Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa
  Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

  Vistawishi bora vya kutoa hivi sasa

  Kuanzia Wi-Fi inayoaminika hadi sehemu inayowafaa wanyama vipenzi, haya ndiyo mambo ambayo wageni wanajali zaidi.
  Na Airbnb tarehe 18 Jun 2020
  Inachukua dakika 4 kusoma
  Imesasishwa tarehe 17 Mac 2022

  Vidokezi

  • Vistawishi maarufu zaidi hivi sasa ni pamoja na sehemu inayowafaa wanyama vipenzi, Wi-Fi na maegesho ya bila malipo

  • Fikiria kuhusu kile kinachoweza kuwavutia wasafiri tofauti, ikiwemo familia na watu wanaofanya kazi wakiwa mbali

  • Sasisha tangazo lako

  Kulingana na takwimu mpya ya Airbnb,* wageni mara nyingi huchuja matokeo yao ya utafutaji ili kupata vistawishi 10 bora. Ikiwa una mojawapo ya vistawishi hivi maarufu, hakikisha kwamba unavijumuisha kwenye tangazo lako ili wageni waweze kukupata wanapotafuta.

  Kile ambacho wageni wanataka zaidi kwa sasa

  Nyumba iliyo mbali na nyumbani
  Matokeo ya utafutaji ya wageni ulimwenguni kote yanaonyesha kwamba vistawishi 10 bora ambavyo wageni wanataka hivi sasa ni:

  1. Bwawa
  2. Wi-Fi
  3. Jiko
  4. Maegesho ya bila malipo
  5. Jakuzi
  6. Mashine ya kufua au mashine ya kukausha
  7. Kiyoyozi au kipasha joto
  8. Huduma ya kuingia mwenyewe
  9. Meza ya kufanyia kazi kwa kompyuta mpakato
  10. Wanyama vipenzi wanaruhusiwa

  Hivi ndivyo unavyoweza kufanya ili kuhakikisha kwamba baadhi ya vistawishi hivi vinafaa wageni kadiri iwezekanavyo:

  • Wi-Fi: Chunguza kwa makini ili kuhakikisha kwamba inafanya kazi na kwamba wageni wanajua jinsi ya kuingia. Fikiria kuweka ishara iliyofunikwa kwa tabaka jembamba mahali fulani kwenye sehemu yako iliyo na maelekezo muhimu.
  • Kiyoyozi: Tunajua kwamba mfumo wa viyoyozi si kitu cha kawaida katika baadhi ya maeneo. Ikiwa unao, wajulishe wageni mahali pa kupata vidhibiti na jinsi ya kuvitumia—ishara iliyofunikwa kwa tabaka jembamba yenye maelekezo inaweza kuwa na manufaa hapa pia. Ikiwa huna, fikiria kutoa kifaa kinachobebeka katika miezi ya majira ya joto.
  • Jiko: Wageni wanaweza kutaka kupika vyakula vyao wenyewe wakati wa ukaaji wao, kwa hivyo hakikisha kwamba una vyombo, sufuria na vikaango na vyombo vya kupikia. Ni wazo zuri kutaja vitu hivi katika maelezo ya tangazo lako.
  • Maegesho: Ikiwa una eneo la kuegesha kwa ajili ya wageni, kumbuka kutoa maelekezo yoyote kabla hawajawasili na usisahau kuchagua maegesho kama kistawishi kwenye tangazo lako.

  Sehemu za nje
  Wageni wengi wanataka kukaa katika maeneo yenye mambo ya kufanya nje. Ikiwa eneo lako lina vijia vizuri vya matembezi na shughuli nyingine za nje, wajulishe wageni kuzihusu katika kitabu chako cha mwongozo au mwongozo wa nyumba.

  Njia nyingine ya kuwasaidia kufurahia hewa safi ni kunadhifisha maeneo ya nje ya sehemu yako. Hakikisha kwamba mandhari ni nadhifu na uzingatie kuongeza (au kubadilisha) vistawishi vifuatavyo:

  • Fanicha za baraza
  • Jiko la kuchomea nyama
  • Vikombe na sahani za nje
  • Michezo na burudani nyingine

  Vifaa vya kufanyia usafi
  Wageni wengi watafurahia fursa ya kudumisha usafi. Ni wazo zuri kuweka:

  • Taulo za karatasi
  • Glavu zinazotumiwa mara moja na kutupwa
  • Kisafishaji cha sehemu mbalimbali
  • Vifutio au kinyunyizaji cha kuua viini
  • Kitakasa mikono cha kuua bakteria
  • Sabuni ya mikono
  Ikiwa unatoa mojawapo ya vistawishi hivi, hakikisha kwamba unavijumuisha kwenye tangazo lako ili wageni waweze kukupata wanapotafuta.

