Kugeuza mahitaji ya juu kuwa mapato ya juu

Tumia zana za kukaribisha wageni za Airbnb ili kukusaidia kufaidikia zaidi na misimu yenye shughuli nyingi.
Na Airbnb tarehe 6 Jan 2025
Imesasishwa tarehe 19 Mac 2025

Likizo, hafla kubwa na hali nzuri ya hewa zinaweza kuongeza mvuto kwenye tangazo lako. Nyenzo za kukaribisha wageni za Airbnb hukusaidia kutumia vizuri zaidi vipindi hivi vya mahitaji ya juu. Zingatia hatua hizi za kuboresha mapato yako.

Endelea kusasisha kalenda yako

Njia moja ya kujiandaa kwa ajili ya msimu wenye mahitaji mengi ni kufungua usiku wa ziada katika kalenda yako. Hatua hii husaidia tangazo lako lionekane zaidi katika matokeo ya utafutaji na inaweza kuongeza mapato yako.

Nenda kwenye kalenda ya tangazo lako na utafute usiku uliozuiwa, ambao unaonekana katika rangi ya kijivu. Fungua usiku wowote uliozuiwa ambao unaweza kukaribisha wageni.

Kuongeza muda wa upatikanaji wako kunawawezesha wageni waweke nafasi mapema zaidi. Mkakati huu ni mzuri hasa kwa maeneo yenye vipindi vinavyotabirika vya mahitaji makubwa, kama vile matukio makubwa ya kila mwaka na misimu ya theluji na ya ufukweni.

Kalenda yako inafunguliwa siku moja moja bila kujali kipindi chako cha upatikanaji. Kwa mfano, ikiwa kipindi chako ni miezi 12, wageni wanaweza kuweka nafasi katika eneo lako hadi mwaka mmoja kabla ya tarehe ya leo  tarehe na upatikanaji wako utasasishwa kila siku.

Weka bei yenye ushindani

Angalia bei za matangazo kama hayo katika eneo lako ili uendelee kuwa na ushindani wakati wa misimu yenye mahitaji makubwa. Ili kulinganisha matangazo yanayofanana, nenda kwenye kalenda ya tangazo lako na uchague mwachano wa tarehe hadi siku 31.

Utaona bei za wastani za matangazo yanayofanana na lako kwenye ramani ya eneo lako. Sababu zinazoamua ni nyumba gani zinazofanana ni pamoja na eneo, ukubwa, vipengele, vistawishi, ukadiriaji, tathmini na matangazo mengine ambayo wageni wanavinjari huku wakizingatia yako.

Matangazo yenye bei ya chini kuliko matangazo yanayofanana nayo yaliyo karibu huwa kwenye nafasi ya juu katika matokeo ya utafutaji.

Ikiwa unatoa bei hiyo hiyo kila usiku, fikiria kubadilisha bei zako siku za wiki na wikendi ili zilingane na mahitaji. Kuweka bei inayobadilika kunaweza kusaidia kuongeza nafasi unazowekewa.

Weka punguzo

Kuweka punguzo ni njia nyingine ya kuonekana kwa wageni. Unaweza kuwahudumia wasafiri anuwai kwa kutoa:

  • Mapunguzo ya kila wiki na kila mwezi. Toa mapunguzo ya kila wiki kwa ajili ya ukaaji wa usiku saba au zaidi au mapunguzo ya kila mwezi kwa ajili ya ukaaji wa usiku 28 au zaidi. Hii inaweza kuongeza muda wa wastani wa kukaa katika matangazo yako yote na kupunguza idadi ya wageni wanaotoka.
  • Punguzo kwa watakaowahi. Weka punguzo kwa nafasi zilizowekwa mwezi 1 hadi 24 kabla ya kuingia na ujenge msingi thabiti wa nafasi zilizowekwa kabla ya misimu yenye shughuli nyingi.
  • Punguzo la dakika za mwisho. Kupunguza bei yako ya kila usiku wakati tarehe ya kuingia inakaribia kunaweza kukusaidia kuwavutia wasafiri wanaofanya maamuzi dakika za mwisho. Mapunguzo kwa nafasi zilizowekwa siku 1 hadi 28 kabla ya kuingia yanaweza kusaidia kujaza kalenda yako na kuongeza mapato yako.

Wageni wanaona wito maalumu katika matokeo ya utafutaji na kwenye ukurasa wako wa tangazo kwa mapunguzo ya kila wiki, kila mwezi na mapunguzo ya dakika za mwisho ya asilimia 10 au zaidi na kwa mapunguzo kwa watakaowahi ya asilimia 3 au zaidi. Bei yako iliyopunguzwa inaonekana kando ya yako ya awali, ambayo imepigwa kistari.

