Andaa sehemu yako
Sehemu ya kukaa ya nyota tano huanza kwa kufuatilia vitu kwa kina kwenye sehemu yako. Nyumba inayovutia wageni inaweza kukuletea tathmini zako za kwanza nzuri.
Kuwa mwangalifu kuhusu kufanya usafi
Wenyeji waliofanikiwa wanapendekeza kufanya mambo haya matatu ili sehemu yako iendelee kung'aa:
Weka umakini kwenye maeneo yanayotumika sana. Futa kaunta, safisha mifereji ya maji na ujaze chupa za sabuni. Hakikisha hakuna nywele zilizobaki.
Acha hewa izunguke katika kila chumba. Fungua madirisha, futa vumbi na usafishe sakafu zote, ikiwemo chini ya samani. Tandika vitanda kwa mashuka safi na utoe mataulo safi kwa kila mgeni.
- Unda orodha kaguzi ya wageni. Fuata utaratibu uleule kabla ya kila mgeni kuingia ili kuepuka kupuuza chochote.
"Niliweka saa sita kati ya nafasi zilizowekwa ili tuweze kufanya usafi wa kina," anasema Daniel, mwanabodi wa Bodi ya Ushauri ya Wenyeji na Mwenyeji Bingwa katika Visiwa vya Kanari, Uhispania. "Sehemu lazima iwe kama inavyoonekana kwenye tangazo lako la mtandaoni."
Kuweka vitu vya msingi
Wageni wanatarajia sehemu yako iwe na vistawishi muhimu. Hivi ni:
- Karatasi ya choo
- Sabuni (ya mikono na mwili)
- Taulo moja kwa kila mgeni
- Mto mmoja kwa kila mgeni
- Mashuka kwa kila kitanda cha mgeni
Wasaidie wageni wajisikie nyumbani kwa kutoa vitu vinavyofaa katika kila chumba, kama vile:
Jiko
- Mipangilio ya meza kwa idadi yako ya juu ya wageni
- Mashine ya kutengeneza kahawa, birika la chai, sufuria na vikaango na vyombo vya kupikia
- Chumvi, pilipili na mafuta ya kupikia
- Sabuni ya vyombo, rafu ya kukausha na nguo au taulo za karatasi
Sebule
- Viti kwa ajili ya idadi yako ya juu kabisa ya wageni
- Runinga yenye huduma ya kutazama maudhui mtandaoni
- Mwongozo wa nyumba wenye maelekezo ya jinsi ya kutumia vifaa
Bafu
- Mataulo ya mikononi na kanyagio la bafuni
- Brashi ya chooni na planja
- Shampuu, kondishena na kikausha nywele
Chumba cha kulala
- Vifuniko vya madirisha na meza zilizo kando ya kitanda zilizo na taa
- Droo au viango vya nguo na nafasi ya mizigo
- Blanketi ya ziada na feni au kipasha joto kwenye chumba
Ukishapangilia sehemu yako, lala humo usiku mzima au uwaombe marafiki wakae kisha watoe maoni. Utaelewa haraka kile kinachokosekana.
Kuweka vitu vya ziada
Wageni hufurahia Wenyeji wanapozingatia maelezo ya kina na kutoa vitu vya ziada ili kufanya ukaaji wao uwe wa starehe zaidi. Hizi zinaweza kujumuisha plagi za sikio, pamba, michezo ya ubao, adapta za umeme na kitu chochote mahususi kwa eneo lako, kama vile mwavuli au mataulo ya ufukweni.
Wenyeji wengi wenye uzoefu wanasema kwamba wanapenda:
- Toa zawadi ya ukaribisho. Toa ujumbe ulioandikwa kwa mkono, kikapu cha vitu vya mahali husika au kitu cha kusherehekea tukio maalumu.
- Unda hali ya starehe kwa kutumia mapambo. Fikiria kuhusu kile kinachokusaidia kupumzika wakati unasafiri. Sanaa ya ukutani, mimea, na mito ya kutupa inaweza kuongeza starehe na haiba.
- Chapisha mwongozo wa nyumba. Weka mwongozo ambapo wageni wataupata kwa urahisi, kama vile kwenye kaunta.
- Angazia vipengele maalumu. Katika maelezo ya tangazo lako, kumbuka chochote unachotoa ambacho kinakidhi mahitaji fulani, kama vile sehemu mahususi ya kufanyia kazi au vipengele vya ufikiaji.
"Nina kitanda cha mtoto cha kusaifira, kiti cha juu, na vitabu na vitu vya kuchezea," anasema Elsie, Mwenyeji huko Nashville, Tennessee.
Ikiwa unataka vidokezi zaidi na hujawekewa nafasi ya kwanza, unaweza kupata mwongozo wa ana kwa ana kutoka kwa Mwenyeji Bingwa. Ni Wenyeji wenye ukadiriaji wa juu na wenye uzoefu mkubwa kwenye Airbnb.
Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.