  Ni nani anayesafiri na jinsi ya kutimiza matarajio yake

  Familia zilizo na watoto
  Unaweza kuwasaidia wazazi walio na watoto wadogo wajihisi wamestareheka zaidi katika sehemu yako kwa kuweka baadhi ya vitu wanavyohitaji zaidi, kama vile:

  • Vitanda vya watoto
  • Viti vya watoto vya kulia chakula
  • Vizuizi vya watoto
  • Vikombe, sahani na vyombo vya watoto
  • Meza ambapo mtoto anabadilishiwa nepi
  • Vifaa vya kufuatilia wanachofanya watoto
  • Vifuniko vya soketi

  Unapaswa pia kuhakikisha kwamba una vitu muhimu vya kutosha kwa ajili ya matumizi ya kawaida, kama vile:

  • Sabuni
  • Shampuu
  • Karatasi ya choo
  • Matandiko na taulo za ziada

  Pata maelezo zaidi kuhusu kukaribisha familia

  Wazazi wa wanyama vipenzi
  Wageni wengi wanataka kusafiri pamoja na wanafamilia wenye miguu minne. Tunajua kwamba haiwezekani kwa baadhi ya Wenyeji kutoa sehemu inayowafaa wanyama vipenzi. Lakini ukiweza, sasa ni wakati mzuri wa kufanya hivyo.

  Wageni wanaosafiri na wanyama vipenzi wanaweza kutaka kujua nini cha kutarajia kwenye sehemu yako, kama vile iwapo una ua uliozungushiwa uzio au baraza binafsi. Unaweza pia kutaka kutoa vistawishi vinavyowafaa wanyama vipenzi kama vile:

  • Mabakuli ya chakula na maji
  • Vifuniko vya fanicha
  • Taulo zilizobainishwa za kufuta miguu ya wanyama vipenzi mlangoni
  • Vifaa vya ziada vya kufanyia usafi

  Pia ni wazo zuri kusasisha sheria za nyumba yako. Unaweza kuwajulisha wageni mambo kama vile idadi ya wanyama vipenzi unaoruhusu kwa kila ukaaji, ni aina gani ya wanyama vipenzi unaokubali na ikiwa ni sawa kumwacha mnyama kipenzi bila uangalizi kwenye sehemu yako.

  Pata maelezo zaidi kuhusu kukaribisha wanyama vipenzi

  Watu wanaofanya kazi wakiwa mbali
  Watu wengi wanaendelea kufanya kazi zao wakiwa mbali na wanaweza kuamua kufanya kazi wakiwa safarini. Unaweza kuwasaidia waendelee kuwa na tija kwa kujumuisha vistawishi vifuatavyo:

  • Wi-Fi ya kasi: Wageni wana matarajio makubwa ya intaneti ya kasi sasa hivi kwa kuwa wengi wao wanafanya kazi wakiwa mbali. Unaweza kufanya majaribio ya kasi ya Wi-Fi yako kwa kutumia programu yako ya Airbnb na ikiwa matokeo yako ni ya polepole, fikiria kuboresha kwenda huduma ya kasi.
  • Meza ya kufanyia kazi kwa kompyuta mpakato: Tafuta dawati au meza karibu na chanzo cha umeme iliyo na kiti chenye kustarehesha (ni bora zaidi ikiwa kinafaa kwa ajili ya mkao wako). Unataka kufanya zaidi ya matarajio? Weka kibanio, rundo la madokezo ya kubandika na kikombe kilichojaa kalamu mpya. Ikiwa una printa au mashine ya kunakili, hakikisha kwamba unayaangazia kwenye maelezo ya tangazo lako.
  • Mashine ya kutengenezea kahawa na birika la chai: Wageni hawa wana uwezekano wa kuthamini msaada kidogo wa kuchangamsha siku zao zenye shughuli nyingi.
  • Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuweka vistawishi vipya

  Kumbuka kusasisha tangazo lako

  Usisahau kuonyesha mabadiliko ambayo umefanya kwa kusasisha vistawishi vyako, maelezo ya tangazo na picha. Kuweka vitu vichache tu vinavyotafutwa sana kunaweza kusaidia katika kuwafanya wageni wahisi wamestareheka zaidi katika sehemu yako na kunaweza kusababisha tathmini nzuri.

  *Kulingana na takwimu za ndani za Airbnb zlizopima vistawishi vilivyotafutwa mara nyingi zaidi ulimwenguni kote kuanzia tarehe 1 Januari hadi tarehe 31 Desemba, 2021.

  Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

  Vidokezi

  • Vistawishi maarufu zaidi hivi sasa ni pamoja na sehemu inayowafaa wanyama vipenzi, Wi-Fi na maegesho ya bila malipo

  • Fikiria kuhusu kile kinachoweza kuwavutia wasafiri tofauti, ikiwemo familia na watu wanaofanya kazi wakiwa mbali

  • Sasisha tangazo lako
  Airbnb
  18 Jun 2020
  Ilikuwa na manufaa?