Kumbuka kwamba punguzo kwa watakaowahi halipatikani wakati kipengele cha Upangaji Bei Kiotomatiki kimewashwa na kwamba mapunguzo ya muda wa ukaaji yanahitaji kufuata sheria na kanuni za eneo husika.

Andaa ziara ya picha

Picha nzuri huvutia umakini, husaidia kuweka matarajio dhahiri na kuwapa wageni uhakika zaidi wa kuweka nafasi kwenye nyumba yako. Fikiria kusasisha picha za tangazo lako unapojiandaa kwa misimu yenye mahitaji mengi.

  • Panga picha zako. Zingatia kupata picha zinazoonyesha maelezo ya kipekee ya nyumba yako, vistawishi maarufu na vipengele vya ufikiaji. Piga picha ya kila chumba na sehemu ambayo wageni wanaweza kutumia kutoka pembe mbalimbali.
  • Pakia picha za mlalo na zenye mwanga wa hali ya juu. Picha zinapaswa kuwa angalau pikseli 800 kwa pikseli 1,200. Mafaili makubwa ni bora zaidi, hadi takriban megabaiti 10.
  • Tumia mtaalamu. Zingatia kuajiri mpiga picha mtaalamu ili akusaidie. Airbnb inaweza kukuunganisha na mtaalamu katika miji mahususi duniani kote.
  • Unda ziara ya picha. Nyenzo ya Airbnb hupanga kiotomatiki picha zako zilizopakiwa kulingana na chumba ili kuwasaidia wageni waelewe mpangilio wa nyumba yako. Unaweza kusogeza, kuondoa na kuongeza picha, uweke maelezo kwenye kila chumba na uandike maelezo mafupi kwa kila picha.

Fanya mchakato wa kuingia na kutoka uwe rahisi

Njia nyingine ya kufanya tangazo lako livutie zaidi ni kurahisisha kuingia na kutoka.

  • Weka huduma ya mgeni kuingia mwenyewe. Kuweka kufuli janja, msimbo au kisanduku cha funguo huwaruhusu wageni wafungue mlango kwa msimbo. Wageni wengi wanapendelea urahisi wa kuingia wenyewe na inaweza kuokoa muda wako. Njia yoyote unayochagua, ni muhimu kumpa kila mgeni aliyeweka nafasi msimbo wa kipekee wa ufikiaji. .
  • Toa maelekezo ya kutoka. Jumuisha hatua zilizo wazi na rahisi, kama vile mahali pa kuweka funguo na kile kinachohitaji kufungwa.

"Ni muhimu usiwalemee wageni kwa kazi hizo kwa sababu jambo la mwisho ambalo ningependa wakumbuke ni urefu wa orodha hiyo kabla ya kutoka," anasema Katie, mwanabodi wa Bodi ya Ushauri ya Wenyeji na Mwenyeji Bingwa huko Palm Springs, California. "Unaweza kujipatia tathmini ya nyota tano kwa sababu tu huna orodha ndefu ya kutoka."

Jiunge na Kilabu ya Wenyeji wa eneo husika

Mamia ya Vilabu vya Wenyeji ulimwenguni kote huwasaidia wenyeji wa Airbnb kuungana na kufunzana. Tumeona kwamba wanachama wa vilabu hivi vya mahali husika hupata mapato mara mbili kuliko wenyeji ambao si wanachama wa kilabu,* na wana uwezekano wa kuwa Wenyeji Bingwa karibu mara tatu.**

Shughuli maarufu za kilabu zinajumuisha:

  • Kubadilishana vidokezi vya kukaribisha wageni ambavyo vinaweza kuongeza mapato
  • Kujadili kanuni za ukodishaji wa muda mfupi
  • Kushiriki huduma za kuaminika za mahali husika (wafanya usafi, mafundi bomba, n.k.)
  • Kuhudhuria hafla za kipekee za kukuza mtandao

*Kulingana na takwimu za ndani za Airbnb, unapolinganisha wastani wa mapato na ukadiriaji wa wastani wa wanachama wa Kilabu cha Wenyeji cha Airbnb ulimwenguni dhidi ya idadi nzima ya wenyeji ulimwenguni kuanzia Septemba 2022 hadi Septemba 2023. Data ya mapato inatofautiana kulingana na mahali, msimu na aina ya tangazo.

**Kulingana na data ya ndani ya Airbnb kuhusu hadhi ya Mwenyeji Bingwa kwa wenyeji waliojiunga kuanzia Julai 2023 hadi Julai 2024.

Unadhibiti bei yako na mipangilio mingine nyakati zote. Matokeo yako yanaweza kutofautiana.

Wenyeji walilipwa kwa ushiriki wao katika mahojiano.

Vidokezi vya kukaribisha wageni vinadhibitiwa na sheria za eneo husika.

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Airbnb
6 Jan 2025
Ilikuwa na manufaa?