Jinsi ya kushughulikia tathmini mbaya

Shughulikia maoni mabaya kwa maelezo thabiti kuhusu maboresho.
Na Airbnb tarehe 4 Mei 2021
Inachukua dakika 2 kusoma
Imesasishwa tarehe 13 Ago 2024

Tathmini mbaya zinaweza kusononesha, lakini hata Wenyeji waliopewa ukadiriaji wa juu wanazipata mara kwa mara. Hivi ni vidokezi vichache vya kushughulikia maoni mabaya ya wageni.

Kujibu tathmini mbaya

Kujibu tathmini husaidia kuwaonyesha wageni kwamba uko tayari kupokea mapendekezo. "Sitarajii Mwenyeji yeyote awe na tathmini zisizo na dosari kwa asilimia 100," anasema Andrew, mgeni ambaye pia ni Mwenyeji Bingwa jijini Berlin. "Ninavutiwa zaidi na wale wanaochukulia maoni ya ukosoaji kwa uzito."

Zingatia vidokezi hivi unapojibu tathmini mbaya:

  • Toa jibu kwa umma. Jibu fupi, la kirafiki linaweza kusaidia kuwahakikishia wageni wengine kwamba unajali yale wanayopitia.
  • Washukuru wageni kwa maoni yao. Hii inaweza kuwa rahisi kama: “Asante kwa tathmini yako! Tunakushukuru sana kwa kutenga muda ili kutafakari kuhusu safari yako.”
  • Eleza jinsi unavyoboresha sehemu yako. Unaweza kuandika: "Tunasikitika kwamba vitanda havikukuridhisha. Usingizi wako ni muhimu, kwa hivyo tumeongeza vifuniko vya godoro."

Unaweza siku zote kuripoti tathmini ambayo inakiuka Sera yetu ya Tathmini, kama vile tathmini ya kulipiza kisasi. Inaweza kuondolewa ikiwa wageni watabainika kuwa wamefanya ukiukaji mkubwa wa sera.

Kuboresha huduma kadiri unavyoendelea

Matatizo ya usahihi na usafi ni sababu mbili za kawaida ambazo wageni huwapa Wenyeji ukadiriaji wa chini ya nyota tano. Tumia maoni ya wageni kama fursa ya kuboresha huduma yako ya kukaribisha wageni.

Hizi ni njia chache za kuwaonyesha wageni kwamba sikuzote uko tayari kuboresha huduma yako:

  • Chukulia maoni kama fursa. Wageni hutoa mitazamo ambayo huenda usingeizingatia, kama vile kwamba unaweza kurahisisha mchakato wa kuingia au kuongeza taulo zaidi.
  • Kuwa wazi. Sasisha picha zako na maelezo ya tangazo ili kuonyesha kile unachotoa kwa sasa. Eleza jinsi unavyoshughulikia matatizo yanayoweza kutokea, kama vile kutoa vizibo vya masikio ikiwa mtaa wako una kelele.

  • Toa huduma jumuishi ya kukaribisha wageni. Zingatia kumfanya kila mgeni ahisi amekaribishwa kwa kutumia lugha isiyoegemea jinsia yoyote na kuangazia vipengele vinavyofikika.
  • Wasiliana na wageni wakati wote wa ukaaji wao. Tumia ujumbe ulioratibiwa kuuliza jinsi mambo yanavyoendelea na ushughulikie matatizo yoyote mara moja.

Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Airbnb
4 Mei 2021
Ilikuwa na manufaa?