Kupata mafanikio wakati ni polepole
Hata matangazo maarufu zaidi yana vipindi vya utulivu vyenye nafasi chache zinazowekwa. Hizi ni baadhi ya njia ambazo unaweza kutumia zana za kukaribisha wageni za Airbnb ili kusaidia kuvutia wageni wakati wa nyakati za polepole.
Weka bei yenye ushindani
Kurekebisha bei yako mara kwa mara kunaweza kukusaidia kudumisha ushindani. Fikiria kufanya yafuatayo kwenye ratiba inayokufaa:
- Weka bei mahususi ya wikendi. Ikiwa unatoa bei hiyo hiyo kila usiku, unaweza kuweka bei tofauti kwa siku za wiki kuliko kwa usiku wa Ijumaa na Jumamosi. Kubadilisha bei kulingana na usiku kunaweza kusaidia kuongeza nafasi unazowekewa.
- Linganisha matangazo yanayofanana nayo. Matangazo yenye bei ya chini kuliko matangazo yanayofanana nayo yaliyo karibu huwa kwenye nafasi ya juu katika matokeo ya utafutaji. Fikiria kurekebisha bei yako ya kila usiku ukilinganisha na matangazo yaliyowekewa nafasi na ambayo hayajawekewa nafasi katika eneo lako.
Nenda kwenye kalenda ya tangazo lako na uchague mwachano wa tarehe hadi siku 31 ili uone bei za wastani za matangazo yanayofanana kwenye ramani ya eneo lako. Sababu zinazoamua ni nyumba gani zinazofanana ni pamoja na eneo, ukubwa, vipengele, vistawishi, ukadiriaji, tathmini na matangazo mengine ambayo wageni wanavinjari huku wakizingatia yako.
"Mimi hufuatilia matangazo yanayofanana na yangu ili niweze kuhakikisha kuwa nina bei ya ushindani," anasema Katie, mwanachama wa Bodi ya Ushauri ya Wenyeji na Mwenyeji Bingwa huko Palm Springs, California. "Ni muhimu kuwa na uwezo wa kubadilika wakati wa mahitaji ya chini ikiwa kweli unataka kuwaleta watu kwenye tangazo lako."
Vutia ukaaji wa muda mrefu na mfupi
Mapunguzo kwa ajili ya ukaaji wa usiku saba au zaidi yanaweza kusaidia kuboresha nafasi yako kwenye utafutaji na kupunguza idadi ya wageni wanaoingia na kutoka, wakati ukaaji wa muda mfupi unaweza kusaidia kujaza nafasi katika kalenda yako.
- Weka punguzo la kila wiki. Wageni wanaona wito maalumu katika matokeo ya utafutaji na kwenye ukurasa wako wa tangazo kwa mapunguzo ya asilimia 10 au zaidi. Bei yako iliyopunguzwa inaonekana kando ya ile yako ya awali, ambayo imepigwa kistari.
- Punguza kima cha chini cha safari yako. Unaweza kuweka kima cha chini cha safari yako mahususi kwa siku ya wiki. Ikiwa mahitaji ni makubwa wakati wa wikendi, unaweza kuruhusu ukaaji wa usiku mmoja katikati ya wiki lakini sio wakati wageni wanaweka nafasi ya Ijumaa au Jumamosi usiku.
"Wakati wa vipindi vya polepole, hakika nitapunguza ukaaji wangu wa chini wa usiku na hiyo hunisaidia kuwavutia watu ambao labda wanakuja tu kwa usiku kadhaa," anasema Felicity, Mwenyeji Bingwa huko Sydney, Australia.
Boresha picha na kutoka
Kusasisha maelezo ya tangazo lako husaidia kuweka matarajio dhahiri na kuwapa wageni uhakika zaidi wa kuweka nafasi kwenye nyumba yako, hasa wakati wa vipindi vya polepole.
- Unda ziara ya picha. Nyenzo ya Airbnb hupanga kiotomatiki picha zako zilizopakiwa kulingana na chumba ili kuwasaidia wageni waelewe mpangilio wa nyumba yako. Unaweza kusogeza, kuondoa na kuongeza picha, uweke maelezo kwenye kila chumba na uandike maelezo mafupi kwa kila picha.
- Weka maelekezo dhahiri ya kutoka. Eleza kile ambacho ni muhimu kwa wageni kufanya kabla ya kuondoka, kama vile kufunga. Mtu yeyote anaweza kuyasoma kabla ya kuweka nafasi na wageni wengi zaidi wanaweka nafasi kwenye matangazo yaliyo na maelekezo ya kutoka. Wageni wametuambia wanapendelea orodha fupi ya kutoka, kwa hivyo fikiria kuweka majukumu machache kabisa.
Jiunge na Kilabu ya Wenyeji wa eneo husika
Mamia ya Vilabu vya Wenyeji ulimwenguni kote huwasaidia wenyeji wa Airbnb kuungana na kufunzana. Tumeona kwamba wanachama wa vilabu hivi vya mahali husika hupata mapato mara mbili kuliko wenyeji ambao si wanachama wa kilabu,* na wana uwezekano wa kuwa Wenyeji Bingwa karibu mara tatu.**
Shughuli maarufu za kilabu zinajumuisha:
- Kubadilishana vidokezi vya kukaribisha wageni ambavyo vinaweza kusaidia kuongeza mapato
- Kujadili kanuni za ukodishaji wa muda mfupi
- Kushiriki huduma za kuaminika za mahali husika, kama vile wafanya usafi na mafundi bomba
- Kuhudhuria hafla za kipekee za kukuza mtandao
*Kulingana na takwimu za ndani za Airbnb, unapolinganisha wastani wa mapato na ukadiriaji wa wastani wa wanachama wa Kilabu cha Wenyeji cha Airbnb ulimwenguni dhidi ya idadi nzima ya wenyeji ulimwenguni kuanzia Septemba 2022 hadi Septemba 2023. Data ya mapato inatofautiana kulingana na mahali, msimu na aina ya tangazo.
**Kulingana na data ya ndani ya Airbnb kuhusu hadhi ya Mwenyeji Bingwa kwa wenyeji waliojiunga kuanzia Julai 2023 hadi Julai 2024.
Unadhibiti bei yako na mipangilio mingine nyakati zote. Matokeo yako yanaweza kutofautiana.
Wenyeji walilipwa kwa ushiriki wao katika mahojiano.
Vidokezi vya kukaribisha wageni vinadhibitiwa na sheria za eneo husika.
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.