Jinsi ya kuwa Mwenyeji Bingwa
Mpango wa Mwenyeji Bingwa wa Airbnb unatambua wenyeji wetu wenye ukadiriaji wa juu, wenye uzoefu zaidi.
Tunasherehekea na kutuza ukarimu wa kipekee kwa kuweka beji kwenye tangazo lao, jambo ambalo linaweza kusababisha uwekaji nafasi zaidi. Asilimia 59 ya wageni wanasema hadhi ya Mwenyeji Bingwa inawafanya wawe na uhakika zaidi katika ubora wa malazi na Wenyeji Bingwa hupata asilimia 60 zaidi kuliko wenyeji ambao si Wenyeji Bingwa* Wenyeji Bingwa pia wanapata Usaidizi mahususi wa Jumuiya, mialiko kwenye hafla maalumu, kuponi za kusafiri na ongezeko katika matokeo ya utafutaji.
Zaidi ya wenyeji milioni 1.3 wamekuwa Wenyeji Bingwa na wewe pia unaweza, kwa kuboresha nafasi unazowekewa na kutoa ukarimu bora.** Kufanya marekebisho machache kwenye kalenda yako, kusasisha tangazo lako na kuwa mwangalifu zaidi kwenye mawasiliano kunaweza kufanya mabadiliko makubwa.
Kidhi matakwa
Mwenyeji Bingwa lazima awe mmiliki wa tangazo aliye na akaunti yenye sifa nzuri na akidhi vigezo hivi vinne ndani ya siku 365 zilizopita:
- Pata nafasi za kutosha. Karibisha wageni kwa angalau nafasi 10 zilizowekwa au nafasi tatu zilizowekwa zenye jumla ya angalau usiku 100 kwa ukaaji wa mara tatu.
- Epuka ughairi. Dumisha kiwango cha kughairi cha chini ya asilimia 1, isipokuwa kwa ughairi kwa sababu ya Matukio Makubwa ya Usumbufu au sababu nyingine halali.
- Wajibu wageni. Dumisha kiwango cha kutoa majibu cha asilimia 90 au zaidi. Kiwango chako cha kutoa majibu ni asilimia ya maulizo mapya ya wageni ambayo umejibu ndani ya saa 24.
- Upatie ukarimu kipaumbele. Dumisha ukadiriaji wa jumla wa 4.8 au zaidi.
Kujibu kwa uwazi na kwa haraka, kuepuka kughairi na kuupa kipaumbele ukarimu pia kunaweza kusaidia nyumba yako ionekane zaidi katika matokeo ya utafutaji na kuongeza mapato yako.
Hivi ni vidokezi vya kukusaidia kukidhi vigezo hivi na kuanza kunufaika na hadhi ya Mwenyeji Bingwa.
Endelea kusasisha kalenda yako
Kufungua usiku zaidi katika kalenda yako husaidia tangazo lako lionekane zaidi katika matokeo ya utafutaji na huongeza fursa zako za kukaribisha wageni wa kutosha ili kukidhi vigezo vya Mwenyeji Bingwa.
Nenda kwenye kalenda ya tangazo lako na utafute usiku uliozuiwa, ambao unaonekana katika rangi ya kijivu. Fungua usiku wowote uliozuiwa ambao unaweza kukaribisha wageni.
Kuruhusu ukaaji wa muda mfupi ni njia nyingine ambayo tangazo lako linaweza kuonekana zaidi katika matokeo ya utafutaji. Unaweza kuweka kima cha chini cha safari yako kulingana na siku ya wiki. Kwa mfano, ikiwa mahitaji ya wageni ni makubwa wakati wa wikendi, unaweza kuchagua kuruhusu ukaaji wa usiku mmoja katikati ya wiki lakini si wakati wageni wanaweka nafasi ya Ijumaa au Jumamosi usiku.
Kutoa huduma inayoweza kubadilika zaidi na kuwaruhusu wageni waweke nafasi karibu na wakati wa kuingia pia husaidia kuvutia uwekaji nafasi zaidi. Chagua muda wa chini wa mapema ambao ni mfupi kama siku hiyo hiyo, kulingana na muda unaohitaji kati ya uwekaji nafasi wa mgeni na kuwasili kwake.
Unaweza pia kuruhusu maombi yenye ilani ya muda mfupi kuliko muda wako wa chini wa kuwasili. Utakumbushwa kupitia na kuidhinisha maombi haya.
