Kuelewa bei kwenye Airbnb
Kuna aina 3 za bei kwenye Airbnb: msingi, wikendi na mahususi. Zinashirikiana ili kusaidia tangazo lako lionekane mwaka mzima na kukusaidia kufikia malengo yako ya mapato.
Airbnb hutoa vidokezi mahususi vya bei kwa aina zote 3 za bei. Hutumia vipengele ikiwemo eneo, vistawishi, nafasi ulizowekewa hapo awali na bei za hivi karibuni katika eneo lako.
Bei ya msingi
Bei yako ya msingi ndiyo bei chaguomsingi kwa usiku wote kwenye kalenda yako. Kwanza unachagua bei hii katika Anza Kutumia Airbnb na unaweza kuibadilisha katika mipangilio yako ya bei wakati wowote.
Kidokezi cha bei ya msingi kilicho na bei inayopendekezwa kinaonekana chini ya idadi unayoweka. Ikiwa unataka kuweka bei tofauti, jaribu kusawazisha gharama zako na kile ambacho wageni wako tayari kulipa. Haya ni mambo machache ya kuzingatia.
- Gharama zako za kukaribisha wageni: Zingatia mambo kama vile rehani, huduma, matengenezo na kodi.
- Thamani unayotoa: Zingatia njia za kufanya tangazo lako liwe tofauti kwa kuangazia vistawishi maarufu, vipengele vya ufikiaji na ukaribu na vivutio vya eneo husika.
- Matangazo sawia: Tumia nyenzo hii ya kupanga bei ili kulinganisha bei ya wastani ya nyumba zilizowekewa nafasi na ambazo hazijawekewa nafasi kwenye ramani ya eneo lako. Matangazo sawia hayataonekana ikiwa unatumia kipengele cha Upangaji Bei Kiotomatiki.
- Jumla ya bei ambayo wageni wanalipa: Ada zozote unazoweka, kama vile ada ya usafi, huathiri jumla ya bei.
Kuanza na bei ya chini ya msingi kunaweza kukusaidia kuwavutia wageni wako wa kwanza na tathmini unapojitahidi kufikia malengo yako ya mapato.
Bei ya wikendi
Unaweza kuongeza malipo kwa wikendi, ambayo ni Ijumaa na Jumamosi usiku. Kubadilisha bei yako kulingana na usiku kunaweza kusaidia kuongeza nafasi zinazowekwa.
Kidokezi cha bei ya wikendi kinaonekana chini ya idadi unayoweka na ni ongezeko la asilimia juu ya bei yako ya msingi. Usipoweka bei ya wikendi, bei yako ya msingi inatumika kwa kila siku ya wiki.
Bei mahususi
Unaweza kuweka bei mahususi kwa usiku wowote. Hii inabatilisha bei yako ya msingi au wikendi kwa usiku unaochagua.
Vidokezi vya bei za kila usiku vinaonekana chini ya bei yako mahususi kila siku ya kalenda yako ili kukusaidia kuweka bei kwa siku tofauti, misimu na matukio maalumu.
Kwa nini huenda usione vidokezi vya bei
Ikiwa huoni vidokezi vya bei, hii inaweza kuwa kwa sababu:
- Kipengele cha Upangaji Bei Kiotomatiki kimewashwa
- Bei yako iko ndani ya kiwango kilichopendekezwa
- Mapunguzo au promosheni tayari zimetumika kwenye usiku huo
- Hakuna data ya kutosha ya kuunda vidokezi vya bei
Ikiwa ungependa kurekebisha bei yako kiotomatiki, washa kipengele cha Upangaji Bei Kiotomatiki.
Unadhibiti bei yako na mipangilio mingine nyakati zote. Matokeo yako yanaweza kutofautiana.
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.