Kwa nini ni muhimu sana kujibu wageni haraka

Kutumia zana za Airbnb kunaweza kukusaidia kujibu kwa urahisi.
Na Airbnb tarehe 4 Mei 2021
Inachukua dakika 2 kusoma
Imesasishwa tarehe 9 Mac 2023

Wenyeji waliofanikiwa zaidi hujibu ujumbe wa wageni mara tu wanapoupokea. Kwa kweli, kuwa na kiwango kizuri cha kutoa majibu kunaweza kusaidia tangazo lako lionekane kwenye orodha ya juu katika utafutaji wa wageni.

Jibu la haraka ni muhimu hasa kabla ya kuweka nafasi, wakati wageni wanaweza kuhitaji taarifa zaidi ili kuweka nafasi, na wakati wa kuingia na kutoka, wakati wageni wanaweza kuhitaji jibu la haraka kwa maswali. Tuliwaomba Wenyeji wanaodumisha kiwango cha kutoa majibu kwa haraka watoe vidokezi vichache.

Kuwa mwenye kutoa majibu zaidi

“Hakikisha kwamba programu yako ya Airbnb, SMS na arifa za barua pepe zinatumika kila wakati, ili zionekane kwenye simu yako ya mkononi ujumbe mpya unapoingia,” anasema Omar, Mwenyeji Bingwa wa Mexico City.

Kuanzia hapo, jaribu zana za Airbnb ili kufanya majibu yako yawe ya kiotomatiki. Kath, Mwenyeji huko Albany, Australia, anapenda kutumia majibu ya haraka. "Yanaokoa muda mwingi na hunisaidia nisiandike kitu kilekile tena na tena," anasema.

Ujumbe ulioratibiwa pia unapatikana kwa urahisi, hasa wakati wa kuingia na kutoka. Keshav, mwanabodi wa Bodi ya Ushauri ya Wenyeji huko New Delhi, India, anatuma ujumbe ulioratibiwa saa 24 kabla ya kila mgeni kuingia ambao unajumuisha maelekezo ya kufikia eneo lake na taarifa nyingine ya kuwasili.

"Ikiwa sioni mgeni wakati wa kuingia ukifika, ninamtumia ujumbe mwingine wa kuuliza, ‘Habari, una taarifa zote? Hapa tena, ikiwa unajaribu kutafuta mahali,"Keshav anasema.

Jinsi kiwango cha kutoa majibu kinavyohesabiwa

Kiwango chako cha kutoa majibu ni asilimia ya ujumbe mpya kutoka kwa wageni ambao umejibu ndani ya saa 24 katika siku 30 zilizopita.

  • Hii ni pamoja na kujibu maulizo mapya kutoka kwa mgeni na kukubali, kutoa idhini ya awali, au kukataa ombi la kuweka nafasi.

  • Kuchukua zaidi ya saa 24 kujibu kutapunguza kiwango chako cha jumla cha majibu na kuongeza muda wako wa wastani wa majibu.

Sehemu muhimu ya kukaribisha wageni ni kuendelea kuitumia akaunti yako ya Airbnb na kujibu ujumbe haraka. Kufanya hivyo huboresha kiwango chako cha kutoa majibu na kulisaidia tangazo lako lionekane kwenye orodha ya juu katika matokeo ya utafutaji.

Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.
Airbnb
4 Mei 2021
Ilikuwa na manufaa?