Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

Andika mwongozo wa nyumba ili ushiriki taarifa kuhusu sehemu yako

Okoa wakati na utoe maelezo muhimu ukitumia maelekezo yaliyoandikwa hapo awali.
Na Airbnb tarehe 18 Nov 2020
Inachukua dakika 4 kusoma
Imesasishwa tarehe 17 Nov 2021

Vidokezi

  • Unda mwongozo wa nyumba

  • Liwe fupi na rahisi kueleweka

  • Jumuisha nenosiri la Wi-Fi kwanza

  • Gundua zaidi kwenye mwongozo wetu kamili ili kuweka tangazo lanye mafanikio

"Je, ninaunganisha vipi Wi-Fi? Themsotati ipo wapi? Je, rimoti ipi inafanya kazi gani? " Haya ni maswali machache ambayo wageni wanaweza kuwa nayo wanapokaa kwenye sehemu yako. Unaweza kuwasaidia wapate majibu na kusaidia kuhakikisha vyombo vyako vya nyumbani na vipengele vingine vinatumiwa kwa usahihi, kwa kutumia zana ya mwongozo wa nyumba ya Airbnb.

Zana ya mwongozo wa nyumba hukuwezesha kuwapatia wageni maelekezo ya wazi ya hatua kwa hatua na huwaelezea wapi wanapoweza kupata vitu muhimu, kama vile vifaa vya usalama au rauta kwa ajili ya Wi-Fi. Unda mwongozo wako mara moja, na hautalazimika kuandika tena au kutuma tena barua pepe kwa kila nafasi inayowekwa, muda mwingi umeokolewa. Na kwa kuwa wageni wanaweza kuupata kwenye programu, wanaweza kuuangalia muda wowote, mahali popote. Mwenyeji Neil kutoka Mountain View, California, anapenda namna ambavyo kipengele hicho humsaidia kuepuka "jumbe za usiku wa manane, simu za hasira, na jambo baya kabisa: tathmini mbaya."

Tumia vizuri zaidi zana ya mwongozo wa nyumba kwa kutumia vidokezi hivi vilivyopimwa na kujaribiwa kutoka kwa Wenyeji kama wewe.

Anza na nenosiri la Wi-Fi

Ni moja kati ya vitu ambavyo wageni wanauliza wanapowasili, kwa hiyo wenyeji wengi wanaweka maelekezo haya kuwa ya kwanza kabisa kwenye mwongozo wao wa nyumba. "Wote wanataka msimbo wa Wi-Fi, kwa hivyo huo ndio ujanja wangu wa kuwafanya wafungue mwongozo wa nyumba na pengine wausome," anasema Marit Anne kutoka Troms, Norway.

Kufikia nenosiri la Wi-Fi kwa urahisi ni muhimu hasa kwa watu wanaofanya kazi mbali na ofisi ambao huenda watahitaji kishiriki kwenye mkutano kwa njia ya video, kumaliza kuandika ripoti mara tu watakapowasili kwenye sehemu yako.

Jumuisha taarifa ya maegesho

Sheria na alama za maegesho barabarani zinaweza kutatanisha, hasa ikiwa wageni wanazungumza lugha nyingine. Ni wazo zuri kutoa maelekezo ya wazi, kama wanavyofanya Wenyeji Ben na Angel kutoka Wellington, New Zealand: "Unakaribishwa kuegesha mbele ya uzio mweupe wa vigingi upande wa kulia wa barabara, karibu na ua wa miti iliyooteshwa."

Angazia sehemu zinazowafaa wanyama vipenzi na familia

Ikiwa unakaribisha wanyama vipenzi au watoto kwenye sehemu yako, huenda ikafaa kutaja vipengele vyote ulivyojumuisha ili kuwashughulikia, hasa kwa kuwa unaweza kushiriki mwongozo wa nyumba yako na wageni kabla hawajafika ili waweze kupanga mapema. Unaweza kutumia mwongozo wako:

  • Elezea mahali ambapo panapatikana mabakuli ya chakula na maji kwa ajili ya wanyama vipenzi
  • Bainisha mataulo yapi ni kwa ajili ya miguu michafu na kufutia miguu ya wanyama vipenzi
  • Taja vistawishi vyovyote kwa ajili ya watoto, kama vile kitanda cha watoto na kiti cha juu
  • Orodhesha vyumba ambavyo vina ving'ora vya moshi na kaboni monoksidi

Waeleze wageni mahali wanapoweza kupata vistawishi (na jinsi ya kuvitumia)

