Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa
  Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

  Unda kitabu cha mwongozo ili ushiriki vidokezi vyako vya eneo husika

  Wasaidie wageni wafahamu eneo lako ukitumia mwongozo mahususi wa usafiri wa kidijitali.
  Na Airbnb tarehe 29 Okt 2019
  Inachukua dakika 2 kusoma
  Imesasishwa tarehe 6 Des 2021

  Vidokezi

  • Unda kitabu cha mwongozo cha kidijitali ili kushiriki mapendekezo binafsi ya eneo lako
  • Unaweza kuwatumia wageni kitabu chako cha mwongozo baada ya kuweka nafasi ili waweze kuweka mipango mapema

  • Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu kamili ili kuweka tangazo lenye mafanikio

  Wenyeji wengi huwapa wageni wao mapendekezo ya eneo lao, kama vile mahali pa kwenda kunywa kahawa au kufurahia chakula cha jioni kisichosahaulika. Badala ya kuandika vidokezi kwa ajili ya kila mgeni, kuunda kitabu cha mwongozo cha kidijitali kwenye Airbnb kunaweza kukusaidia kuokoa muda kwa kuyaweka mapendekezo yako katika mahali pamoja.

  Wageni wanaweza kufikia kitabu chako cha mwongozo kwenye kichupo chao cha Safari na kutoka kwenye tangazo lako au unaweza kuwatumia moja kwa moja katika ujumbe ukitumia Nyenzo yetu ya Shiriki Mapendekezo. Hivi ndivyo unavyoweza kutumia vyema kitabu chako cha mwongozo ili uweze kuonyesha mazingira ya eneo lako na kuwapa wageni uzoefu halisi na wa kipekee.

  Kitabu cha mwongozo ni nini?

  Kitabu cha mwongozo ni fursa yako ya kuwapa wageni taarifa iliyopangiliwa ambayo inaangazia ukarimu wako na vitu vinavyotoka kwenye jumuiya yako. Unaweza kuunda kitabu mahususi cha mwongozo kwenye Airbnb ili wageni wakifikie kwa urahisi.

  Wewe ndiwe unayeamua mapendekezo unayotoa, kwa hivyo fikiria kuhusu mapendekezo ambayo ungeyataka kama msafiri. Mara nyingi wageni wanafurahia mapendekezo ya mikahawa, kutembelea maeneo yenye vivutio, maduka ya kipekee na matukio ya kuvutia ya maeneo ya nje.

  Vidokezi 5 kwa ajili ya kuunda kitabu kizuri cha mwongozo

  1. Kifupishe. Fanya iwe rahisi kwa wageni kupitia mapendekezo yako kwa haraka kwa kufupisha kila pendekezo. Wasaidie wageni waelewe eneo au tukio hilo ni nini na kwa nini wanapaswa kulijaribu.
  2. Kifanye kiwe binafsi. Mapendekezo yenye uzito hutokana na maarifa binafsi na yale uliyopitia. Ni vyema kupendekeza tu maeneo ambayo wewe mwenyewe umefurahia.
  3.
  Taja vipengele maalumu. Hakikisha kwamba umejumuisha vipengele vyovyote vya kipekee au maarufu, kama vile baraza nzuri ya nje ya mkahawa au sehemu maalumu ya duka yenye bidhaa zinazotoka katika eneo lako.
  4.Jumuisha picha. Ili kufanya kitabu chako cha mwongozo kivutie zaidi, unaweza kupakia picha ambayo umepiga pale inapowezekana ya kila eneo unalopendekeza.
  5. Hakikisha kimesasishwa. Hakikisha kwamba unatathmini kitabu chako cha mwongozo mara kwa mara ili kuhakikisha kwamba taarifa zote bado ni sahihi na uweke mapendekezo mapya.

   Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuunda kitabu mahususi cha mwongozo

   Je, una matangazo zaidi ya moja?

   Vitabu vya mwongozo huunganishwa na akaunti yako ya Mwenyeji, si tangazo binafsi (jambo ambalo huwasaidia Wenyeji wenye vyumba au nyumba nyingi za kupangisha). "Sasa ninaweza kuunda kitabu kimoja cha mwongozo kwa ajili ya eneo langu ambacho kitafaa matangazo yangu yote matatu," anasema Ann, Mwenyeji Bingwa huko Sedgwick, Maine.

   Namna ambavyo wageni wanapata kitabu chako cha mwongozo

   Wageni wanaweza kufikia kitabu chako cha mwongozo kutoka kwenye kurasa za tangazo na wasifu wako na vilevile kwa kwenda kwenye Kichupo chao cha Safari, ambapo kitaonekana kiotomatiki wakati nafasi iliyowekwa itakapothibitishwa.

   Unaweza pia kutaka kushiriki kitabu chako cha mwongozo unapowasiliana na wageni kupitia ujumbe. Unaweza kufanya hivyo kwa urahisi kwa kubofya ikoni ya Shiriki Mapendekezo kwenye kikasha chako cha Mwenyeji. Nyenzo hii pia hukuruhusu kupendekeza mchanganyiko uliopangiliwa wa Matukio ya Airbnb ya eneo lako.

   Tunajua kwamba unajitahidi ili kuunda sehemu za kukaa za kukumbukwa—na tunatumaini kwamba kitabu cha mwongozo cha kidijitali kitakusaidia kuwaunganisha wageni na shughuli nzuri za eneo lako.

   Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

   Vidokezi

   • Unda kitabu cha mwongozo cha kidijitali ili kushiriki mapendekezo binafsi ya eneo lako
   • Unaweza kuwatumia wageni kitabu chako cha mwongozo baada ya kuweka nafasi ili waweze kuweka mipango mapema

   • Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu kamili ili kuweka tangazo lenye mafanikio

   Airbnb
   29 Okt 2019
   Ilikuwa na manufaa?