendeshe huduma zake vizuri na kuwasaidia wenyeji. Zinalipia gharama za vitu kama vile:
- Kuchakata malipo ya wageni
- Uuzaji wa matangazo kwa wageni
- Usaidizi kwa wateja wa saa 24
Ninapata wapi ada ya huduma?
Fungua nafasi yoyote iliyowekwa kwenye kalenda yako au muamala wowote katika dashibodi yako ya mapato, ili uone mchanganuo wa bei. Utapata ada ya huduma kwenye mstari wake.
Pata maelezo zaidi kuhusu ada za huduma kwenye Kituo cha Msaada, ambacho kina makala kuhusu:
*Baadhi hulipa zaidi, ikiwemo baadhi ya wenyeji wenye matangazo nchini Italia na Brazili.
**Wenyeji walio na sera kali sana za kughairi wanaweza kulipa ada ya juu zaidi.
Katika baadhi ya nchi na maeneo, kodi hujumuishwa kwenye jumla ya bei iliyoonyeshwa. Jumla ya bei ikiwemo kodi huonyeshwa siku zote kabla ya kulipa.
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.