Wasiliana kwa ufanisi

Tuma taarifa kwa wageni katika nyakati muhimu.
Na Airbnb tarehe 22 Feb 2024
Inachukua dakika 2 kusoma
Imesasishwa tarehe 22 Feb 2024

Kuwasiliana kwa uwazi na kwa haraka na wageni kunaweza kusaidia kupata ukaaji mzuri na kuhimiza tathmini nzuri. Tumia vidokezi hivi ili kuongoza njia yako.

Kuanza na mambo ya misingi

Jinsi unavyowasiliana na wageni husaidia kuweka mwelekeo wa ukaaji wao. Jitahidi kadiri uwezavyo:

  • Patikana. Washa kipengele cha arifa ili upokee na kujibu ujumbe wa wageni haraka. Annette, Mwenyeji jijini San Francisco, anasema kwamba hata kwa matatizo madogo, anawaomba wageni "wasiliana nasi mara moja na tutayashughulikia."

  • Kuwa mwazi. Onyesha kwa usahihi kile ambacho wageni wanapaswa kutarajia. "Kile unachowaambia wageni wako watakipata na kile wanachokikuta wanapowasili vinapaswa kulingana," anasema Daniel, Mwenyeji huko San Francisco.

  • Kuwa wazi. Waulize wageni jinsi unavyoweza kuwasaidia wajisikie huru na kukaribishwa. "Kutakuwa na mambo ambayo sisi kama Wenyeji hatutarajii," anasema Sadie, Mwenyeji Bingwa huko Santa Fe, New Mexico.

  • Kuwa mwenye kujali. Jinsi unavyoshughulikia tatizo kunaweza kuacha mvuto wa kudumu. "Unaweza kubadilisha hali ngumu kuwa uwekaji nafasi mwingine ikiwa utaishughulikia kwa usahihi, kwa kuonyesha huruma na kufanya kazi haraka ili kuitatua," anasema Felicity, mwanabodi wa Bodi ya Ushauri ya Wenyeji na Mwenyeji Bingwa huko New South Wales, Australia.

Kutuma ujumbe katika nyakati muhimu

Tarajia kile ambacho wageni wanahitaji kujua ili kutoa huduma nzuri na kupunguza maswali, hasa katika nyakati hizi:

  • Maulizo au ombi la kuweka nafasi. Jibu ndani ya saa 24 wageni wanapowasiliana nawe. 

  • Uthibitisho wa kuweka nafasi. Tuma ujumbe wa "asante kwa kuweka nafasi" ili kuwasiliana na kuwajulisha wageni kwamba unapatikana ili kujibu maswali yoyote.

  • Kuwasili. Wakumbushe wageni siku moja au mbili kabla ya kuwasili mahali wanapoweza kupata maelekezo yako ya kuingia kwenye programu na ushiriki maelezo yoyote muhimu kuhusu kuingia ndani. Uliza jinsi kila kitu kinavyoendelea ndani ya siku moja ya kuingia.

  • Kuondoka. Tuma ujumbe muda mfupi baada ya kutoka ukiwashukuru wageni na kuwaomba waandike tathmini. Watolee tathmini mapema kadiri utakavyoweza.

Kufanya ujumbe wako utumwe kiotomatiki

Kuwa na kiwango kizuri cha kutoa majibu hulisaidia tangazo lako lionekane kwenye orodha ya juu katika utafutaji wa wageni kwenye Airbnb. Tumia vipengele hivi kutarajia na kujibu maswali ya kawaida:

  • Majibu ya haraka. Katika kikasha chako, chagua kutoka kwenye orodha ya violezo, au uandike na uhifadhi yako mwenyewe. Utaongozwa kufanya haya yawe mahususi kwa kutumia misimbo mifupi inayojaza maelezo ya wageni, nafasi iliyowekwa na tangazo.
  • Ujumbe ulioratibiwa. Wageni wanapokea ujumbe huu kiotomatiki katika nyakati fulani ukiwa na taarifa muhimu kwa ajili ya ukaaji wao. Unaweza kufanya ujumbe huu uwe mahususi kwa kutumia misimbo mifupi pia.

Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Airbnb
22 Feb 2024
Ilikuwa na manufaa?