Ikiwa unahitaji usaidizi wa ziada wa kukaribisha wageni kwenye eneo lako, unaweza kuweka mwanafamilia, rafiki, jirani au unaweza kupata mwenyeji mwenza wa eneo husika, mwenye ubora wa juu kwenye Mtandao wa Mwenyeji Mwenza (inapopatikana).*
Wenyeji wenza wanaweza kukusaidia kidogo au mengi- ni juu yako na mwenyeji mwenza wako. Pata maelezo zaidi kuhusu kile ambacho wenyeji wenza wanaweza kufanya, pamoja na kuangalia vidokezi vyetu vya kukaribisha wageni.
Unaweza kuchagua ruhusa kwa kila mwenyeji mwenza ili kupunguza kile anachoweza kufikia na kusimamia kwenye tangazo lako. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ruhusa za mwenyeji mwenza zinavyofanya kazi.
Unaweza kuwaalika hadi wenyeji wenza 10 kwa kila tangazo. Matumizi yako ya nyenzo za mwenyeji mwenza, ikiwemo kuongeza wenyeji wenza kwenye tangazo lako, yanadhibitiwa na Masharti ya Ziada ya Mwenyeji Mwenza.
Katika baadhi ya nchi, unaweza kufanya kazi na mwenyeji mwenza mwenye uzoefu ambaye hutoa huduma anuwai ili kuwasaidia wenyeji.* Unaweza kuendelea kudhibiti tangazo lako huku ukipata msaada unaohitaji. Tafuta mwenyeji mwenza kwenye Mtandao wa Wenyeji Wenza na uanze kujadili jinsi utakavyoshirikiana.
Je, tayari wewe ni mwenyeji wa Airbnb anayevutiwa na mwenyeji mwenza?Jiunge na Mtandao wa Wenyeji Wenza na ujipatie mapato kwa masharti yako mwenyewe kwa kuwasaidia wenyeji kutunza nyumba na wageni wao.
Mtandao wa Wenyeji Wenza unapatikana katika maeneo mahususi, kwa sasa nchini Australia, Brazili (unaendeshwa na Airbnb Plataforma Digital Ltda), Kanada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japani, Korea, Meksiko (unaendeshwa na Airbnb Global Services Limited), Uhispania, Uingereza na Marekani (unaendeshwa na Airbnb Living LLC).
*Wenyeji ndani ya Mtandao wa Wenyeji wenza kwa kawaida wana ukadiriaji wa juu, viwango vya chini vya kughairi na uzoefu thabiti wa kukaribisha wageni kwenye Airbnb. Ukadiriaji unategemea tathmini za wageni kwa matangazo wanayokaribisha wageni au mwenyeji mwenza na huenda usiwakilishe huduma za kipekee za mwenyeji mwenza.