Vidokezi vya kuepuka ughairi unaoweza kuzuilika

Sasisha kalenda yako mara kwa mara, weka bei inayokufaa na kadhalika.
Na Airbnb tarehe 4 Mei 2021
Inachukua dakika 2 kusoma
Imesasishwa tarehe 16 Feb 2023

Vidokezi

  • Pata vidokezi vya kusimamia na kusasisha kalenda yako

  • Weka bei na bei ya kila usiku inayokufaa

  • Wafahamu wageni wako

Mara baada ya mgeni kuweka nafasi ya safari, kile anachofikiria ni kuota jua ufukweni au kutalii jiji jipya, kwa hivyo kughairi kunaweza kuwa jambo la kutamausha. Kughairi kunaondoa kuaminiana kati ya Wenyeji na wageni na kunaweza kusababisha utozaji wa ada na adhabu.

Wenyeji hufanya kazi nzuri sana ya kuheshimu nafasi zilizowekwa na kufanya zaidi ya walivyotarajiwa ili kuwasaidia wageni kila siku. Hivi ni baadhi ya vidokezi vinavyoweza kukusaidia kuepuka ughairi wowote unaoweza kuzuiwa.

Kuhakikisha kwamba kalenda yako imesasishwa

Omar, Mwenyeji Bingwa huko Mexico City, anapendekeza ufuate mielekeo ya usafiri na upange mapema. “Elewa msimu wa usafiri katika eneo lako, msimu wa idadi ya juu ya wasafiri, wasafiri wengi na wasafiri wachache, ili uweze kupanga upatikanaji wa kalenda yako mapema kwa ajili ya ukaaji wa muda mfupi, muda wa wastani au muda mrefu,” anasema.

  • Zuia tarehe mahususi pale unapojua kwamba hutaweza kukaribisha wageni.
  • Bainisha kiasi cha ilani ya mapema unachohitaji kutoka kwa wageni.
  • Panga kalenda yako kwa hadi miaka miwili mapema.
  • Angalia kalenda yako mara kwa mara kisha urekebishe kadiri inavyohitajika.
Elewa msimu wa usafiri katika eneo lako ili uweze kupangia mapema upatikanaji wa kalenda yako.
Superhost Omar

Kuchagua mipangilio sahihi ya kalenda na kuweka nafasi

Kuweka Nafasi Papo Hapo ni njia nzuri ya kuokoa muda na jitihada, maadamu kalenda na mipangilio yako inasasishwa mara kwa mara.

Unaweza kufanya mipangilio yako ya kuweka nafasi ikufae kwa kuweka kiwango cha chini na kiwango cha juu chamuda wa kukaa, kiasi gani cha ilani ya mapema unachopendelea na muda unaohitaji ili kujiandaa kwa ajili ya wageni.

Kuweka bei inayokufaa

Kuunda mkakati wa kupanga bei kunahusu kupata kiwango bora ambapo unawavutia wageni na kufurahia kile unachojipatia.

  • Weka bei mahususi kwa ajili ya usiku, wiki au miezi mahususi.
  • Fanya utafiti wa bei ya kila usiku kwa ajili ya matangazo kama hilo katika eneo lako.
  • Ili kuondoa makisio, washa kipengele cha Upangaji Bei Kiotomatiki.

Kuwajua wageni watarajiwa

Mawasiliano yanayoendelea pamoja na wageni ni muhimu na nyenzo zetu za kutuma ujumbe hufanya iwe rahisi kudumisha mawasiliano.

  • Ikiwa ungependa kupata maelezo zaidi kuhusu mgeni mtarajiwa, soma tathmini zake.
  • Unaweza kutuma majibu yale yale ya haraka kwa wageni wote watarajiwa ili kuwasiliana na kupata taarifa zaidi.
  • Wezesha ujumuishaji kwa kuwauliza wageni wako, Je, unahitaji nini ili kuhisi umestareheka na umekaribishwa katika sehemu yangu? 
  • Toa idhini za awali na himizo kwa wageni ambao wanawasiliana nawe kabla ya kuweka nafasi. Tumegundua kwamba wakati mwingine wageni huwasiliana na Wenyeji kabla ya kuweka nafasi ili kupima ikiwa watakubaliwa na kukaribishwa.

Zaidi ya yote, kumbuka sera yetu ya kutobagua. Kwa kukaribisha wageni kwenye Airbnb, unakubali kuwatendea wageni wote kwa ujumuishaji na kwa heshima.

Pata taarifa zaidi kuhusu ughairi wa Mwenyeji

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Vidokezi

  • Pata vidokezi vya kusimamia na kusasisha kalenda yako

  • Weka bei na bei ya kila usiku inayokufaa

  • Wafahamu wageni wako

Airbnb
4 Mei 2021
Ilikuwa na manufaa?