Kuboresha msimu wenye wageni wengi

Fungua kalenda yako, weka bei ya ushindani na urahisishe kuingia na kutoka.
Na Airbnb tarehe 11 Nov 2024
Imesasishwa tarehe 19 Mac 2025

Msimu wa kilele unakuja. Hizi ni njia chache ambazo unaweza kutumia zana za kukaribisha wageni za Airbnb ili kufaidika zaidi na wakati ambapo mahitaji ya wageni ni makubwa.

Endelea kusasisha kalenda yako

Jitayarishe kwa ajili ya msimu wenye shughuli nyingi katika eneo lako kwa kufungua usiku wa ziada katika kalenda yako. Hatua hii husaidia tangazo lako lionekane zaidi katika matokeo ya utafutaji na inaweza kuongeza mapato yako.

Zingatia kima cha chini cha urefu wa safari yako unapofungua usiku katika kalenda yako. Utahitaji kukaa ndani ya kima cha chini cha safari yako au kupunguza kima cha chini cha urefu wa safari yako ya kawaida. Pia unaweza kuunda urefu mahususi wa safari kwa usiku mahususi unaofungua.

"Ni muhimu sana uhakikishe kwamba kalenda inafunguliwa wakati wa msimu wenye shughuli nyingi," anasema Myranda, Mwenyeji Bingwa huko Little Rock, Arkansas. "Badala ya kupumzika siku kadhaa baada ya mgeni kutoka, ninahakikisha kuwa ninaweza kubadilika zaidi katika msimu huo ili niweze kukaribisha wageni zaidi."

Nenda kwenye kalenda ya tangazo lako na utafute usiku uliozuiwa, ambao unaonekana katika rangi ya kijivu. Fungua usiku wowote uliozuiwa ambao unaweza kukaribisha wageni.

Kuongeza muda wa upatikanaji wako zaidi ya kima cha chini cha miezi mitatu kunawawezesha wageni waweke nafasi mapema zaidi. Unaweza kufungua kalenda yako hadi miaka miwili mapema. Tangazo lako litaonekana katika matokeo zaidi ya utafutaji na katika orodha fupi ya matokeo ikiwa kuna maeneo machache yanayopatikana wakati huo.

Kalenda yako inafunguliwa siku moja moja bila kujali kipindi chako cha upatikanaji. Kwa mfano, ikiwa kipindi chako ni miezi 12, wageni wanaweza kuweka nafasi katika eneo lako hadi mwaka mmoja kabla ya tarehe ya leo.

"Tumia fursa wakati mahitaji ni mengi," anasema Jimmy, Mwenyeji Bingwa huko Palm Springs, California. "Labda wenyeji wengine hawako tayari na kalenda zao hazijafunguliwa. Kwa kuchukua hatua mapema, utajifaidi katika vipindi hivyo vya mahitaji makubwa."

Weka bei yenye ushindani

Ili uendelee kuwa na ushindani wakati wa msimu wenye idadi kubwa ya watu, angalia bei za matangazo yanayofanana na lako katika eneo lako na uzingatie kurekebisha bei yako ya kila usiku. Ikiwa unatoa bei hiyo hiyo kila usiku, fikiria kubadilisha bei zako siku za wiki na wikendi ili zilingane na mahitaji. Kuweka bei inayobadilika kunaweza kusaidia kuongeza nafasi unazowekewa na mapato yako.

Ili kulinganisha matangazo yanayofanana, nenda kwenye kalenda ya tangazo lako na uchague mwachano wa tarehe hadi siku 31. 

Utaona bei za wastani za matangazo sawia yaliyo karibu kwenye ramani ya eneo lako. Vitufe kwenye ramani hukuruhusu kuangalia matangazo yaliyowekewa nafasi au ambayo hayajawekewa nafasi. Sababu zinazoamua ni matangazo gani yanayofanana ni pamoja na eneo, ukubwa, vipengele, vistawishi, ukadiriaji, tathmini na matangazo mengine ambayo wageni wanavinjari huku wakizingatia lako.

Matangazo yenye bei ya chini kuliko matangazo yanayofanana nayo yaliyo karibu huwa kwenye nafasi ya juu katika matokeo ya utafutaji.

"Ikiwa ni wakati wenye shughuli nyingi na bado hatuwekewi nafasi, mimi hukagua mara mbili nyumba zilizo katika eneo langu," anasema Felicity, Mwenyeji Bingwa huko Sydney, Australia. "Ninapaswa kuwa na bei ya ushindani."

