Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Sera ya Tathmini ya Airbnb

  Ili kujenga tovuti ya uaminifu, tunaiomba jumuiya yetu isaidie kuhakikisha kwamba tathmini kwenye Airbnb ni muhimu, zinaarifu na haziiweki jumuiya yetu katika hatari ya kudhuriwa. Kwa hivyo, tunatarajia tathmini zote zizingatie mambo yafuatayo:

  1. Tathmini hazipaswi kukiuka sera yetu ya maudhui

  Baadhi ya maudhui hayaruhusiwi kamwe kwenye Airbnb. Unaweza kutathmini Sera ya Maudhui ya Airbnb ili kupata maelezo zaidi.

  2. Tathmini hazipaswi kuwa na ubaguzi

  Tathmini zinasaidia zaidi zinapotoa taarifa isiyo ya kibaguzi na ya kweli. Kwa hivyo, hatuwaruhusu watu binafsi au taasisi ambazo zinamiliki au zinazoshirikiana na tangazo au tathmini kuchapisha tathmini za biashara zao. Pia hatuwaruhusu watu ambao wamethibitishwa kutoa matangazo shindani au matukio kuchapisha tathmini za washindani wao wa moja kwa moja.

  Huruhusiwi kuhamasisha tathmini nzuri, kutumia tishio la tathmini mbaya ili kuongoza matokeo unayotaka, au kushawishi tathmini ya mtu mwingine kwa ahadi ya malipo.

  Huruhusiwi pia kukubali nafasi bandia zilizowekwa kwa kubadilishana na tathmini nzuri, kutumia akaunti ya pili ili kujiandikia tathmini, au kupanga na washirika wa biashara ili wakupatie tathmini nzuri.

  Aidha, tathmini zinaweza kuondolewa kwenye tovuti kwa ajili ya sehemu za kukaa ambapo ukiukaji mkubwa wa Sera ya Sherehe na Hafla umefanyika. Hii ni kuwasaidia wenyeji wajisikie huru zaidi kuingilia kati wakati sherehe yenye kuvuruga inafanyika, bila kuogopa kuandikiwa tathmini ya kibaguzi.

  3. Tahtmini zinapaswa zihusike na hali

  Fanya tathmini zako zihusike kwenye Airbnb na sehemu yako ya kukaa au tukio, kwani wageni wanasoma tathmini zako ili kujifunza kumhusu mwenyeji na tangazo lake. Tathmini ambazo ziko nje ya mada zinaweza kuvuruga mawazo na haziwasaidii wageni wengine kufanya maamuzi ya ufahamu ya kuweka nafasi. Kwa sababu hii, tathmini zinapaswa kuzingatia mwingiliano wako na wanajumuiya wengine na wakati wako kwenye ukaaji au tukio.

  Ili tathmini ziweze kuhusika, tunapendekeza uepuke mambo yafuatayo:

  • Maoni kuhusu mtazamo wa mtu wa kijamii, kisiasa, au kidini
  • Maneno machafu, matusi na dhana kuhusu tabia au utu wa mtu
  • Maudhui yanayotaja hali ambazo mtu hawezi kabisa kuzidhibiti
  • Maudhui kuhusu huduma ambazo hazihusiani na Airbnb (kwa mfano, shirika la ndege, huduma za teksi, mkahawa, n.k.)
  • Maoni kuhusu nafasi zilizowekwa zamani za Airbnb, wenyeji, au wageni, au kuhusu bidhaa ya Airbnb ambapo haihusiani na tangazo, mwenyeji au mgeni unayekadiria

  Tunapopokea ripoti ya tathmini ambayo inakiuka sera hii, tunaweza kuiondoa tathmini hiyo kutoka kwenye tovuti yetu. Ukiukaji unaorudiwarudiwa unaweza kusababisha kusimamishwa au kulemazwa kabisa kwa akaunti inayowajibika (zinazowajibika) na tathmini hizo.

  Kuripoti tathmini ambayo inakiuka sera yetu

  Ili kuripoti tathmini kwa kukiuka sera ya tathmini ya Airbnb, wasiliana nasi.

  Ikiwa unahisi tathmini si ya kweli

  Ingawa tunawahimiza na kuwatarajia wanajumuiya wote wachapishe tathmini zilizo na taarifa ya kweli na sahihi, Airbnb haisuluhishi mabishano kuhusu ukweli wa tathmini. Tunatarajia mwandishi wa tathmini atetee maudhui ya tathmini yake. Ikiwa unataka kujibu tathmini, fahamu jinsi ya kufanya hivyo.

  Kwa taarifa zaidi kuhusu jinsi tunavyochunguza na kupatanisha mabishano ya tathmini, soma kuhusu Upatanishi wa Airbnb wa Mabishano kwa ajili ya Tathmini.

  Ulipata msaada uliohitaji?

  Faragha Yako

  Tunatumia vidakuzi na teknolojia zinazolingana ili kusaidia ufanye maudhui yawe upendavyo, kurekebisha na kupima matangazo na kutoa uzoefu bora. Kwa kubofya SAWA au kuwasha chaguo katika Mapendeleo ya Vidakuzi, unakubaliana na jambo hili kama ilivyoainishwa kwenye Sera yetu ya Vidakuzi. Ili kubadilisha mapendeleo au kuondoa ridhaa, tafadhali sasisha Mapendeleo ya Vidakuzi yako.