Jinsi ya kuboresha utaratibu wako wa kukaribisha wageni

Pata vidokezi kuhusu kufanya usafi, kuingia na mawasiliano.
Na Airbnb tarehe 4 Mei 2021
Inachukua dakika 2 kusoma
Imesasishwa tarehe 1 Mei 2024

Huduma ya kukaribisha wageni inachukua muda, lakini mara baada ya kuizoea, unaweza kuboresha sehemu nyingi za ratiba yako. Kwa njia hiyo, unazingatia kuunda uzoefu wa kukumbukwa kwa ajili ya wageni wako.

Pangilia vizuri ratiba yako ya kufanya usafi

Kuweka utaratibu wa kufanya usafi husaidia kufanya kazi za wageni ziwe rahisi.

  • Zingatia kuajiri mfanya usafi mtaalamu ili kusaidia kudumisha uthabiti.
  • Chagua matandiko na taulo zenye rangi zinazofanana, ili uweze kuzifua zote mara moja.
  • Weka seti ya ziada ya matandiko na mataulo kwa ajili ya wageni wengine watakaoingia mapema.
  • Panga usafi wa kina mara kwa mara ili kufanya usafi liwe jambo rahisi baada ya mgeni kuondoka na kabla ya mwingine kuingia
  • Ratibu mpangilio wa kujirudiarudia wa bidhaa zako za usafi na vitu vingine muhimu, kama vile karatasi ya choo na sabuni. Hii inaweza kuokoa muda na kukusaidia kuepuka kukosa vifaa.
  • Nunua kwa wingi ili uweke bidhaa ambazo wewe na wageni mnazitumia zaidi, kama vile shampuu na kondishena. 

Kuwasiliana kwa njia iliyo dhahiri na yenye ufanisi

Kujibu ujumbe wa wageni si lazima liwe jambo la kutumia muda mwingi. Kutumia zana za Airbnb kunaweza kuanzisha mawasiliano yenye ufanisi zaidi na wageni.

  • Pakua programu ya Airbnb ili ujibu haraka. Jisajili kwenye kipengele cha arifa kwa simu na uwashe sauti kwenye kifaa chako.
  • Tumia ujumbe ulioratibiwa ili kushiriki maelezo fulani wakati wageni wana uwezekano wa kuyataka, kama vile kuthibitisha kwamba wageni walipokea maelekezo ya kuingia siku moja kabla ya ukaaji wao.
  • Weka majibu ya haraka kujibu maswali ya kawaida haraka kwa kuandika majibu mapema. Kichupo cha Ujumbe kinapendekeza kiotomatiki ni lipi kati ya majibu yako ya haraka linaweza kutumika vizuri kwenye mazungumzo.

Kuunda mchakato wa kuingia bila usumbufu

Kurahisisha kuingia kunaweza kuwasaidia wageni wako wajisikie kukaribishwa. Fikiria kumweka Mwenyeji Mwenza ili kusaidia kusimamia tangazo lako na uwekaji nafasi.

  • Tumia mwongozo wa Kuwasili katika kichupo cha Matangazo yako ili kuweka maelezo muhimu, ikiwemo njia yako ya kuingia na muda, maelekezo, mwongozo wa nyumba na nenosiri la Wi-Fi.
  • Weka chaguo la kuingia mwenyewe,kwa kutumia vicharazio, makufuli janja au visanduku vya funguo ili kuokoa muda na kuwapa wageni urahisi zaidi wa kufanya mambo.
  • Toa mwongozo wa nyumba kushiriki maelekezo, kama vile jinsi ya kutumia vistawishi au kufikia Wi-Fi.

Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Airbnb
4 Mei 2021
Ilikuwa na manufaa?