Weka punguzo

Kuweka punguzo ni njia nyingine ya kuonekana kwa wageni wakati wa msimu wako wenye shughuli nyingi. Unaweza kuwahudumia wasafiri anuwai kwa kutoa:

  • Mapunguzo ya kila wiki na kila mwezi. Fikiria kutoa mapunguzo ya kila wiki kwa ajili ya ukaaji wa usiku saba au zaidi na mapunguzo ya kila mwezi kwa ajili ya ukaaji wa usiku 28 au zaidi. Hii inaweza kusaidia kuboresha nafasi yako kwenye utafutaji, kujaza nafasi kwenye kalenda yako na kupunguza idadi ya wageni wanaoingia na kutoka.
  • Punguzo kwa watakaowahi. Kuweka punguzo kwa watakaowahi kwa nafasi zilizowekwa mwezi 1 hadi 24 kabla ya kuingia kunaweza kukusaidia kuwavutia wageni wanaopanga mapema.

Wageni wanaona wito maalumu katika matokeo ya utafutaji na kwenye ukurasa wako wa tangazo kwa mapunguzo ya kila wiki au kila mwezi ya asilimia 10 au zaidi na kwa mapunguzo kwa watakaowahi ya asilimia 3 au zaidi. Bei yako iliyopunguzwa inaonekana kando ya bei yako ya awali, ambayo imepigwa kistari.

Kumbuka kwamba punguzo kwa watakaowahi halipatikani wakati kipengele cha Upangaji Bei Kiotomatiki kimewashwa na kwamba mapunguzo ya muda wa ukaaji yanahitaji kufuata sheria na kanuni za eneo husika.

"Ninatumia punguzo kwa watakaowahi ninapopangilia kalenda yangu kwa mwaka," anasema Anne, Mwenyeji Bingwa huko Tarragona, Uhispania. "Hii huwa inajaza kalenda yangu haraka na watu wanaopata punguzo kwa kawaida hawaghairi."

Fanya mchakato wa kuingia na kutoka uwe rahisi

Angalia njia za kurahisisha kuwasili na kuondoka kwa wageni wako. Jumuisha maelekezo ya kuingia ili kuwasaidia kuelewa jinsi ya kufika kwako na kufungua mlango wa mbele wanapowasili.

  • Weka maelezo muhimu. Unaweza kuweka na kurekebisha njia yako ya kuingia, muda na maelekezo katika mwongozo wako wa kuwasili. Kutoa huduma ya mgeni kuingia mwenyewe kwa kufuli janja, msimbo au kisanduku cha funguo huwaruhusu wageni wafungue mlango kwa msimbo, hata kama wanawasili usiku sana.
  • Onyesha jinsi ya kuingia ndani. Jumuisha picha au video ya kuwasaidia wageni kuona taswira ya mchakato huo. Mwombe rafiki ajaribu maelekezo yako ili kuhakikisha kuwa yako wazi.

Fikiria kutoka kama jambo la mwisho ambalo wageni wako watakumbuka kuhusu sehemu yako. Kuifanya iwe rahisi kunaweza kuwakumbusha kuhusu ukaaji mzuri waliopata.

  • Toa maelekezo dhahiri ya kutoka. Chagua kutoka kwenye orodha ya majukumu katika mwongozo wako wa kuwasili. Eleza kile ambacho ni muhimu kwa wageni kufanya kabla ya kuondoka, kama vile kuzima vitu na kufunga. Mtu yeyote anaweza kuyasoma kabla ya kuweka nafasi.
  • Rahisisha kadiri uwezavyo. Fikiria ikiwa ni muhimu kwa wageni kufanya kazi fulani, kama vile kukusanya taulo zilizotumika na kutupa takataka.

"Ni muhimu kwa wageni kuwa na maelekezo moja au mawili tu rahisi kwa sababu wanajaribu kutoka kwenye nyumba yako," anasema Karen, Mwenyeji Bingwa huko Nelson, Kanada. "Inafanya mchakato huo kuwa rahisi sana."

Unadhibiti bei yako na mipangilio mingine nyakati zote. Matokeo yako yanaweza kutofautiana. 

Wenyeji walilipwa kwa ushiriki wao katika mahojiano.

Vidokezi vya kukaribisha wageni vinadhibitiwa na sheria za eneo husika.

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Airbnb
11 Nov 2024
Ilikuwa na manufaa?