Weka mkakati wako wa bei

Rekebisha upatikanaji wako na utoe mapunguzo ili kushughulikia mahitaji ya wageni.
Na Airbnb tarehe 1 Des 2020
Imesasishwa tarehe 9 Jan 2025
Weka mkakati wako wa bei
Kupanga bei yenye ushindani
Weka mkakati wako wa bei

Kupitia bei yako mara kwa mara kunakusaidia usalie kuwa mwenye ushindani. Fikiria vidokezi vifuatavyo unapoandaa mkakati wako wa kupanga bei.

Cha kufanya mara kwa mara

Amua ni mara ngapi unataka kutathmini na kurekebisha bei yako. Haya ni mambo machache ya kufanya kwenye ratiba inayokufaa.

  • Fungua usiku zaidi: Fungua usiku wowote katika kalenda yako ambao unajua unaweza kukaribisha wageni. Hatua hii husaidia tangazo lako lionekane zaidi katika matokeo ya utafutaji na inaweza kuongeza mapato yako.
  • Fanya urefu wa safari uwe mahususi: Angalia mapengo kati ya nafasi zilizowekwa. Ikiwa mapengo ni mafupi kuliko kima cha chini cha safari yako, hakuna mtu anayeweza kuweka nafasi ya usiku huo. Kuweka muda wa chini wa kukaa kwa tarehe mahususi kunaweza kukusaidia kujaza kalenda yako.
  • Linganisha matangazo sawia: Kuangalia bei za nyumba zilizowekewa nafasi na ambazo hazijawekewa nafasi katika eneo lako kunaweza kukusaidia kuweka bei yenye ushindani.

"Ninapenda kuangalia matangazo sawia ili niweze kulinganisha bei zangu, kuhakikisha kwamba bei yangu si ya juu sana au ya chini sana na kutafuta bei iliyo bora," anasema Karen, Mwenyeji Bingwa huko Nelson, Kanada.

Pia unaweza kuwasha kipengele cha Upangaji Bei Kiotomatiki wakati wowote ili urekebishe bei yako kulingana na uhitaji wa eneo lako. Zana hii ni muhimu sana ikiwa unataka kuboresha bei yako bila kuifuatilia kila wakati.

Kushughulikia nyakati ambazo wageni ni wachache

Hata matangazo maarufu zaidi yanaweza kuwa na vipindi vya ukimya vyenye nafasi chache zinazowekwa. Hizi hapa ni njia chache za kusaidia tangazo lako lionekane zaidi unapojiandaa kwa nyakati ambazo hazina wageni wengi.

  • Toa mapunguzo: Mapunguzo kwa sehemu za kukaa kuanzia wiki moja na sehemu za kukaa kuanzia mwezi mmoja yanaweza kusaidia kujaza kalenda yako na kupunguza idadi ya wageni wanaoingia na kutoka. Kuweka punguzo la dakika za mwisho kunaweza kuwavutia wageni wanaoweka nafasi siku 1 hadi 28 kabla ya kuwasili.
  • Fupisha ilani ya mapema: Kuwaruhusu wageni waweke nafasi karibu na wakati wa kuingia kunaweza kukusaidia kuvutia nafasi zaidi zinazowekwa. Chagua muda wa mapema ambao ni mfupi kama siku hiyo hiyo, kulingana na muda unaohitaji kati ya uwekaji nafasi wa mgeni na kuwasili.
  • Ruhusu ukaaji wa muda mfupi: Kupunguza kima cha chini cha urefu wa safari yako huwavutia wageni wanaoweka nafasi ya ukaaji wa muda mfupi. Una chaguo la kuweka kima mahususi cha chini cha safari yako kulingana na siku ya wiki.

"Kwa kweli ninapata sehemu zaidi za kukaa ambazo ni za muda mfupi," anasema Jimmy, Mwenyeji Bingwa huko Palm Springs, California. "Ni sehemu za kukaa za dakika za mwisho ambazo watu hawajapanga, kwa hivyo siku mbili zinaonekana kama likizo nzuri. Urahisi ni wa kuvutia."

Kushughulikia nyakati ambazo wageni ni wengi

Nyenzo kadhaa za Airbnb zinaweza kukusaidia ufaidike zaidi na nyakati ambazo mahitaji ya wageni ni makubwa. Hizi ni mbinu chache za kuzingatia.

  • Weka punguzo kwa watakaowahi: Kutoa punguzo kwa nafasi zilizowekwa mwezi 1 hadi 24 kabla ya kuingia hukusaidia kuwavutia wageni wanaopanga mapema. Kwa mapunguzo ya asilimia 3 au zaidi, wageni wanaona wito maalumu katika matokeo ya utafutaji na kwenye ukurasa wako wa tangazo. Bei yako iliyopunguzwa inaonekana kando ya ile yako ya awali, ambayo imepigwa kistari.
  • Weka promosheni mahususi: Kuendesha promosheni ni njia nzuri ya kuchochea nafasi zaidi zinazowekwa kwa nyakati fulani. Unapotoa mapunguzo ya asilimia 15 au zaidi, wageni wanaona wito maalumu kwenye ukurasa wako wa tangazo na katika matokeo ya utafutaji. Kuna matakwa fulani ya kuendesha promosheni, kama vile kuwa na angalau nafasi moja iliyowekwa katika mwaka uliopita.
  • Ongeza kipindi chako cha upatikanaji: Unaweza kufungua kalenda yako hadi miaka miwili mapema. Tangazo lako litaonekana katika matokeo zaidi ya utafutaji na katika orodha fupi ya matokeo ikiwa kuna maeneo machache yanapatikana wakati huo.

"Wakati mwingine ninapata watu wanaoweka nafasi mwaka mmoja mapema kwa ajili ya likizo zao za majira ya joto au kwa ajili ya Krismasi miezi sita mapema," anasema Anne, Mwenyeji Bingwa huko Tarragona, Uhispania. "Watu ambao huwa wanaweka nafasi mapema kwa kawaida hawaghairi. Ni muhimu pia kwa sababu utajua mapema kinachokuja."

Unadhibiti bei yako na mipangilio mingine nyakati zote. Matokeo yako yanaweza kutofautiana.

Wenyeji walilipwa kwa ushiriki wao katika mahojiano.

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Weka mkakati wako wa bei
Kupanga bei yenye ushindani
Weka mkakati wako wa bei
Airbnb
1 Des 2020
Ilikuwa na manufaa?