Weka bei yenye ushindani
Matangazo yenye bei ya chini kuliko matangazo mengine sawia yaliyo karibu huwa kwenye nafasi ya juu katika matokeo ya utafutaji. Fikiria kurekebisha bei yako ya kila usiku ikilinganishwa na ushindani wako ili kukusaidia kukaribisha angalau nafasi 10 za ukaaji.
Ili kuangalia bei ya matangazo yanayofanana katika eneo lako, nenda kwenye kalenda ya tangazo lako na uchague mwachano wa tarehe wa hadi siku 31.
Utaona bei za wastani za matangazo yanayofanana na lako kwenye ramani ya eneo lako. Sababu zinazoamua ni matangazo gani yanayofanana ni pamoja na eneo, ukubwa, vipengele, vistawishi, ukadiriaji, tathmini na matangazo mengine ambayo wageni wanavinjari huku wakizingatia lako.
Ikiwa unatoa bei hiyo hiyo kila usiku, fikiria kurekebisha bei zako za siku za wiki na wikendi ili kuvutia wageni zaidi. Kubadilisha bei kulingana na usiku kunaweza kusaidia kuongeza nafasi unazowekewa na mapato yako.
Weka punguzo
Kuweka punguzo ni njia nyingine ya kuonekana kwa wageni. Unaweza kuwahudumia wasafiri anuwai kwa kutoa:
- Mapunguzo ya kila wiki na kila mwezi. Toa mapunguzo ya kila wiki kwenye ukaaji ambao ni usiku saba au zaidi au mapunguzo ya kila mwezi kwenye ukaaji ambao ni usiku 28 au zaidi. Hii inaweza kuongeza muda wa wastani wa kukaa katika matangazo yako yote na kupunguza idadi ya wageni wanaotoka.
- Punguzo kwa watakaowahi. Weka punguzo kwa nafasi zilizowekwa mwezi 1 hadi 24 kabla ya kuingia na ujenge msingi thabiti wa nafasi zilizowekwa kabla ya misimu yenye shughuli nyingi.
Wageni wanaona wito maalumu katika matokeo ya utafutaji na kwenye ukurasa wako wa tangazo kwa mapunguzo ya kila wiki au kila mwezi ya asilimia 10 au zaidi na kwa mapunguzo kwa watakaowahi ya asilimia 3 au zaidi. Bei yako iliyopunguzwa inaonekana kando ya bei yako ya awali, ambayo imepigwa kistari.
Kumbuka kwamba punguzo kwa watakaowahi halipatikani wakati kipengele cha Upangaji Bei Kiotomatiki kimewashwa na kwamba mapunguzo ya muda wa ukaaji yanahitaji kufuata sheria na kanuni za eneo husika.
Weka mkazo kwenye ukarimu wa nyota tano
Wageni wanathamini mawasiliano ya haraka, ya wazi na vigezo vya Wenyeji Bingwa vinahitaji wenyeji kuwa na kiwango cha kutoa majibu cha angalau asilimia 90. Kuandaa majibu ya haraka uwajibu wageni kwa urahisi na kwa ufanisi.
Majibu ya haraka ni violezo vya ujumbe mfupi ambavyo vinashughulikia mada mahususi ambazo wenyeji mara nyingi huulizwa. Unaweza kuyaandika au kuyahariri mapema ili kuyatuma unapokuwa ukipiga gumzo na mgeni.
Kulenga kupata tathmini za nyota tano pia kunamaanisha kutarajia mahitaji ya wageni na kujitahidi kadiri uwezavyo kuyakubali wakati wowote inapowezekana.
- Ongeza mguso binafsi.Mambo madogomadogo, kama vile kutoa kahawa uipendayo ya mahali ulipo au barua ya ukaribisho iliyoandikwa kwa mkono, yanaweza kusaidia sana kuwafanya wageni wahisi wamethaminiwa kipekee.
- Wasaidie wageni wajisikie wako nyumbani. Jaribu kuiona sehemu yako na yote unayotoa kwa mtazamo wao. Mambo kama vile kuruhusu kuingia mapema na kuweka taulo zilizokunjwa na kupangwa vizuri yanaweza kuweka tofauti kati ya ukadiriaji mzuri wa jumla na ukadiriaji bora.
