Vidokezi vya kukaribisha wageni wenye mahitaji ya ufikiaji

Weka vipengele mahususi vya nyumba yako ili kuwasaidia wageni kuweka nafasi wakiwa na uhakika.
Na Airbnb tarehe 7 Apr 2021
Imesasishwa tarehe 2 Des 2024

Wageni walio na mahitaji ya ufikiaji wanataka kujua jinsi nyumba inavyoweza kuwafaa kabla ya kuweka nafasi. Wanaweza kuchuja matokeo ya utafutaji ya Airbnb kwa ajili ya vipengele mahususi, kama vile ufikiaji usio na ngazi na maegesho ya walemavu.

Nyumba zilizothibitishwa kuwa zinafaa kwa watumiaji wa viti vya magurudumu pia zinaangaziwa katika Aina ya Zinazofikika. Ili kustahiki, nyumba yako lazima iwe na ufikiaji wa mlango usio na ngazi, angalau chumba kimoja cha kulala na bafu lenye marekebisho kama vile vyuma vya kujishikilia au kiti cha kuogea.

Ni muhimu kutoa taarifa iliyo wazi na sahihi kuhusu nyumba yako. Hivi ni baadhi ya vidokezi vya kuunda sehemu ya kuvutia ambayo wageni wenye mahitaji ya ufikiaji wanaweza kuiwekea nafasi wakiwa na uhakika.

Weka vipengele vya ufikiaji kwenye tangazo lako

Vipengele vinavyoweza kulisaidia eneo lako lionekane ni pamoja na:

  • Maegesho ya walemavu
  • Kijia chenye mwangaza kinachoelekea kwenye mlango wa mgeni
  • Ufikiaji usio na ngazi unaoelekea kwenye mlango wa mgeni
  • Ufikiaji wa vyumba usio na ngazi
  • Milango yenye upana wa zaidi ya inchi 32 (sentimita 81)
  • Bafu lisilo na ngazi
  • Vyuma vya kujishikilia vya choo na/au bafu
  • Kiti cha kuogea
  • Kifaa cha kumwinua mtu kinachoning'inia darini au kinachosogezwa
  • Kifaa cha kumwinua mtu kwenye bwawa la kuogelea au beseni la maji moto

Vipengele vyote vya ufikiaji vinatathminiwa kulingana na miongozo ya ufikiaji ya Airbnb kabla ya kuchapishwa kwenye tangazo lako. Ikiwa kipengele hakikidhi miongozo au hakijaonyeshwa wazi kwenye picha, tunaweza kukuomba upakie picha tofauti au uondoe kipengele hicho kwenye tangazo lako.

Kushiriki picha nyingi za kila chumba huwasaidia wageni kuamua iwapo nyumba yako inakidhi mahitaji yao.

  • Andika maelezo mafupi ya kila picha. Kwa mfano, maelezo ya picha ya bafu yanaweza kuongeza maelezo: "Hili ndilo bafu pekee katika nyumba lililo na ufikiaji usio na ngazi. Choo na bafu vina vyuma vya kujishikilia."

  • Piga picha kutoka pembe nyingi. Kwa mfano, picha za bafu zinaweza kuonyesha eneo la kila chuma cha kujishikilia na kijia kipana, tambarare kwenye sakafu ili kufikia choo na bafu.

Pata maelezo zaidi kuhusu kupiga picha vipengele vya ufikiaji

Wasaidie wageni wajisikie wamekaribishwa

Wape wageni maelezo wanapokutumia ujumbe kuhusu vipengele vya ufikiaji vya nyumba yako. Kuuliza na kujibu maswali machache tu kunaweza kuleta mabadiliko makubwa.

Mifano ya vianzisha mazungumzo muhimu:

  • Una maswali gani mahususi kuhusu nyumba?
  • Ninaweza kufanya nini ili kufanya ukaaji wako uwe wenye starehe zaidi?

Jitahidi kadiri uwezavyo kukubali maombi yanayofaa, kama vile kufanya iwe rahisi kusogea kwenye sehemu yako. Fikiria iwapo mabadiliko madogo yanaweza kusaidia kuwafanya wageni wahisi wamekaribishwa. Mawazo machache:

  • Sogeza fanicha ili kuunda vijia pana zaidi kupitia vyumba na sehemu za wazi.
  • Weka vifaa vya nyumbani kama vile taulo na vyombo katika maeneo ambayo ni rahisi kufikia.
  • Ondoa vizuizi kwenye soketi za umeme.

Kumbuka kwamba si maeneo yote yatakayofaa wageni wote, iwe wana mahitaji ya ufikiaji au la. Hata hivyo, huwezi kukataa nafasi iliyowekwa kwa sababu mtu ana ulemavu, kama ilivyobainishwa katika Sera yetu ya Kutobagua. Pia huwezi kutoza ada ya mnyama kipenzi kwa wanyama wa huduma, ambao hawachukuliwi kuwa wanyama vipenzi.

Unda kitabu cha mwongozo ambacho ni jumuishi

Kitabu chako cha mwongozo ni fursa ya kuonyesha ukarimu wako na jiji lako kwa kushiriki vidokezi vya eneo lako. Unaweza kuweka mapendekezo ya migahawa, kutazama mandhari mbalimbali na shughuli za nje. 

Unapounda kitabu chako cha mwongozo, fikiria kile ambacho wasafiri wenye mahitaji ya ufikiaji wanaweza kutafuta. Kwa mfano, unaweza kutambua migahawa iliyo na vijia vyenye miteremko, vijia vya kutembelea vilivyo na lami na vivutio vilivyo na viti vinavyofikika. Unaweza pia kushiriki taarifa kuhusu usafiri wa umma.

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Airbnb
7 Apr 2021
Ilikuwa na manufaa?