Baada ya safari ndefu, inaweza kuwa vigumu kupata na kutumia baadhi ya vifaa muhimu vya nyumbani. Wenyeji Joh na Gian kutoka San Francisco wanatoa mifano hii:

  • "Kipasha Joto: Utakuta thermostati ukutani, karibu na runinga. Tafadhali kumbuka kuizima unapoondoka.
  • Choo: Tafadhali, hakuna kitu chochote kitakachoingia chooni isipokuwa tu karatasi za chooni. Kuna chombo kidogo cha taka kwa ajili ya kila kitu.
  • Vifaa vya jikoni: Vyombo na vikombe vipo upande wa juu wa kabati katika upande mmoja wapo wa mikrowevu. Vyombo vya fedha viko kwenye droo upande wa kushoto wa oveni, na masufuria yapo kwenye kabati. Jisikie huru kutumia mojawapo ya vitu hivi kadiri utakavyohitaji kuandaa chakula chako kitamu. Utakapomaliza, utakuweka vyombo vichafu kwenye mashine ya kuoshea vyombo. Vyombo vitakapokuwa vimejaa, tutawasha mashine.”

Wenyeji ambao hawaishi kwenye nyumba hiyo au karibu na nyumba hiyo pia wanapendekeza kujumuisha maelekezo kuhusu taka, maji, na maelezo mengine ambayo ni ya kipekee katika eneo hilo:

  • "Taka: Weka taka zako kwenye chombo cha kuweka taka kilichopo kwenye sehemu ya nyumba chini ya ardhi. Tafadhali usiweke taka nje au kwenye baraza, mahali ambapo ndege, nguchiro, na viumbe wengine wanaweza kuingia.” -Kim, Upson, Wisconsin
  • "Maji na Umeme: Tafadhali kuwa mwangalifu kuhusu kiwango cha maji na umeme unachotumia. Maji ya moto yanapatikana kwa kiwango kidogo.” -Fred, Placencia, Belize

Maliza na maelekezo ya hatua kwa hatua kwa ajili ya vyombo vya ndani na elekroniki

Maelekezo ya kina ni muhimu, wanasema wenyeji Joh na Gian. Hivi ndivyo wanavyoelezea kwa kutumia huduma zao za kutazama video mtandaoni:

"Jinsi ya kujiunga kwenye Netflix, Prime Video na huduma nyingine za kutazama video mtandaoni:

  1. Washa runinga iliyomo chumbani, kisha subiri kidogo. Wakati huu, utaona tu theluji.
  2. Baada ya dakika moja, bonyeza kitufe chenye rangi nyingi, chenye umbo la almasi.
  3. Chagua programu unayotaka kuiunganisha, kisha bonyeza kitufe kikuu. Kwa Netflix, tunakualika utumie akaunti ya Mgeni tuliyounda kwa ajili yako."

Lifanye liwe fupi na rahisi kutumia

Wenyeji wengi wanasisitiza umuhimu wa kufanya mwongozo wa nyumba yako kuwa mfupi na kuelezea mambo muhimu tu. "Hupaswi kuwafanya wageni wahisi kana kwamba ni lazima watembee kwenye uwanja wa mabomu ili kumfanya mwenyeji afurahi," anasema mwenyeji Tina kutoka Nanaimo, Canada. "Pata uwiano sahihi kati ya mahitaji yako na kuwafanya wageni wako wahisi kukaribishwa nyumbani kwako."

Mara baada ya kuandika mwongozo wako wa nyumba, unaweza kufikiria kuweka karatasi iliyobandikwa kwenye karatasi ngumu mahali fulani kwenye nyumba yako, ikiwa na maelekezo ya wazi kuhusu jinsi ya kuingia kwenye Wi-Fi. Ni njia moja wapo tu ya kufanya taarifa iwafikie wageni kwa urahisi. Na kusaidia kuhamasisha tathmini nzuri, kila wakati.

Pata maelezo ya jinsi ya kuweka mwongozo wa nyumba

Taarifa zilizo ndani ya makala hii zinaweza kuwa zimebadilika toka zilipochapishwa.

Vidokezi

  • Unda mwongozo wa nyumba

  • Liwe fupi na rahisi kueleweka

  • Jumuisha nenosiri la Wi-Fi kwanza

  • Gundua zaidi kwenye mwongozo wetu kamili ili kuweka tangazo lanye mafanikio
Airbnb
18 Nov 2020
Ilikuwa na manufaa?