- Wasiliana. Wajulishe wageni kwamba wanaweza kuwasiliana nawe au mwenyeji mwenza wako wakati wowote. Weka mipangilio yako ya arifa ili uarifiwe wageni wanapotuma ujumbe.
Zingatia mvuto wa tangazo lako
Kusasisha mara kwa mara ukurasa wa tangazo lako kunaweza kukusaidia kuwavutia wageni sahihi kwenye sehemu yako.
Picha nzuri huvutia umakini, husaidia kuweka matarajio dhahiri na kuwapa wageni uhakika zaidi wa kuweka nafasi kwenye nyumba yako. Fikiria kusasisha picha za tangazo lako ili kukusaidia kufikia hadhi ya Mwenyeji Bingwa.
- Panga picha zako. Zingatia kupata picha zinazoonyesha maelezo ya kipekee ya nyumba yako, vistawishi maarufu na vipengele vya ufikiaji. Piga picha ya kila chumba na sehemu ambayo wageni wanaweza kutumia kutoka pembe mbalimbali.
- Pakia picha za mlalo na zenye mwanga wa hali ya juu. Picha zinapaswa kuwa angalau pikseli 800 kwa pikseli 1,200. Mafaili makubwa ni bora zaidi, hadi takriban megabaiti 10.
- Tumia mtaalamu. Zingatia kuajiri mpiga picha mtaalamu ili akusaidie. Airbnb inaweza kukuunganisha na mtaalamu katika miji mahususi duniani kote.
- Unda ziara ya picha. Nyenzo ya Airbnb hupanga kiotomatiki picha zako zilizopakiwa kulingana na chumba ili kuwasaidia wageni waelewe mpangilio wa nyumba yako. Unaweza kusogeza, kuondoa na kuongeza picha, uweke maelezo kwenye kila chumba na uandike maelezo mafupi kwa kila picha.
Kile ambacho tangazo lako linasema ni muhimu kama jinsi linavyoonekana. Kichwa cha tangazo lako, maelezo na vistawishi vinatoa fursa zaidi za kuwavutia wageni na kuweka matarajio ya wazi ya ukaaji wao.
- Jumuisha kichwa kifupi cha tangazo kinachotoa maelezo. Hakikisha kwamba kichwa cha tangazo lako kinatoa mtazamo wa kipekee ulio sahihi wa nyumba yako na mazingira. Kwa mfano, "Studio tulivu karibu na Uffizi" kinaonyesha kwa maneno machache kwamba eneo hilo ni fleti yenye utulivu, iliyoko katikati huko Florence, Italia.
- Maelezo dhahiri na thabiti ya tangazo huwa na mwelekeo wa kufanya vizuri zaidi. Jumuisha maelezo halisi ambayo yanaelezea kile ambacho wageni wanaweza kutarajia kuona, kusikia na kupata kwenye eneo lako. Kwa mfano, unaweza kusema ua wa nyuma umejengewa uzio na kuna nafasi ya kutosha ya watoto na wanyama vipenzi kucheza.
- Weka kila kistawishi unachotoa. Zingatia vistawishi maarufu ambavyo unaweza kuweka au kuboresha, kama vile kuondoa kisanduku cha funguo na badala yake kuweka kufuli janja au kuboresha Wi-Fi yako. Vistawishi maarufu ambavyo wageni wanatafuta ni pamoja na huduma ya kuingia mwenyewe, Wi-Fi, mashine ya kufua, mashine ya kukausha, televisheni au televisheni ya kebo na eneo la kuchomea nyama.***
*Kulingana na mapato ya wastani kwa Wenyeji Bingwa na wasio Wenyeji Bingwa kuanzia Oktoba 2023 hadi Oktoba 2024.
**Kulingana na takwimu za ndani za Airbnb kufikia tarehe 7 Oktoba, 2024.
****Kulingana na data ya Airbnb inayopima vistawishi vilivyotafutwa mara nyingi zaidi ulimwenguni kote kuanzia tarehe 1 Januari hadi tarehe 30 Juni, 2024.
Unadhibiti bei yako na mipangilio mingine nyakati zote. Matokeo yako yanaweza kutofautiana.
Wenyeji walilipwa kwa ushiriki wao katika mahojiano.
Vidokezi vya kukaribisha wageni vinadhibitiwa na sheria za eneo husika.
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.