Unachohitaji kujua kuhusu kukaribisha familia zilizo na watoto
Andaa sehemu yako kwa uzingativu na usasishe tangazo lako.
Na Airbnb tarehe 21 Jul 2020
Imesasishwa tarehe 18 Jun 2025
Maelezo madogo yanaweza kuleta tofauti kubwa kwa mtu yeyote anayesafiri na watoto wadogo. Kutoa vistawishi maalumu au vifaa kwa ajili ya familia kunaweza kuifanya nyumba yako ivutie wageni wengi zaidi.
Kuandaa sehemu yako
Fikiria kusasisha nyumba yako ili kuifanya iwe ya kufaa kwa familia. Hakikisha unachukua tahadhari za msingi za usalama ili kusaidia kulinda wageni wako na nyumba yako.
- Chagua fanicha imara na salama na uepuke vioo, ikiwezekana.
- Weka vitu vinavyoweza kuvunjika na vyenye ncha kali mahali ambapo watoto hawawezi kufikia.
- Zuia uwezekano wa vyombo kuvunjika kwa kuweka vikombe na sahani za plastiki zinazoweza kutumika tena jikoni mwako.
- Weka makomeo kwenye makabati na vifuniko vya ulinzi kwenye soketi za umeme.
- Chagua nyenzo za kudumu, ambazo ni rahisi kusafisha, kama vile vitambaa vyenye utendaji wa juu.
- Toa vitu vinavyoombwa sana, kama vile taulo na mashuka ya ziada.
- Funika sakafu za mbao ngumu kwa mikeka inayoweza kuoshwa.
- Weka ving'ora vya moshi na kaboni monoksidi na ubadilishe betri mara kwa mara.
- Weka kizima moto karibu na jiko la jikoni.
- Jumuisha nambari za simu za dharura za eneo lako katika mwongozo wa nyumba yako na kwenye kadi ya marejeleo ya haraka kwa ajili ya wageni.
Kusasisha tangazo lako
Mara baada ya kuandaa nyumba yako, onyesha upya maelezo ya tangazo lako na usasishe vistawishi ili kusaidia kuvutia nafasi zinazowekwa na kuweka matarajio. Wageni wanaweza kutumia vichujio vya utafutaji ili kupunguza machaguo yao.
- Weka kila kistawishi unachotoa, ikiwemo vitu maarufu kama vile kitanda cha mtoto na kiti cha watoto kukalia wanapokula.
- Ikiwa una mashine ya kuosha au ya kukausha, taja iwapo unatoa sabuni ya kufulia na ikiwa kuna tozo zozote za ziada.
- Ikiwa una beseni la kuogea, weka kidokezo katika maelezo ya tangazo lako na ujumuishe picha kwenye matunzio yako ya picha.
- Kagua kwa makini kwamba picha zako zinaonyesha kila kitu ambacho umeelezea.
- Weka mapendekezo yanayofaa familia kwenye kitabu chako cha mwongozo, kama vile viwanja vya michezo vilivyo karibu na mahali pa kuchukua au kujaza tena vifaa.
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.
Airbnb
21 Jul 2020
Ilikuwa na manufaa?