Punguza vitu kwenye sehemu yako ili kuwafurahisha wageni

Eneo lenye mpangilio ni zuri kwa wageni na ni rahisi kwa wasafishaji kulifanyia usafi.
Na Airbnb tarehe 10 Feb 2020
Inachukua dakika 3 kusoma
Imesasishwa tarehe 8 Mac 2023

Wageni wanathamini sehemu safi na iliyopangwa. Iwe unakaribisha wageni kwenye chumba cha kujitegemea au nyumba nzima, jaribu vidokezi hivi kutoka kwa Wenyeji ili kupunguza vitu kwenye sehemu yako.

Kufanya eneo lako liwe safi kuliko hapo awali

"Ninaona kwamba kadiri msongamano vitu unavyokuwa mdogo, ndivyo sehemu hiyo inavyokuwa safi na nadhifu zaidi," anasema Kath, Mwenyeji huko Albany, Australia. Wageni wanajali sana usafi. Sehemu isiyo safi ni mojawapo ya sababu kuu za tathmini mbaya, kwa mujibu wa data ya Airbnb.

"Kupunguza mparaganyo na vitu kwenye sehemu zisizo na mwinuko ni muhimu," wanasema Wenyeji Bingwa Jay na Lynne huko Blanco, Texas. "Hii inafanya kufanya usafi kuwa rahisi zaidi, huwapa wageni nafasi ya kuweka vitu vyao na huwasaidia wageni wasisahau vitu, kwa sababu wanaweza kuviona wanapokiangazia macho chumba kwa mara ya mwisho."

Kuacha sehemu kwa ajili ya vitu vya wageni

Wageni wanahitaji maeneo ya kuweka nguo zao, vifaa vya usafi na vitu vingine binafsi. Kuwa na sehemu tupu ya kabati na droo kunaweza kukuhitaji kuondoa vitu visivyohitajika. "Ikiwa sijakitumia au kuvaa kwa mwaka mmoja au miwili, hakitatunzwa vizuri," anasema Sarah, Mwenyeji huko Sayulita, Meksiko.

Unaweza kutoa nafasi zaidi, hasa ikiwa unakaribisha wageni kwa ajili ya sehemu za kukaa za muda mrefu kama Jessica, Mwenyeji huko Seoul, Korea Kusini. "Nina hakika watakuwa na vitabu, zawadi za kumbukumbu, picha za familia, na ‘vitu vyao’ wanavyotaka kuweka kwenye meza ya kando ya kitanda au dawati au kwenye rafu," anasema.

Kupangilia vistawishi

Fikiria kuhusu njia bora ya kuonyesha vistawishi ili wageni waweze kuvipata kwa urahisi. Chantal, Mwenyeji huko Yvignac-la-Tour, Ufaransa, ana kabati maalumu kwa wageni: "Lina kila kitu kuanzia chupa ndogo za maji hadi karatasi ya choo, vyote vimepangwa kwa rafu na kwa aina katika vikapu tofauti."

Mara baada ya kupangilia vitu, kumbuka kuchukua hesabu ya mashuka na vifaa vingine na ugawe au utupe chochote ambacho kimechakaa.

Kuzingatia jiko na bafu

“Mimi binafsi sipendi wakati inaonekana kana kwamba kila kitu kilichomo jikoni kwenye tangazo kinatoka kwenye ununuzi wa ofa ya punguzo au vitu ambavyo vilitupwa mahali fulani,” anasema Alexandra, Mwenyeji huko Lincoln, California.

Toa kile ambacho wageni wanahitaji sana jikoni na kwenye mabafu, na uondoe vilivyobaki. Wengi watafurahia vitu kama kifungua chupa na kiyoyozi, lakini hawatahitaji aina tatu ya kila kimoja.

Kutupa mabaki

Inaweza kuonekana kuwa ni matumizi mabaya ya vitu kutunza vitu ambavyo wageni waliopita waliacha kwa ajili ya wageni wajao, lakini hilo si wazo zuri. Michelle, Mwenyeji huko Chicago, anaweka tu vyakula na vinywaji ambavyo "vimefungwa kama vilivyonunuliwa" kama vile maji ya kwenye chupa, soda viungo vya matumizi ya mara moja."

Kuweka msawazo

"Kila kitu kwenye chumba kinapaswa kuwa na kusudi," anasema Kelly, Mwenyeji huko Austin, Texas. "Hiyo haimaanishi kwamba chumba hakipaswi kuwa maridadi au kuwa na mwonekano wa kupendeza na kuvutia."

Uwiano sahihi kati ya kuvutia na umuhimu wa matumizi utatofautiana kutoka sehemu moja na nyingine, lakini kuna vidokezi kadhaa vya kuzingatia:

  • Usijiangalie wewe kupita kiasi. Weka maeneo ya wageni bila vitu kama vile picha za familia, michoro ya watoto, na mavazi na viatu.
  • Ubunifu kidogo ni jambo zuri. Kazi ya sanaa ya eneo husika ikiwa katika fremu, samani ya kipekee au kioo cha aina yake vinaweza kuifanya sehemu yako ionekane zaidi.
  • Ongeza mapambo kiasi. Vitu kama vile mimea na mito vinaweza kuipa sehemu yako hisia ya kuwa nyumbani, maadamu vimetumika kidogo na kupangwa kwa makusudi.
Airbnb
10 Feb 2020
Ilikuwa na manufaa?